Gluk
JF-Expert Member
- Mar 23, 2017
- 1,859
- 3,024
Kama kuna watu wanapata shida sana hapa mjini basi ni sisi wapangaji hususani sisi wa kipato cha chini.
Hii nyumba niliyopanga ina visanga sijawahi kuona. Kisanga cha kwanza mvua ikinyesha kidogo tu godoro lazima lielee si bondeni ila maji yanaingia mithili ya mtu aliyeko nje.
Kwahiyo kipindi hiki cha masika nimekuwa kama mtu mwenye watoto wanaokojoa kitandani kila jua linapowaka lazima nianike godoro nje.
Nimekaa miezi miwili ila naona kama nimekaa mwaka mzima kwa tabu ninayoipata. Hivi vyumba vya elfu 30,000 ni pasua kichwa sana hapa mjini.
Upande wa pili wa kupata totozi kipindi hiki nimekuwa mpole maana naogopa kupata aibu ya karne pale nitakapomleta mtoto gheto na mvua ikanyesha.
Wito kwa wenye nyumba mnatutesa sana wapangaji kutupangishia vyumba vinavyoingiza maji pindi mvua inyeshapo ili hali mnajua
Acha niishie hapa maana nina hasira sana na huyu landlord.