Comment yako nzuri kwa matumizi ya baadae na inafaa kwa ajili ya ku-screen shot kwa kumbukumbu ya baadae, upiga mulemule maana vijana wengine huangalia madhari ya mji au huduma zitakazoweza kuwafanya wake eneo hilo comfortably pasipokuangalia changamoto zilizopo na kuzitafutia mradi.
Kuna mdau amesema Shinyanga pa hovyo hakuna huduma za chakula labda mchana, kwa kauli hii tayari wazo la biashara limepatikana kwa mtu kuanzisha baba lishe ila baada ya kufanya uchunguzi wa kwanini mchana kuna chakula alafu usiku magumashi
Inaonekana sasa kumbe kuna usimba na yanga katika kutoa hoja!Shinyanga na Tabora pote ni semi desert climate iwaje unasema Shinyanga pakame
Je Tabora na Shinyanya wapi pako karibu na Ziwa Vickitoria Hujui maeneo ya karibu na water bodies yanapata mvua nyingi zaidi through out the year
Tabora na Shinyanga pote pamekaa kizee kizee kabisa Tena Shinyanga ianazidiwa na baadhi ya wilaya zaka
Tabora na penyewe ipamekaa kimagumashi tu Mzunguko wa pesa pote huko Tabora na Shinyanga Mdogo
Labda ungeuliza wilaya zake Kahama Na Nzega ndio zina future mbeleni
Sent using Jamii Forums mobile app
Mada ni tabora mjini na shy town achana na kahama na mwaduiTaa ya kuongozea magari hata kahama ipo wala co ajabu,,,Shinyanga wamewekewa rami sio chin ya 50 kilometres i think,, taa za barabara mpya na bado wanaenderea kuweka, tabora je?
Hebu nitajie viwanda vitatu tu mlivyonavyo huko ubangini?? Shinyanga nirienda napajua na tabora nirishawai kwenda.
Post ya juu naongeza na kiwanda cha bati kirichoko kahama,,,tabora je mnacho??
Nitajie viwanda vitatu jomba!
Sikubaliani na wewe, labda kwa sababu huijui Tabora. Ukweli ni kwamba mji wa Tabora ni mkubwa kuliko Shinyanga na unaendelea kupanuka kwa kasi. Tatizo la Tabora ni kujengwa sehemu yenye majimaji mvua ikinyesha hutapatamani. Ule mji kuna roho ya umaskini ndio maana hakuna tajiri anayefamika nchini kwamba ni wa Tabora. Wakazi wengi wa Tabora ni watu wa kawaida. Ule mji hauna mzunguko wa fedha ni kama kijiji cha maendeleao tu. Kama wewe una mtaji wako na unataka ukawekeze Tabora nakupa pole kwa sababu hautapiga hatua kamwe maana pale pana roho ya umaskini !Vichaa na vijicho, hicho kizazi kilishapita.
Sasaiv Tbr ni mji wa tofauti sana.
Zamani miaka ya 70'/80' hayo unayosema yalikuwepo na yalitokana na vijana kupendelea sana kutumia'msubha' ndiyo uliowafyetua akili na bhange la Tbr hata Jamaica wanalijua!
Me kuna watoto zangu wanaishi na kufanyakazi huko, hivyo huenda mara kwa mara kutembelea wajukuu zangu huko.
Tabora ni pazuri na ni mji wa kawaida wenye kubeba sifa zilezile kama za miji mingine hapa Tz.
Lakini ukitaka kulinganisha na Shinyanga,Tabora ni pazuri zaidi na mzunguko wake wa pesa ni mkubwa.
Sent using Jamii Forums mobile app
Ni mara ya pili nausikia huo mgogoro wa serikali kwenye tumbaku wanagombania nini kwani mkuu?Tabora ni pazuri by far, gata population tabora mjini ni watu around 230,000 wakati shinyanga mjini ni 170,000.
Mji wa Tabora ni mkubwa kuliko mji wa Shy, tatizo la Tabora mjini ni huo uislam ambao ndio unaleta uswahili.
Of course ugomvi wa serkali na makampuni ya tumbaku utapunguza sana mzunguko wa hela pale mjini, kwani wakulima wa tumbaku, japo ni kwa msimu, ni watu wanaoongeza sana mzunguko wa pesa.
