Shibuda: "Hakuna chama kama CCM" akitoa Semina elekezi MaRC na MaDC Dodoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shibuda: "Hakuna chama kama CCM" akitoa Semina elekezi MaRC na MaDC Dodoma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, May 27, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  May 27, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]


  MBUNGE wa Maswa Mashariki, John Shibuda (Chadema) ameibuka na kusema kuwa kama angekuwa na uwezo, angehakikisha kuwa chama chenye kauli za uchochezi kinashikishwa adabu na kwamba hadi sasa hajaona chama chenye nguvu mithili ya CCM. Amekifananisha chama hicho tawala kuwa na nguvu sawa na mngurumo wa ndege ya kivita (Airforce). Alisema kuwa, mfumo wa sasa wa vyama vingi umezaa hasira kwa sababu CCM inataka kutawala, ilihali wapinzani nao wanaitaka nchi ili waitawale.

  Shibuda aliyasema hayo jana mjini hapa, alipokuwa akitoa mada ya Demokrasia na Siasa wakati wa mafunzo elekezi ya Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya yanayoendelea hapa. Alikuwa akiwasilisha mada hiyo iliyoandaliwa na Mpango wa Kutathimini Utawala Bora Afrika (APRM). Alisema kuwa gazeti moja la kila wiki mapema wiki hii lilikuwa na habari iliyokuwa na maneno `CCM yakaribia kuaga Ikulu’, lakini akasema kamwe hajawahi kuona chama chenye mngurumo wa Airforce kuweza kuizidi CCM na kushika nchi. “Ningekuwa na uwezo mara ninaposikia kuna uchochezi sitamkamata mtu aliyetoa maneno ya uchochezi, bali nitakipiga faini chama chake kwa lengo la kuhakikisha kuwa kinabadili lugha zake, kwani chama chenye uchochezi kikipigwa faini mara nyingi kitakuwa na nguvu tena?” alihoji Shibuda.

  Alisema kuwa, fitna mara nyingi zimekuwa malighafi za kisiasa kutokana na maneno matamu, lakini APRM ni chujio na kuwa mfumo wa vyama vingi huzaa wawindaji. “Kiongozi anayekaa ofisini hawezi kujua kiu ya wananchi wake, ni lazima kujisahihisha na kujitathimini, kwani Serikali na siasa ni kama mapacha, lakini cha muhimu ni kujiuliza vipi tutalinda mitaji yetu? Kwani kuna vishawishi vya kuacha mema na kukumbatia upumbavu, lakini matunda matamu hutambulishwa na mbegu za kuzaa matunda matamu,” alisema.

  Aliongeza kuwa, siasa za sasa zimejaa unafiki mfano wa malezi ya machokoraa (watoto wasio na makazi maalumu) ambayo hayakupata malezi ya baba na mama. “Mfumo wa vyama vingi unazaa hasira kwa sababu tunataka kuwakomoa wapinzani na CCM inasema inataka kuwamaliza wapinzani, lakini ukimaliza mazalia ya mbu malaria haitakuwepo,” alisema.

  Alisema kuwa, Rais Jakaya Kikwete ni mwanasiasa na bila siasa hakuna kilainishi cha kuongoza na kutawala . “Wakoloni walitumia machifu wa Kisukuma kutawala, wanaweza kukushangilia ukajua wanafurahia kumbe wanatafuta mwanya wa kukuadhibu,” alisema Shibuda. Alisema kuwa mwanzoni alikuwa CCM na sasa yuko upinzani, hivyo ana taswira ya nchi inakoelekea. Aliongeza: “Najiuliza, naacha urithi gani kwa wadogo zangu waliochaguliwa kuwa Wakuu wa Wilaya?”.

  Shibuda aliwataka viongozi wa Serikali kuhakikisha wanatunza vizuri historia ya nchi akisisitiza historia inahifadhiwa, lakini kama mtoto ni chokoraa, hatakuwa na uwezo wa kutunza historia. Aliongeza kuwa, siasa ni daraja la maoni kwa ajili ya kuongoza umma na kila chama kimekuwa kikishindana kwa lengo la kuhakikisha kuwa kinashinda uongozi.

