Shinyanga: Kada wa CHADEMA akamatwa na polisi!

Shinyanga: Kada wa CHADEMA akamatwa na polisi!

Ghiti Milimo

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2011
Posts
5,157
Reaction score
7,701
Kada maarufu wa CHADEMA Shinyanga mjini,Bwana Oscar Kaijage,juzi Jumamosi alikamatwa na askari polisi,na kuzuiwa kituo cha kati,na leo Jumatatu amesafirishwa kwenda Tabora,na kukabidhiwa kwa askari wa huko.
Sababu kuu ya kukamatwa,ni kuhusishwa na tukio la kumwagiwa tindikali Bwana Musa Tesha,9 Sept,2011 huko Igunga kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa Mbunge,ambapo mgombea wa CCM,bwana Peter Kafumu,alimshinda mgombea wa CHADEMA,bwana Joseph Kashinde.
Bwana Oscar,alifuatwa dukani kwake stand ya mabasi SHY mjini,mnamo saa 9 mchana ,na askari nane,ambao hawakuvaa sare.
Baada ya mazungumzo ya muda mfupi,askari hao,waliwaomba majirani wa duka hilo,nikiwemo mimi,tusogee ili tuwe mashuhuda,wanapompekua.
Hata hivyo,hawakukuta kitu chochote walichokihitaji,na kuamua kuondoka naye,kwenda kumpekua nyumbani kwake.
Nako pia,hawakuambua kitu.
Nilidokezwa na askari mmoja nifahaminiaye naye kuwa anatuhumiwa kushiriki ile issue ya tindikali Igunga.
Leo mchana,nimepata taarifa kutoka ofisi ya RPC SHY,kuwa amepelekwa Tabora,kwenda kufunguliwa mashitaka huko,Igunga/Tabora.
-----NAOMBA NISIONGEZEE NENO LOLOTE!
 
150419_355026611263437_1951252696_n.jpg

Mlianza kutembea na sumu mfukoni na sasa mnatembea na vidumu vya tindikali
 
Asante Lwakatare ushirikiano wako na jeshi la polisi unazaa matunda. Nasubiri mchoro wa Morogoro kwa hamu.
 
Kuna tetesi kuwa CCM wakishirikiana na Polisi wamepeleka Igunga Picha ya kijana anayetuhumiwa kummwagia Tindikali kada wa CCM kule Igunga na kumpatia picha hiyo yule kijana aliyemwagiwa tindikali ili iwe rahisi kumtaja pindi atakapotakiwa kufanya hivyo.

Hii ni tetesi tusubiri tuone kitakachofanyika.
 
Mwigulu kutuma vijana Ndago na kuhusishwa na utekwaji na kuteswa raia, mbona hakamatwi? Ilaaniwe ccm daima kwa matumizi mabaya ya vyombo vya dola.
 
Nonesense!

hatutarijii tofauti na hii coment yako, maana hata wewe mwenyewe ni mtuhumiwa. just a matter of time. hamuwezi kuachiwa mkitanua na kudhuru watu tu kama vile nchi haina utawala wa sheria.
 
duuuuh hivi policcm wamepania kuimaliza chadema eeeh??? Tunamtaka Mwigulu Nchemba nae afikishwe mahakamani
 
Last edited by a moderator:
Ludovick hata kama awe amehong'wa au hakuhong'wa kuwageuka waajiri wake (CHADEMA). Kama kweli haya tunayoyasikia yatakuwa yalikuwa yanapangwa na kufanywa na viongozi waandamizi wa CHADEMA, basi huyu jamaa atakuwa shahidi mzuri sana kama kigezo cha Turn States Evidence kitakuwa kinatumika ikichukuliwa kuwa hakuwa tu mfanyakazi wa CHADEMA makao makuu bali pia alikuwa rafiki wa karibu wa Mkuu wa idara ya ulinzi na Usalama ya CHADEMA, Lwakatare.

Kuna uwezekano pia akawa Discredited witness kwenye sarakasi hili.

Yetu ni macho na tutasikia mengi.
 
Hivi hawa jamaa wanafanya siasa za namna gani hizi? Kumbe migaidi imejificha katika jamii inauwa watu inajifanya miungwanaaa? Hatari sana hii
 
Makamanda kama hamhusiki msife moyo maana hakuna jambo jema lipatikanalo kirahisi kumbukeni wasira alisema 2015 hamtafika so kuweni makini kwa kila hatua mnayokanyaga
 
kumbe huondio usalama mnao sema uko imara zaid ya wa taifa,haya matukio yameanza baada ya cdm kuwa na usalama wao na kuendelea kutafuta wanao wapinga,mlianza na ulimboka alivyo kataa kundelea na mgomo.zitto alipotaka urais na kibanda alipo ondoka
 
Nduka na M23 lazima mjifikirie kwanza kabla ya kutoa opinion maana mnaonekana kama vile nyie ni vihiyo a.k.a Tabularassa
 
Back
Top Bottom