Pdidy
Platinum Member
- Nov 22, 2007
- 61,787
- 37,992
SHIDA KUU YA WANAWAKE SIYO KUSIKIA — NI KUTOKUJUA KUTAMBUA SAUTI SAHIHI.
Wanawake wengi wana sikio la kipekee la kiroho — wanaweza kusikia. Lakini changamoto yao kubwa ni kutotofautisha nani anayeongea.
Sauti ya mwanaume ikija kwa upole, kwa maneno matamu na ahadi nyingi, anasikia — lakini hajui kama ni sauti ya shetani inayotumia mwanaume.
Anaweza kusikia “nakupenda” lakini hakujua kama hiyo sauti ilifungwa sumu ndani yake.
Ndiyo maana Eva alianguka Edeni — alimsikia nyoka, lakini hakutambua nani anaongea kupitia nyoka.
Wanawake wengi leo wanapoteza kusudi kwa sababu walivutwa na sauti zenye ahadi zisizo na kusudi.
Aliambiwa atapendwa, akabeba mimba. Aliambiwa ataoa, akajitoa. Lakini hakumwambia Roho Mtakatifu:
“Nifundishe kutofautisha sauti. Nisaidie kujua nani anayeongea.”
Wanawake wengi hawana shida ya kusikia, bali shida yao ni haraka ya kuitikia kabla ya kuchunguza.
Haraka ya kupendwa. Haraka ya kuwa na ndoa. Haraka ya kujazwa mapenzi — bila kuuliza, “Je, huyu ni wa kutoka kwa Mungu au ni wa kutoka kwa tamaa?”
Ni rahisi kwa mwanamke kushawishika na maneno kuliko kuona matendo.
Ni rahisi kuamini ahadi kuliko kuchunguza dhamira.
Na hivyo, kabla hujajibu “ndiyo” kwa mwanaume, kabla hujajitoa moyo, kabla hujatoa usichokuwa tayari kurudisha, mwambie Roho Mtakatifu:
“Sauti ni nyingi, maneno ni mengi, lakini niongoze katika sauti Yako. Nisaidie kujua nani ni wa kusudi, na nani ni mhalifu wa moyo wangu.”