SHINYANGA:Wanafunzi wa Kike tu KUPAGAWA na MAPEPO Tafsriri yake nini

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,722
Juzi ITV walionyesha tukio la kusikitisha wanafunzi wa kike shule moja Kijiji cha MASCUT huko shinyanga wakipagawa mapepo hovyo huku wavulana wakigeuka wachungaji kuyakemea.
Waalimu wanashauri shule ifungwe,
Masomo yamesimamishwa siku mbili,
Hili tukio sio la kwanza mashuleni...

NINI TAFSIRI YA TUKIO HILI

1:Mapepo yanauswahiba na wanawake? Kwa nini wanafunzi?
2:Wanakijiji hawapendi watoto wao wa kike waende shule?
3:Uchawi vijijni ni kikwazo cha elimu?
4:Ikithibitika kuna wazazi wako nyuma ya hayo matukio, Suluhisho ni adhabu kwao au wajengewe uwezo wa kubadilika fikra zao?
5:Kwa nini ikitokea Mlipuko wa jumuia wa mapepo mara nyingi huwa ni Shuleni?
6:pangekuwa hakuna imani za kidini tatizo hilo lingetulizwaje kitaalamu?

Matukio kama haya huwa yanatuaibisha sisi watu wa vijijini...
 
hii ishu inaonekana inafanywa na wazazi wa hao watoto coz inasemekana wanataka watoto wasisome waolewe tu kwa nini hayo mapepo yabague wakike tu? ingawa wengine wanasema matukio kama haya hutokea kwa shule za mademu watupu but mbona hiyo shule ni mchanganyiko
 
Back
Top Bottom