Shinyanga: Fisi avamia nyumbani kwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kishapu na kuua Mbuzi, kondoo 16

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
Katika hali isiyokuwa ya kawaida fisi amevamia nyumbani kwa Diwani wa kata ya Lagana ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga,Boniface Butondo kisha kuua mbuzi na kondoo 16.


Butondo ameiambia Malunde1 blog kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Aprili 4,2019 majira ya 10 alfajiri katika kijiji cha Lagana ambapo fisi huyo ameshambulia watoto wa mbuzi na kondoo katika nyumba ya mifugo hao wapatao 16.


“Ilikuwa majira ya saa 10 alfajiri ndipo fisi huyo alipoingia katika nyumba hiyo na baada ya kusikia makelele ya mbuzi na kondoo hao wadogo wanafamilia wakaamua na kuita majirani wazingira nyumba kwa marungu, mikuki,mawe na pia kufanya kazi ya kufumua paa juu ,wakafanikiwa kumuua majira ya saa 1 na tayari alikuwa ameshakula watatu na kuua wengine 13 na kubakiza wanne ”,ameeleza Butondo.


“Mimi ni mfugaji wa mbuzi na kondoo,hao watoto wa mbuzi na kondoo nimejengea nyumba yao,mbuzi na kondoo wakubwa nao banda lao,kwa kweli tukio hili limenisikitisha sana na limetokea wakati mimi sipo nyumbani”,ameongeza Butondo.
mbuzi (4).jpeg
 
Shinyanga mjini maeneo ya pandagichiza mida ya saa 1 na nusu usiku fisi wanaanza kulia na kurandaranda mitaani kama mbwa ...kwa wana pierre liquid wanaopenda kutembea kwa miguu baada ya kulewa wajihadhari sana
 
Shinyanga mjini maeneo ya pandagichiza mida ya saa 1 na nusu usiku fisi wanaanza kulia na kurandaranda mitaani kama mbwa ...kwa wana pierre liquid wanaopenda kutembea kwa miguu baada ya kulewa wajihadhari sana
Mwenyewe umeandika panaitwa "PANDAGI CHIZA"
maana yake tembeeni au kanyageni kwa tahadhari/vizuri so hapo ukikosea tu umeliwa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa nimegundua ni kwa nini ccm inahusishwa na fisi (fisiem)! huyo mdudu anaonekana ni mroho, mlafi na mbinafsi aliyepitiliza. Pole sana mh.diwani kwa hasara uliyoipata.
 
Back
Top Bottom