Shibuda: Maaskofu muacheni Rais afanye kazi

Ameyasema hayo huku akisisitiza kua kitendo cha maaskofu kuendelea kumuandama Raisi Jk mara kwa mara si cha kiungwana huku akiwa amefanya mambo mengi huku akiungwa mkono na BAKWATA huku wao wakisema Rais amefanya mambo mengi mazuri kwenye kipindi chake cha uongozi.

Source: Gazeti Jambo Leo

Wamuache afanye kazi gani?
Wanachofanya ni kumhimiza afanye kazi.
 
siku ya ufunguzi wa kampeni za CDM,nilikuwepo jangwani,..alpopewa mda kuongea nilifunika uso kwa aibu,hakuongea point hata moja zaidi ya misemo ya kipumbavu.,nikajua kwa vile CDM kuna watu makini watampa shule,.lakini wapi..mbwa mzee hafundishiki.
 
Ha haa haa! Guys you are very funny! Hivi lengo la mtoa mada ilikuwa tumjadili Mh. huyu (personality yake) au tufanye upembuzi yakinifu kwa maneno aliyoyasema.

Mi binafsi naona maneno aliyoyasema yana Mashiko kwa sababu siku za karibuni kumezuka wimbi la viongozi wa dini (Nikimaanisha wakristo na waislamu) kuidadavua Serikali kila kukicha sasa najiuliza hiviii siku serikali nayo ikiacha kazi zake za msingi (MISSION) na kuanza kuzidadavua dini hizi kwa staili ya mipasho kama wanavyofanya wao patatosha kweli!!
My take : kila mmoja afanye kazi zake za msingi kama ni kuikosoa Serikali vipo vyama vya Upinzani na Wanaharakati wengine sio kazi ya taasisi za kidini.
Wewe umo humohumo pia,je waliyosema maaskofu hayana ukweli? Je unaona uwajibikaji wowote serikalini? Na wewe unafanza nini km siyo kujadili personality badala ya content!
 
DINI zinaingia kupita kiasi kwenye SIASA na kila dini/dhehebu linaingia kwa maslahi yake sio ya Taifa. Shibuda yuko sahihi kwa hili. Tukiliachia hili liendelee hatutakuwa mbali sana na NIGERIA muda si mrefu ujao.
 
Mie mwenyewe nawashangaa sana maaskofu badala ya kukemea ufisadi ndani ya makanisa yao ambapo mafisadi wengi ndimo wanamo tokea na wao kuwakumbatia wanamwandama Rais. Hii yaonyesha maaskofu wana ajenda ya siri kwani kipindi cha BWM hatukuwasikia kabisa. Maaskofu fanyeni kazi yakuwafunza mafisadi ndani ya makanisa yenu waache uovu huo, kwani mafisadi wengi ni wakristo.

Badala ya kuwatenga huwatukuza na kuwawekea viti vya mbele kwenye makanisa yao, huwaalika kwenye harembee zao na wengine hata kufikia hatua ya kuwasafisha hadaharani. Ingalikuwa bora kama wangaliwafukuza au kuwatenga makanisani kwao kwanza ili wapate uhalali wa kuisema serikali vibaya juu ya ufisadi.
 
DINI zinaingia kupita kiasi kwenye SIASA na kila dini/dhehebu linaingia kwa maslahi yake sio ya Taifa. Shibuda yuko sahihi kwa hili. Tukiliachia hili liendelee hatutakuwa mbali sana na NIGERIA muda si mrefu ujao.

Mkuu kuna nini huko Nigeria? Boko haram? Nasikia walilipua makanisa siku ya xmas. Somalia wanajiita alshabab, Sudan janjaweed, Pakistan Taliban, kidunia alqaida. Sisi hapa bongo wataibuka na jina gani, tusubiri tuone
 
Ukweli shibuda ni mlopokaji lakini kwa upande mwingine hawa viongozi wetu wa makanisa hawaeleweki ni wanafki wameakuwa kama popo tena ni vuguvugu
 
Mie mwenyewe nawashangaa sana maaskofu badala ya kukemea ufisadi ndani ya makanisa yao ambapo mafisadi wengi ndimo wanamo tokea na wao kuwakumbatia wanamwandama Rais. Hii yaonyesha maaskofu wana ajenda ya siri kwani kipindi cha BWM hatukuwasikia kabisa. Maaskofu fanyeni kazi yakuwafunza mafisadi ndani ya makanisa yenu waache uovu huo, kwani mafisadi wengi ni wakristo.

unawashangaa vipi Maaskofu wewe? inaelekea you are not well informed; huwa husomi vyombo vya habari ila unasikiliza talalila za mitaani, huna kumbukumbu kabisa, Maaskofu waliisema sana serikali ya BWM ila kwa kuwa ilikuwa ni serikali sikivu alifuata ushauri kwa maslahi ya taifa
wewe na shibuda ni sawa kabisa tutawapaka wanja na ina mkaimbe taarabu na ghani maana shibuda inaelekea ni bingwa wa mipasho na wala sio kiongozi CDM walifanya makosa hawakumtambua kabla kuwa ni KIGEUGEU
Shibuda nae Kigeugeu!!!!!
 
