Shida za ndoa ( maoni ya wanaume)


for sure, wengine wana kazi na mshahara na haujulikani unafanya nini. Haki walizokuwa wanadai si pamoja na kufanya hayo?
 

inaelekea wewe umekaa kibiashara sana. Kwani haki mnazozidai sio hizo? Simtetei ila msipende kukwepa majukumu sana kama mtu wewe. Maisha ni kusaidiana na sio kuchunana. Huo sio utu!
 

Ongea nae, asijekuwa ana nyumba ndogo anahudumia wakati wewe unaumia peke yako. Tumia busara ujue ukweli wa huo mkopo kama kachukua kweli au la. Je mna tabia ya kukaa chini kila mwezio kuangalia maendeleo ya kazi zenu za mwezi mzima?
 
Khaa! hebu asikuchoshe kwa majukum ambayo si yako,mwishowe uzeeke mapema.Pole sana my ndg,dawa ya huyo mume ni kuvunja ukimya,zungumza nae kinyume na hapo ataendelea kujikausha siku zote.Asipobadilika,mpunguzie huduma mf chakula! asipokuta akikuuliza mwambie hakuna kwsbb hakuacha hela ya matumizi.Nachukia sana wanaume dizain hii.
 

Kwenye kuhudumia mgodi dady iz the head of the family, mambo mengine beijing inatawala mtatuua jamani embu tuoneeni huruma wababa,, big up kwa huyo jamaa unapopata chance tupia mzigo kwa mama nae aangaike nao,, hahaha raha
 
sishangai haya yapo tena sana.Yanaendekezwa na wanandoa wasiokaa na kuongea .

MOSI;Mnachukulia mambo kuwa rahisi tu pasipokujua mwisho wake ni urithi mbaya kwa watoto wenu.KAENI ONGEENI ILI JUKUMU LA MALEZI LIWE LENU WOTE HAO WATOTO NI WENU WOTE.

PILI;Binadamu siyo mtu wa kudumu kuna kufa .je akifa mume au mke nani mlezi?.Vip hatma ya mali zenu mnazomiliki kisiri bila kuweka wazi?

TATU; wanaume wote hawako hivyo ni malezi tu ya baadhi ya wanaume ndo yananyofanya mambo yawe hivyo.
 
Hahaha. Kama unaunga mkono mfumo wa waarabu kwa nini unataka wanawake waende shule? Kuna wanaume wanaoa wanawake wasomi halafu wanataka kuwaachisha kazi. I find that very selfish, ukizingatia angeweza kuoa mwanamke asiesoma kabisa.
 
Sasa watoto wa kwako, wanaitwa kwa jina lako, na hutaki kukopa kila saccos wasome kidhungu? Shukuru Mungu anakusifia kwa wenzie kuwa wenetu wanasoma academia. Kuna mdada kila akija kwangu anamponda mumewe hana kitu, hela haionekani sijui jamaa useless. Na huyo dada ni msomi wa MBA but proffessional jobless. Kila siku ananibadilishia magari na nna hakika ananunuliwa na mumewe. At least appreciation iwepo. (nilivyo mwizi ningekuwa mkeo watoto wakidengua kula nawaambia 'papaa is struggling kununua chakula. Dont mess this up!).
 

ahahahahahahahhaaaaaaaaaaaaaaaaa_igwe like this..lo
 
Ipo kazi kubwa anayoifanya mume wake japo hataki kuitaja hapa. Usiidharau nayo ni kazi kubwa vilevile. Baadhi ya wanaume inawashinda tena siku hizi ni wengi kwelikweli.
 

Dawa yake ni kumpikia Pilau na Kuku, akiuliza umetoa wapi hela ya kufanya hivyo mwambie wenzake wanamsaidia kutunza familia yake.
 

Mbona mkiguzwa kidogo mwaleta malalamiko??? Hayo kwetu wanaume mbona ni kama habari za asubuhi?? Sikiliza kwangu mambo yalivyo; Mke wangu alikuwa mama wa nyumbani (ingawa siku hizi hamtaki kusikia hilo)nikampatia mtaji wa kufunga kuku 450 tu, lakini kwa upande wangu nimeajiriwa na kipato changu ni kinakaribia 3M kwa mwezi. Nimejenga nyumba 2 bila hata senti ya wife, moja nimepangisha, nasomesha watoto pekee yangu, nina gari 2 moja yangu lingine la kwake. Lakini anachosema na kuwaambia ndugu zake ni kwamba simjali, simununulii mahitaji kama wengine wanavyofanyiwa na mbaya kabisa kaamua kuacha kunitayarisha chai asubuhi wakati naenda kazini ingawa vifaa vya kutayarisha chai hiyo asubuhi kwa haraka vipo mpaka naondoka yeye kalala. Ninachosema toka moyoni unaweza kupita wiki 2 bila kusemezana. Ukweli hakuna anachoingiza kwenye familia hata kuku wake hao kidogo akiuza hela hujui ameitumiaje,Je,hali ya namna hiyo nitaendelea nayo mpaka lini, sijui nitafute small house?? Anyway, hayo kwa wanaume tumeyazoea lakini likitokea kwa akina mama zetu ni kulalamika mkitusingizia kwamba sisi ndio vichwa vya nyumba
 



sawa sawa
 



kama upo hapa hapa dsm
me nakaa huku tabata kimanga
naomba nimsaidie brother kuhudumia iyo familia
wanaume tumeumbiwa matesoo kuhangaikaa..
 