Future ya baora pia ni bright, barabara ya kwenda itigi ikiisha, barabara ya kwenda kigoma na mpanda nazo zikiwa na lami, na bado barabara ya kutoka mbeya ambayo itachelewa sana kuwa lami yote, tabora patabadilika na kuwa hub ya huo ukanda
Shinyanga hapawezi kukua kwa kasi ya tabora, tayari pameshamezwa na kahama na watu wa pale wanategema sana kahama na mwanza kwa mahitaji, wafanyabiashara wa kati wa shinyanga wanapakimbia, wengi wamekimbilia igunga na tabora mjini.
Watu wa tabora soko lao kubwa ni tabora mjini, so biashara za tabora mjini zina uwezo wa kukua haraka kuliko shy, shinyanga watu wanaenda kahama, bariadi na mwanza.
Kwa hali ya hewa tabora ni better kiliko shinyanga, shida ya maji soon itakwisha mara maji ya lake victoria yatakapofika hapo.
Kama unafkkiria biashara, au kuishi, i d advise you kwenda tabora, you wont regret
Sent using Jamii Forums mobile app
Acha kufananisha shinyanga na tabora,,,ukiachilia mbali shy mjini,,kwa kahama tu hafui dafu tabora yako sembuse shy mjin!
Tabora mzunguko wa pesa ni mdogo,,watu wake hawana pesa, hutangatanga miji mingine kutafuta maisha,, bora hata ya singida pamechangamka alakini co unyamwezn
Niriwahi kutembelea shinyanga nikajionea, kwakweri uwezi fananisha na tabora japo muzunguko wake co mkubwa saana.
Shinyanga
Alimasi
Zahabu
Taa za barabarani
Rami kila kona
Viwanda vya pamba
Kiwanda cha juice, soda na maji
Kwanda cha pastik
Kiwanda cha gesi/Mihan
Kiwanda cha nyuzi
Hospitali ya mkoa na rufaa imejengwa virevire
Mashule, madispensary kibao jombaa.
Tabora,
Mkaa
Asali
Maembe
Maneno maneno sanaa,, fitina,,kwendeana kwa waganga kwa waco na imani.
Kwanin kinondon icwe juu more than kahama! Sabab yote ile ni dar moja pua na mdomo yani imo ndani ya jij la dar,,ukilinganisha na kahama ilioko mbari na mkoani shinyanga takribani 2hrs.,,,mfano jij la mwanza natambua ndilo jij la pili kwa ukubwa Tanzania na la pili kwa mzunguko wa pesa,,ndan ya jij la mwanza kuna wilaya mbiri za, nyamagana na ilemela ivyo uwezi sema nyamagana mzunguko wake ni mkubwa kuliko kahama wakati lile lote ni jiji.
Kuna wakati nilikua Karema, moja kati ya sehemu wamapolima Sana mpunga na mahindi na hawatumii mboleaHawa jamaa ni hatari sasahivi wameshafika hadi lukwa jamaa hawafai kabisa.
Sent using Jamii Forums mobile app
Igunga vs nzega nani mshindi?Sikubaliani na wewe, labda kwa sababu huijui Tabora. Ukweli ni kwamba mji wa Tabora ni mkubwa kuliko Shinyanga na unaendelea kupanuka kwa kasi. Tatizo la Tabora ni kujengwa sehemu yenye majimaji mvua ikinyesha hutapatamani. Ule mji kuna roho ya umaskini ndio maana hakuna tajiri anayefamika nchini kwamba ni wa Tabora. Wakazi wengi wa Tabora ni watu wa kawaida. Ule mji hauna mzunguko wa fedha ni kama kijiji cha maendeleao tu. Kama wewe una mtaji wako na unataka ukawekeze Tabora nakupa pole kwa sababu hautapiga hatua kamwe maana pale pana roho ya umaskini !
Shinyanga ni mji mdogo kwa Tabora ila una baadhi ya watu wenye uwezo mkubwa kuliko Tabora na pale shughuli za kiuchumi ni zaidi ya Tabora ndio maana kuna viwanda vingi pale kuliko Tabora. Kwa ujumla Shinyanga kuna roho ya utajiri kama ilvyo maeneo yote ya usukumani.