Hivi huyu mzee alisoma mpaka lanne la zamani labda,maana amebaki chadema kama kichekesho tu hata hawana time naye.Hana hadhi ya kuongea na maaskofu wala kuwakaribia. kazi anayoweza ni kuimba mashairi ya kutetea theposho.Tumuache amalizia mudawake huyu ni kichaa. Chadema hawakumjua inabidi time ijayo chadema wawe wana interview watu wa kugombea kwa muda mrefu sio kwa zima moto.Pia nadhani ccm wamekwisha kumuhonga maana ili warudishe lile jimbo ccm.
 
Always be specific. Viongozi wa dini wanaoikosoa serikali wana hoja za msingi zilizosheheni uzalendo au la? Kuwa kiongozi wa dini sio kwamba unapoteza sifa ya kutoa mawazo yako maana hii haki ya asili. Kokote duniani viongozi wa dini wanatoa hoja ziwe za kusifia au kukosoa.Mbona viongozi hao wa dini wanapoisifia serikali hatusikii malalamiko? Kuikosoa imekuwa nongwa? Halafu watu kama wewe na Shibuda muelewe kuwa serikali inatengenezwa na awatu wa kawaida wanaofanya makosa na madhambi na wanatakiwa kukosolewa na kuambiwa point blank. Wakifanya vizuri watasifiwa wakifanya vibaya wabomolewe.

Na lazima tuwe wakweli. Hivi serikali hii inayofanya kazi kwa style ya zima mato itasifiwa kwa lipi? Napata tabu wale wanaoitetea pale inapokosolewa. Uchimi imeshindwa, demokrasia imeminya, kisheria inanyima watu haki yao-malipo ya wazee waliokuwa wa Jumuia ya Afrika Mashariki iliyovunjika mwaka 1977, mgombea binafsi, mshindi wa urais kutopingwa mahakamani, litania ni ndefu, elimu imekuwa ni duni na chanzo cha kuwagawa Watanzania kati ya wale wanaomaliza shule za kata na shule nzuri zenye majina ya Watakatifu
 
huyu ni mnafiki!

shibuda ni mtu mabaye sio mnafiki... he not an Ass kisser kama viongozi wengine... yeye ni mtu wa kutema kavu.. mfano posho aliweka wazi msimamo wake...! wakati wengine wanajifanya wakipinga mlango wa nyuma wanapokea...!

Hebu ninyi viongozi wa dini muacheni mh. Rais Dr. JK afanye kazi.. yake!
 
Huyu jamaa ananikera sana na upopo wake,yaani hana msimamo kabisa anapepea kama bendera.
 
Moja ya sababu ya kukubaliki kwa CHADEMA kwa wananchi ni kule kutetea masilahi ya wanyonge dhidi ya serikali ya CCM, kosa kubwa kwa chama hiki ni kule kutokuwa na mfumo sawa na sahihi wa malipo kwa viongozi wake walioko mikoani na wilayani. Ni kweli kabisa ili chama kikubalike kwa wananchi ni kutetea masilahi ya wanyonge wa kawaida lakini ni lazima tukubali kuwa ustawi wake ni lazima kukwepa kwa namna yoyote kuingia katika migogoro. Ushauri wangu kwa chama hiki ili kukwepa atakaye taka kuingiza chama hiki katika migogoro ni kumuenzi marehemu Chacha Zakayo Wangwe kwa kuwajali viongozi wake walioko mikoani na wilayani ambao huingia katika vikao vya juu vya maamuzi. Ni lazima tuelewe kuwa kuwatengemea Wazee wa Chama kuepusha migogoro ipo siku watagonga ukuta. Watu wa aina ya Shibuda wakitaka kuiuwa CHADEMA ni kuonekana kuwatetea viongozi wa chama hiki waliko mikoani na wilayani hasa ile mikoa ambayo ni kama imesahaulika hasa kwa kutonufaika hata kidogo na kile chama kinachopata kama ruzuku au ufadhiri. Ni lazima tuelewe kuwa kura ya M/kiti wa mkoa wa Kilimanjaro au Mwanza ni sawa na kura ya M/kiti wa mkoa wa Lindi au Pwani katika kufanya maamuzi. Ni lazima kama chama kuhakikisha masilahi ya watu hawa yawe sawa pasipo kujali kuwa mkoa huu uliingiza kura kiasi gani kwenye chama ambazo zimepelekea kupata ruzuku. Nimeshauri hivi kwa sababu kuna malalamiko mengi sana kwa baadhi ya viongozi wa mikoani kuonekana chama makao makuu kutowajali kimasilahi kama mikoa mingine. Ushahidi wa hili jinsi marehemu Wangwe alivyokubalika kwa wajumbe kutoka mikoani. VIONGOZI MTAFAKARI. Naomba kuwasilisha.
 
Ameyasema hayo huku akisisitiza kua kitendo cha maaskofu kuendelea kumuandama Raisi Jk mara kwa mara si cha kiungwana huku akiwa amefanya mambo mengi huku akiungwa mkono na BAKWATA huku wao wakisema Rais amefanya mambo mengi mazuri kwenye kipindi chake cha uongozi.

Source: Gazeti Jambo Leo

Maneno sawia kabisaaa. Kwani inaonekana huko Tanzania Maaskofu ndio watakaoleta mtafaruku nchini mwenu.

Bora Shibuda umeliona hilo na kulikemea tena hadhwarani.

Hongera sana kwa kuona mbaaaali

 
Back
Top Bottom