inaelekea wewe umekaa kibiashara sana. Kwani haki mnazozidai sio hizo? Simtetei ila msipende kukwepa majukumu sana kama mtu wewe. Maisha ni kusaidiana na sio kuchunana. Huo sio utu!

Nimekaa kibishara haswa haswaaaaaa! Kumfuga mtu mchezoooo! Hata paka simfugi itakuwa dume zimaaaaa! NEVER!!!!!!!!!! Mimi nipo kiasili zaidi kuwa mwanamke ni wa kulelewa tuuuuu! Mi natafuta sana pesa ila kwa matumizi yangu binafsi na ndugu zangu. Mi mwanaume nikiwa namuhudumia kwa kweli heshima itakuwa hakuna!!!!

Mimi defination yangu ya mwanaume ni yule anaejiamini, na mwenye uwezo wa kukabili majukumu kunizidi. Vinginevo itamchulia kwa wasiwasi sanaa.

Hayo ya kusaidian ndo mwanzo wa kutupiwa zigo lote la majukumu kama bi dada ukabiliane nalo, sababu umeonesha uwezao wa hali ya juu kuyakabili. Ila ukiwa wazi kuwa hapa wewe dume ukiwa nyonde nyonde jahazi linazama, sababu wewe ndo tunakutegemea mwenyewe anafoulisha vitu na kufanikisha.

Kulelea mwanaume NOOOOOOOOO (Labda awe super handsome lol!)
 
Ukisikia pata potea kwenye ndoa ndiyo kama hii.
Wanaume wako wa aina mbili kuu:
A. Waliokuwa na malengo na wenye kujua nini maana ya kuwa mume
B. Wababaishaji wasiojua kuoa maana yake nini.
SIFA ZAO:
Walioko kwenye Kundi A.Hawa utawatambua toka uchumba. Wamejifunza kujitegemea mapema hata kama wana wazazi au walezi wenye uwezo wa kuwahudumia.Utawaona wanajishughulisha na shughuli mbalimbali kutegemeana na alipo. Kama ni mwanafunzi akifunga shule basi utamuona hapendi kukaa bure bila shughuli, utamuona mara anatafuta tempo au biashara ndogo ndogo na pesa yake anajua kuweka akiba na akiwa na mpenzi utamuona akiwa mkarimu wa kiasi na siyo kupitiliza.Kama ametoka familia isiyo na uwezo hafichi.Anakua muwazi sana na atakueleza ni jinsi gani anatamani ajibailishe kwa kujenga familia bora.Huyu kila afanyacho ni kwa ajili ya familia na siyo kwa ajili yake.Kama ametoka familia yenye uwezo, hatumii fedha kama chambo na pia hajionyeshi au kujigamba kuwa katoka kwenye utajiri.Mara nyingi atakua na maongezi ya kutafuta vyake na siyo kutegemea vya kwao.

Walioko kundi B. Hawa ni watata sana.Wana maneno matamu, si wachapa kazi kivile japo wanaweza kuwa na pesa na hata kukupa zawadi lukuki.Ukiona pia mwanaume anatanguliza pesa sana kwenye urafiki au mapenzi ujue mtu huyo ni kama anawekeza.Akija kuoa, atataka kuvuna,Si ajabu na mshahara wako akataka upitie account yake au umpelekee salary slip! Ukiona kakuachia mshahara basi atakutegea utunze familia na kusomesha watoto. In short anakufanya kama vile wewe ni shamba lake anavuna.Kwa kifupi mtu kama huyu ulipaswa umwepuke toka uchumba maana akikuoa mtu kama huyu utakoma na huwezi kumbadilisha.
Usiombe upate mume kutoka kundi hili ambaye katoka familia maskini.Utalia na kusaga meno\!Kila mara atakumbushia kua yeye siyo baba yako.Atakutaka wewe na watoto wako mjitegemee na mumsaidie kwani alipata shida sana.Ukimkuta ambaye hataki kukumbuka alikotoka, basi anaweza kukutelekeza akatafuta nyumba ndogo pale anapopata uwezo wa kiuchumi.
 
Don't spend or give money.spend your money to dress up and good time .umeme ukikatwa usilipe,usimwekee chakula,atabadilika.mwanaume Ana kutreat unavyotaka.Good luck you deserve better ,don't settle for that.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…