The Humble Dreamer
JF-Expert Member
- Oct 12, 2015
- 7,442
- 10,233
Mwanaume aliyetambulika kwa jina moja la Athumani amefariki dunia mara baada ya kukanyagwa na gari hilo katika stendi kuu ya mabasi ya Shinyanga, mwili wake umepelekwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Taarifa zinasema kua Basi hilo linalofanya safari zake kati ya Mwanza na Dar es Salaam lilimkanyaga Ajenti Athumani wakati akirukia kwenye Basi hilo na kisha kuangukia uvunguni mwa Basi na kukanyagwa na kufariki dunia hapo hapo.
Polisi wako pembeni wanaangalia tu.
Pia wanaoonekani pichani wakimsaidia marehemu ni wananchi wakawaida sana, mashaka yangu ni je, wana uelewa wa kutosha juu ya maambukizi ya magonjwa ama virusi pindi ikitokea ajali ilihali wenye mavazi mazuri wamesimama wakitazama kama viongozi waelekezi tu?.....
Ushauri: Hii tabia ya kurukia gari au kushuka kwenye gari wakati gari hilo likiwa kwenye motion ni hatari sana. Watu wengi hufanya hivyo ili kuokoa muda au kuonyesha wepesi ila fahamu unahatarisha uhai wako. Ni vema usubiri gari lisimame ushuke.