Melki the Storyteller
JF-Expert Member
- May 3, 2022
- 5,700
- 9,779
Naona nchini Tanzania uhuru umeanza kuzidi, na watu wanaibua vitu vya kijinga kila kukicha!
Assume wazazi wanafanikiwa kupata mtoto, wanakaa, wanajadili jina la mtoto wao, wanaamua kumuita jina ambalo hata kwenye mfumo wetu wa majina wa Tanzania, Africa na dunia kiujumla haupo!
Mzazi anaitwa Mkulungwa Masasa (Baba), Sajlath Madaa (Mama), mnapata mtoto mnamuita Fiston Mayele
N.B: Majina ya wazazi tajwa hapo juu siyo halisi
Halafu kwenye cheti cha kuzaliwa cha mtoto
Baba: Mkulungwa Masasa
Mtoto:Fiston Mayele
Hii yote ni kwa sababu ya ushabiki wa kijinga! Wazazi wanafikiria wakati huu, na hawamfikirii mtoto kabisa!
Hivi ikitokea katika maisha yake cheti chake kikahitajika, hivi atazungumza nini ili aeleweke? Shuleni atumie Fiston Mayele, kwenye application ya loans chuo kikuu jina la baba lisomeke Mkulungwa Masasa, hata kama mimi ndo loan officer namnyima mkopo!
Sijui wazazi wengine wamekula maharage ya wapi! Fiston Mayele Mkulungwa Masasa, haiingii akilini! Sijui kwenye kitambulisho cha taifa, NIDA, huyu mtoto atawaeleza vipi ili wamwelewe!
Wazazi mbadilike,
Ziada: Muache kuwapachika local names watoto wenu, wakikua wanayakataa, wanaleta shida! Eti, Mabolo Mkuyenge, haki ya nani hata kama mimi ndo mtoto ntalikataa!
Nawasilisha: