Shilingi ngapi hizo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shilingi ngapi hizo?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Ntemi Kazwile, May 28, 2010.

 1. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #1
  May 28, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Utajisikiaje pale unapompatia mam sap wako hela ya matumizi ya mwezi, kabulungutu kazito kidogo (kamafungwa kwenye bundles za ten ten) anazicheki halafu anauliza shilingi ngapi hizi (huku akiwa amekunja uso), bila hata kusema ahsante mume wangu... halafu wewe hapo umejikamua kinoma. TRA, pension na wenye madeni yao wamekamua, uko choka mbayaaaaaa.

  Kama ungekuwa wewe ungelijibu nini
   
 2. m

  masanja mwema Member

  #2
  May 28, 2010
  Joined: Mar 31, 2010
  Messages: 26
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 5
  unamwangalia tu na kumwacha kama alivyo!! hajui entendalo! na wala sio kosa lake la kutokuwa na shukrani!
   
 3. Mpeni sifa Yesu

  Mpeni sifa Yesu JF-Expert Member

  #3
  May 28, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  unatakiwa kumwambia, hebu lete nizihesabu kwanza, akikupatia, ndo utajua la kufanya hapo, na ndo unatakiwa kuonyesha kuwa wewe ni mwanaume baba wa nyumba...ktk nyumba si kuna kichwa cha nyumba mwanaume na wengine ni mbavu na sehemu zingine za mwili? au?
   
 4. m

  masanja mwema Member

  #4
  May 28, 2010
  Joined: Mar 31, 2010
  Messages: 26
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 5
  mimi nimekuwa nikitembea na kina dada wanne kwa nyakati tofauti tofauti, na kwa kweli kila mmmoja ana uzuri wake, maumbile na kitabia pia! wa kwanza tatizo lake ni mvutaji sigara mmoja mzuri sanaa! japo yeye anaficha ila mimi najua hilo! wa pili ni mtoto wa kawaida tu, ila anaonekana ni mwongo mwongo sana, wa tatu pia ni msichana sanaa wa sura, naposema mzuri ni mzuri kweli si utani, ubaya wake kila anapopita haishi kuitwa itwa na watu wenye pesa, wa nne ni mdada mzuri wa wastani, japo kwa sasa naye nimemgundua kuwa kuna vitu anakuwa anajificha navyo,kuna wakati niliomba simu yake niitumie na nikaona kuwa kuna kila mara anawasiliana na mijitu miwili mabazo namba zake hajazipatia majina, ninasema vile kwani nilijaribu japo kwa dak. chache kuscrol namba hizo nikaona lamost ni kila siku namba hizo zinaingia! wana jf nipeni ushauri wenu kwani kwa sasa nimefikia makamo ya kutaka kuwa na mke wa kusihi naye, je ni yupi kati ya hawa anafaa?
   
 5. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #5
  May 29, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Mi nadhani kwanza watu wakufundishe jinsi ya kuanzisha Tread humu Jf.
  Mada iliyokuwa inazungumzwa hapa ni nyingine na wewe ndani ya hiyo mada umaanzisha mjadala mwingine.
  mwanzoni kabisa mwa page ya jukwaa hili kuna sehemu imeandikwa 'post new topic' bofya hapo na utaweza kuanzisha mjadala na watu watakushauri.
   
 6. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #6
  May 29, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  mhh kwanza umeingia kinyume nyume....
   
 7. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #7
  May 29, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,839
  Likes Received: 2,000
  Trophy Points: 280
  Hutakiwi kumjibu kwa mdomo maana haitaleta maana kitu unachotakiwa kufanya tafuta avatar ya BOFLO then nenda kaimplement iwe ndio jibu lako kwake.....joke bana husije vunja ndoa. Jambo la muhimu ni kumweka chini your wife na kumweleza kiunagaubaga kipato cha na jinsi unavyostruggle kuyaweka maisha sawa...isije kuwa wife anahisi una small house somewhere else na ndo unakoacha burungutu kubwa
   
 8. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #8
  May 29, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  masanja mwema [​IMG]
  Junior Member
  Join Date Wed Mar 2010
  Posts 2

  Karibu saana! Eh! pitia haraka haraka kule mafunzoni (FAQ) ama mPM Invicible!

  @ Ntemi; unazichukua halafu unapotea mwezi mzima teh teh! NOPE; Mweleze hapo hapo tena ukikemmea hiyo tabia yake isiyokuwa na shukrani! Mtolee uvivu kabisa! Ila usimbandike vibao!
   
Loading...