Nimekutana na changamoto hii nikifuatilia passport, naombeni ushauri

Yohimbe bark

JF-Expert Member
Sep 1, 2019
1,052
2,590
Habari magreat thinkers,

Last week nilienda immigration kufatilia passport nikiwa na kila kitu wanachotaka kama cheti cha kuzaliwa, affidavit ya mzazi na barua ya utambulisho kutoka serikali ya mtaa.

Nimefanya process zote vizuri tu ile nimeenda kwa afisa wa mwisho akawa anakagua form zangu akaona kwenye cheti changu cha kuzaliwa sehemu ya mama mzazi jina la baba yake halipo lipo jina la mama tu tatizo likaanzia hapo nikaambiwa cheti ni fake inabidi niende RITA niombe cheti kingine cha kuzaliwa, nikasema fine nimefika RITA nikaambiwa inabidi niapply online na niambatanishe leaving certificate ya form 4 au 6 na barua ya utambulisho kutoka serikali ya mtaa.

Tatizo ni kwamba leaving certificate zinaonesha nimezaliwa 1994 na nida yangu inaonesha nimezaliwa 1993 na cheti nilichoambatanisha mwanzo cha kuzaliwa immigration kinaonesha nimezaliwa 93, issue ni kwamba hata nikitafuta cheti cha kuzaliwa kingine bado kitatoka cha 94 kwasababu ya zile leaving certificate nikienda immigration wataona miaka inatofautiana na kwenye NIDA so nipo njia panda naombeni ushauri wakuu nifanyeje? mtanisamehe kwa uandishi m'bovu.
 
Kwenye hiyo affidavit umeweka maelezo Gani, Je huyo afisa uhamiaji ameisoma vizur affidavit yako,

Tafuta afisa uhamiaji mwenye uzoefu akupe maelezo sahihi, maana Kuna vijana wanekuja hapo juzijuzi bado hawajui mpango kazi
 
Hiyo affidavit hata hakuifikia mzee kwasababu ilikua mwisho wa page ila ina majina yote ya mama, na ndugu zake baadhi niliwaandika pia mkuu
 
Affidavit yako ilitosha kukamilisha makosa yaliyoko kwenye birth certificate, nasio kwenda RITA,

Tafuta afisa uhamiaji mwenye uzoefu akupe maelezo sahihi

Yani mkuu acha tuu, nilimtafuta afisa mmoja nikamueleza akaniambia haina shida hiyo issue ila niongeze nguvu akataka laki 2 nikakomaa nae mpaka nikampa laki na 30 akasema after 1 week kila kitu kitakua poa juzi nimemchek kasema bado leo nimemtext anasema issue bado ngum kwasababu wanataka cheti kingine cha kuzaliwa nimemuambia kama issue haiwezekani aniambie mpaka sasa hajanijibu.
 
Kwenye hiyo affidavit umeweka maelezo Gani, Je huyo afisa uhamiaji ameisoma vizur affidavit yako,

Tafuta afisa uhamiaji mwenye uzoefu akupe maelezo sahihi, maana Kuna vijana wanekuja hapo juzijuzi bado hawajui mpango kazi
Sahihi
 
Habari magreat thinkers, Last week nilienda immigration kufatilia passport nikiwa na kila kitu wanachotaka kama cheti cha kuzaliwa, affidavit ya mzazi na barua ya utambulisho kutoka serikali ya mtaa, nimefanya process zote vizuri tuu ile nimeenda kwa afisa wa mwisho akawa anakagua form zangu akaona kwenye cheti changu cha kuzaliwa sehemu ya mama mzazi jina la baba yake halipo lipo jina la mama tuu tatizo likaanzia hapo nikaambiwa cheti ni fake inabidi niende RITA niombe cheti kingine cha kuzaliwa, nikasema fine nimefika RITA nikaambiwa inabidi niapply online na niambatanishe leaving certificate ya form 4 au 6 na barua ya utambulisho kutoka serikali ya mtaa. Tatizo ni kwamba leaving certificate zinaonesha nimezaliwa 1994 na nida yangu inaonesha nimezaliwa 1993 na cheti nilichoambatanisha mwanzo cha kuzaliwa immigration kinaonesha nimezaliwa 93, issue ni kwamba hata nikitafuta cheti cha kuzaliwa kingine bado kitatoka cha 94 kwasababu ya zile leaving certificate nikienda immigration wataona miaka inatofautiana na kwenye NIDA so nipo njia panda naombeni ushauri wakuu nifanyeje? mtanisamehe kwa uandishi m'bovu.
Toa helaaaa
 
