Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,117
- 7,169
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tabora Mjini kupitia Chama cha Wakulima (AAFP), Habiba Bunduki, amezindua kampeni zake akiahidi kuboresha maisha ya wananchi kwa kujenga barabara za juu (flyover) katika barabara za Tabora Mjini pamoja na kubadilisha mazingira ya elimu ili kuhakikisha wanafunzi wanapata fursa ya kusoma katika mazingira bora zaidi endapo atachaguliwa kuwa mbunge.