Ardhi ya Shinyanga ina rutuba kuliko ile ya Tabora ambayo ni kichanga tu. Pale Sginyanga watu wanawekeza na ni rahisi kutajirika kuliko Tabora. Unaweza ukalima mpunga vijiji na ndengu yote ni mazao yanauoingiza pesa ndefu. Ndio maana Mji wa Igunga unapiga hatua kwa sababu mazingira yake yanafanana na Shinyanga kwa kuwa na mbuga zenye rutuba kuliko hicho kichanga cha Tabora.
Sent using Jamii Forums mobile app
Bila nzega Tabora ni kichaka.... Nzega inaunganisha Tabora na dunia.Kwani nzega kuna gari ambayo huwa haipiti pale?
Sema kahama ipo njiani bwana. Sema hata Tabora inajitahidi ni kati ya mikoa iliyokuwa imetengwa kipindi cha nyerere.
Sent using Jamii Forums mobile app
Shinyanga mjini hovyo sana.
Hata ukitaka breakfast hakuna sehemu insyoeleweka ukanywa chai uka enjoy.
Chakula cha uhakika ni mchana tu tena sehemu moja tu ambayo wakati mwingine pia wanapika vibaya tu.
Ni sehemu ambayo bara bara ni chafu zimejaa udongo ijapokuwa ni za lami.
Usafiri wa tax ni wa shida,wafanya biashara hii wana nyodo na waongo.Unakubaliana nae unaamka mapema kuwahi basi,ikinyesha mvua tu anazima simu.
Biashara ni ngumu sana shinyanga,nadhani ni sehemu mojawapo ngumu Tanzania.
Maji ya ziwa yapo ila wanachanganya na maji ya bwawa chafu sana la ning"hwa na kuyafanya yawe ya chumvi na mabaya sana.
Bora Tabora sana utapata hata bookshop ya kueleweka,library nzuri,taasisi za mafunzo zinazoeleweka,na bara bara safi zisizo na mchanga
Sent using Jamii Forums mobile app
Fikra zako zimetua dar.....yaani nchi nzima dar tu ndiyo mahali pa kuishi...badili mtazamo wako sasa.Nimezunguka bar maarufu shinyanga zote hakuna kitu, nimeamua kuja Level One pia pamepoaaa hatari, tupo wateja watatu.! Acheni Dar ibaki kuwa Dar kwa japo watu wa mikoani mnaiponda ila Dar ni kila kitu.! Pale Gwanzuu Tegeta ukienda hata siku za kawaida lazima uta-enjoy, sasa hapa duun hata wahudumu ndo hvyo tena. Anyway nitapita Tabora pia kupaangalia.
Siku ukizungumzia ndugu nitag Aisee, nataman kufaham Sana mkuuHili la vichaa lina sababu nyingi sana nikipata muda nitalizungumzia.
Sent using Jamii Forums mobile app
Nzega ni mji mkubwa kuliko Igunga lakini Igunga kuna matajiri wengi kuliko NzegaIgunga vs nzega nani mshindi?
Shinyanga sehemu gani ni kame?Tabora hali ya hewa safi, tatizo ni Uswahili mwiiingi na Uchawi, pia mauaji ni kitu cha kawaida hasa kwa maeneo ya pembeni, mzunguko wa pessa kawaida sana.
Shinyanga pakame mnooo, ushamba mwiiiingi na biashara hazitoki pia na kama zinatoka Wanaukabira
Wewe chura hujafika Katavi, Simiyu, na Ruvuma yani mtu aliyetoka Manyara atajiona ana afadhali.
Hapo kwenye rangi nyekundu nimetumia sekunde 30 kupaelewa nikajikuta natabasamu 😂Umasikini bana ni shida sana nenda sa hivi Shy kamwambie Jambo,Fresho,Gaki etc hio Shy ni mbaya sijui haina mzunguko wa hela kama atakuelewa then ukitoka hapo nenda Tabora kaulize ma don wa Tabora kama mji huo ni mbaya kama watakuelewa.
Cha msingi we jiangalie wapi mishe zako zitafanikishwa then zama mazima.
Mtu atakwambia mji fulani hauna Shopping malls,sijui mahotel yenye swimming pools,hauna maghorofa yenye lift then wewe binafsi jiulize hivyo vitu vilivyotajwa vinakusaidia nini binafsi?
Je uwepo au kutokuwepo kwake kuna athari zozote na mishe zako
Fanya maamuzi chap.