...John Shibuda; kama anavyofahamika ni "mjanja" wa kuchezea siasa kwa kuwa ndio "mradi" wake (political enterprising) na ndio kusema, alipopigwa chini na CCM (jimboni) kwake aliamua kuhamia CHADEMA...kwa kuwa aliamini hawezi kushindwa vita vya kisiasa (yeye kama mwanasiasa anajua mbinu za kucheza na siasa na au kupigana vita vya kisiasa)...na mara zote mpiganaji wa kisiasa hutafuta ushindi...Shibuda mwaka 2010 aliitumia mbinu hiyo baada ya kukosa nafasi CCM alidandia basi la uchaguzi la CHADEMA na kushinda kiti cha ubunge....!
Inawezekana alivyoamua kuhamia CHADEMA mwaka 2010 wapangaji mikakati wa "intelijensia" wa CHADEMA hawakumjua "jenerali" huyu au...?! Tuyaache, Shibuda anatumia "mizungu" ya kisiasa na ndio kusema kwamba yeye (kama mwanasiasa) anaitumia siasa kuendesha maisha yake, kwa jinsi hiyo yupo tayari kuchukua njia yoyote alimuradi kufikia malengo yake ya ujasiriamali wa kisiasa.
Inawezekana ametumia "cheo" hicho kwa kuwa ni mpiganaji mwenye mbinu za kuongoza mapambano ya kisiasa kama anavyosadifu tangu akiwa CCM na sasa CHADEMA. Ukimjua Shibuda hakusumbui - ni "political opportunist" na hakubali kushindwa kirahisi!