Shigongo amvaa Tundu Lissu

Njaa nuksi bana usiombe.. Amegeuka leo kuwa pambe na yeye.. Si alisema ccm wamemzurumu huyuu???
 
Shigongo ni msukuma mnafiki sasa kaamua kuwa mpiga debe wa msukuma mwenzake baba Jesca apate kupewa vicent kidogo,njaa mbaya huzaa ukabila
 
Shigongo anajielewa sana. Huyo Lissu hana uzalendo hata chembe. Kabaki kumshangilia Lowassa tu!
Uzalendo upi? Lisu tokea 1998 anapigania haya makinikia iweje useme Hana uzalendo? Bunge la ndiyooo lililipitisha mikataba mibovu magufuli alikuwa ni mmojawapo leo hii kaja na blackmail apige pesa za wazungu kama mkapa mnajidai kumshangilia, kuna nini jipya? Malalamiko yapo tokea siku nyingi sana.
 
Kumbukeni Shigongo ni PhD holder!
PhD za kuiba mitihani kisha kukosa Akili kama Lipumba hazina maana bora kujinadi kuwa ni darasa la saba kama Mbunge wa Geita kuliko kujinadi usomi wakati vichwani hakuna Taaluma wala maarifa kuliko wa darasa la 7.
 
lisu kaanza zamani tokea 1998 kupinga huu wizi wa madini cha ajabu magufuli kaja 2017 kupinga kapewa sifa zote wakati kipindi cha kupitisha mikataba mibovu alikuwa ni mmojawapo wa wabunge wa CCM wasema ndiyooooo...
 
shigongo huyu. kwenye stori ya maisha yake alisema hawezi kua na akaunt kwenye mitandao ya kijamii
 
Lissu niwakuogopwa kama Ukoma
huyu Ni msaliti
unachomuogopea lissu ni nini, kaiba au kafanya nini, wa kuogopa ni hao waliotufikisha hapa mpaka sasa, uozo mfanye nyie mnaopiga na kuwaburuza viwete mnakuja kulaumu lissu, kila iitu ndio ndio, hatimae mnalaumu upinzani, kwani wao ndiobwaliosign uozo mliotufanyia, kajambe huko
 
nikwambie kitu, kijani kupita 2020 lazima roho za watu zipotezwe, na demographic itokee, manake ninavyoona kupita kwa hawa watu 2020 lazima waue na damu imwagike, hivi hivi, tukienda kihalali kijani mbona chali mapema, mtatumia ubabe wenu muue raia hapo mtaingia, omba uhai na uzima na mark my words
 
Binafsi sijawahi kumuheshimu Lissu, namlinganisha na Mchungaji Mtikila....yaani wanalazimisha kusikilizwa na watu hata kama kuna ukweli wao watapinga na kuleta hoja tofauti ili tu wapate watu wa kuwasikiliza. Huyu kijana kajimalizia ushawishi kwa jamii.
 
Mbona anajipendekeza kwa ccm? Mbona amekuwa MTU wa kutafuta kiki kwa mlango wa ccm? Ajipange upya kwani hawezi kumchalenge Lissu
 
Huyu si ndiye alikuwa anaililia CCM imlipe madeni yake. Hawezi kuwa na nongwa nao
 
Shigongo, naye anajaribu bahati yake anaweza kupata chochote.
 
Shigongo asiye na hata MB moj a ya kisheria ya mikataba ya madini anajilinganisha na Lissu nimwambie tu kuwa" tumefika hapa kwa sababu ya ccm,Waliofunga mikataba hii niccm,waliwachagua kuongoza wizara nic ccm Leo wanajivua gamba au wanafunua nyeti zao?


Wizi ,ubadhirifu Wa makada Wa ccm haujaanza leoWaziri Mkuu Mstaafu na Marehemu Ndg Edward Moringe Sokoine akiwa kwenye mkutano Wa ccm(chini ya chama kushika hatamu anasema"


....." Vijana wengi Leo wanamali zaidi kuliko wazee waliofanya kazi miaka therathini hadi arobaini. Lakini wanaiuliza serikali iwaulize hiyo Mali wameipata wapi,hivi kwa nini mzazi asimuulize mwanae Mali hii umeipata wapi?" 23/10/1983

Aliendelea kuonya zaidi kada huyu

*...ole wake kiongozi mzembe na asiye na nidhamu nitakayemkuta kiongozi Wa siasa hana usalama Wa aina yeyote,usalama wake nikuomba kudra za mwenyezi Mungu na wananchi peke take,viongozi wazembe na wabadhirifu wahesabu Siku zao". 26/3/1983

Kipindi hiki kuna chama kimoja ccm hakukuwa na Lisu makosa haya yameendrlea hadi Leo nyumba kuuzwa,Bank kuuzwa,na Viwanda vyetu kuuzwa.Ni tangu hapo hadi leo makosa yanafanywa na wanaccm waliopewa dhamana na wananchi.

Anawezaje Shigongo kuja na hoja dhaifu hizi?

Wakati Mnyika na Zitto anatimuliwa Bungeni ,serikali ya ccm ilikuwa ughaibuni na sasa imetudi kuona tunaibiwa?

Ikiwa kweli ccm imedhamilia ,leteni mikataba Bungeni ya gesi na madini tuone unaowatetea kama watatoka!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…