Pole mkuu, Kwa kupigwa
 
Nenda NIDA ukabadilishe mwaka wa kuzaliwa ili ufanane na leaving certificate ulio ambatanisha kwenye passport application yako.
Ukifika NIDA kawarushie lawama kwamba wao ndio walikosea kuweka mwaka wako wa kuzaliwa kua 1994 badala ya 1993.
Baada ya hapo watakupa form ya kufanya marekebisho kisha utalipia pesa kidogo haizidi 20k na kisha watakurekebishia mwaka ila namba na mengineyo yatabaku vilevile.
 
akawatupie lawama

Sent from my SM-G965U using JamiiForums mobile app
 
Kwenye hiyo affidavit umeweka maelezo Gani, Je huyo afisa uhamiaji ameisoma vizur affidavit yako,

Tafuta afisa uhamiaji mwenye uzoefu akupe maelezo sahihi, maana Kuna vijana wanekuja hapo juzijuzi bado hawajui mpango kazi
Affidavit skuizi haisaidii kwenye uhitaji wa documents kama hizo, labda kama angeamua kwenda mahakama ya ardhi akapate Deed Poll Certificate ambayo itakosoa mwaka wa 1994 na kuhalalisha mwaka 1993. Then hiyi ndio itakayo someka katika maisha yake yote.
 
Yani mkuu acha tuu, nilimtafuta afisa mmoja nikamueleza akaniambia haina shida hiyo issue ila niongeze nguvu akataka laki 2 nikakomaa nae mpaka nikampa laki na 30 akasema after 1 week kila kitu kitakua poa juzi nimemchek kasema bado leo nimemtext anasema issue bado ngum kwasababu wanataka cheti kingine cha kuzaliwa nimemuambia kama issue haiwezekani aniambie mpaka sasa hajanijibu.
Affidavit yako ilitosha kabisa kumaliza tatizo lako na hata kama affidavit ilikosewa , unaweza kuibadilisha ,
Na Sio kwenda RITA.

Jaribu kumuuliza wakili aliye kutengenezea affidavit hili swala , anaweza kukupa mwongozo, mzuri
 
Kwenye passport, affidavit haikubaliki. Pale inatakiwa aende na Deed Poll Certificate
 
Ndio mkuu, akaseme wao ndio wamekosea mwaka wake wa kuzaliwa badala ya 1993 wakaweka 1994
Akienda Nida wataangalia kwenye system kama ni wao Nida wamekosea basi Sio kesi , ila kama ni yenye amekosea, ajiaandae kutoboka mfukoni,

Na ndio maana sitaki aende Nida, hili swala Lina Ishia Kwa mwanasheria Tu
 
Habari magreat thinkers, Last week nilienda immigration kufatilia passport nikiwa na kila kitu wanachotaka kama cheti cha kuzaliwa, affidavit ya mzazi na barua ya utambulisho kutoka serikali ya mtaa, nimefanya process zote vizuri tuu ile nimeenda kwa afisa wa mwisho akawa anakagua form zangu akaona kwenye cheti changu cha kuzaliwa sehemu ya mama mzazi jina la baba yake halipo lipo jina la mama tuu tatizo likaanzia hapo nikaambiwa cheti ni fake inabidi niende RITA niombe cheti kingine cha kuzaliwa, nikasema fine nimefika RITA nikaambiwa inabidi niapply online na niambatanishe leaving certificate ya form 4 au 6 na barua ya utambulisho kutoka serikali ya mtaa. Tatizo ni kwamba leaving certificate zinaonesha nimezaliwa 1994 na nida yangu inaonesha nimezaliwa 1993 na cheti nilichoambatanisha mwanzo cha kuzaliwa immigration kinaonesha nimezaliwa 93, issue ni kwamba hata nikitafuta cheti cha kuzaliwa kingine bado kitatoka cha 94 kwasababu ya zile leaving certificate nikienda immigration wataona miaka inatofautiana na kwenye NIDA so nipo njia panda naombeni ushauri wakuu nifanyeje? mtanisamehe kwa uandishi m'bovu.
Ndiyo mtaelewa maana ya kuweka records vizuri.
 
Nenda NIDA ukabadilishe mwaka wa kuzaliwa ili ufanane na leaving certificate ulio ambatanisha kwenye passport application yako.
Ukifika NIDA kawarushie lawama kwamba wao ndio walikosea kuweka mwaka wako wa kuzaliwa kua 1994 badala ya 1993.
Baada ya hapo watakupa form ya kufanya marekebisho kisha utalipia pesa kidogo haizidi 20k na kisha watakurekebishia mwaka ila namba na mengineyo yatabaku vilevile.

Issue ni kwamba wakati tunafatilia NIDA tuliambatanisha na copy za vyeti vya kuzaliwa sasa nitawalaumu vipi wakati cheti changu kinaonesha nimezaliwa 93.
 
Back
Top Bottom