  Aidha, Shibuda alitumia fursa hiyo kukishukuru CCM kutokana na uelewa wake, huku akisema hataki chama hicho kife, kama ambavyo pia hataki Chadema ife. Mafunzo hayo elekezi yanayofanyika mjini Dodoma yanahudhuriwa na Wakuu wa Mikoa 24, Makatibu Tawala wa Mikoa 25 na Wakuu wa Wilaya 133.

   
 2. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #2
  May 27, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mimi mrengo wa kati ngoja nipite waje wa mrengo wa kushoto watakavyo mshukia atajuta.Sitaki kuona damu
   
 3. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #3
  May 27, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Shibuda anawafunda wote, si CCM si Upinzani.

  Nna uhakika ukimsoma na au ukimsikiliza kwa makini, utaelewa kuwa huyu mtu ana falsafa ya hali ya juu na si wengi wanaoweza kumuelewa. Ni mtu mahiri, makini, na ni mwansiasa wa ukweli.

  Kila mwanasiasa mwenye fikra njema inapaswa ajifunze kutoka kwa huyu Mzee.
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  May 27, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Jambo moja muhimu la kujiuliza, kwa nini CCM na Serikali yak wamekazana kumwalika Shibuda kwenye makongamano na semina elekezi? Kwa nini hawakumwalika mtu mwingine kutoka Chama Cha upinzini kutoa mada hizo isipokuwa Shibuda? Kuna kila dalili nyuma ya pazia kinachoendelea, na busara ya viongozi wa Chadema kutuliza vichwa na kitakachotokea Shibuda atawakumbuka akina Masumbuko Lamwai, Kaburu, Shitambala na wengineo.

  CCM ni mabingwa wa kumwaga cho chote pale wanapokuhitaji, wakishafanikisha walichokusudia unatelekezwa.
   
 5. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #5
  May 27, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,070
  Likes Received: 6,533
  Trophy Points: 280
  Acha waje wenye taaluma zao.
   
 6. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #6
  May 27, 2012
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Tupe source
   
 7. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #7
  May 27, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  ndo kauli mbiu mnayokuja nayo siku hizi ili muendele kumtumia mamluki wenu cdm.
   
 8. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #8
  May 27, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,996
  Likes Received: 2,651
  Trophy Points: 280
  Huo mpango wao tulisha ushtukia zamani,kwa sasa hauna nguvu tena acha waendelee kubwabwaja tu,na kujipa matumaini wakati wanasubiri kaburi lao 2015.
   
 9. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #9
  May 27, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Unataka kutwambia CCM hawakuilewa "falsafa ya hali ya juu" ya Shibuda ndiyo maana wakamtema 2010?
  No wonder JK na NEC yake sasa wanajifunza kwa Shibuda BRAVO Shibuda!
   
 10. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #10
  May 27, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  kwa nini shibuda anawatukana watoto wa mitaani?kuwaita chokoraa maana yake nini?
   
 11. h

  hans79 JF-Expert Member

  #11
  May 27, 2012
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  Apimwe akili, unasema nyumba hii chafu nawe hutoki ina maana una matatizo. Jana wananchi wamesema aondolewe,mkiti kasema kadogo sana hako hakana ubavu taratibu zinafuatwa ili kumwadabisha. Mchukue anawafaa cha pombe, hakuna aliye juu ya chama kaondoka Kaburu sembuse huyo cha urafi.
   
 12. Boniface Evarist

  Boniface Evarist JF-Expert Member

  #12
  May 27, 2012
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 1,100
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Politics is a dirty game! No formula to guide it whenever you feel to conquer then it applies to the situation.
  Definetely he exaggerated to CCM this will not be perceived clear to CHADEMA
  Think on terming Airforce One to the gambaz... do you think Gwandaz will like this?
  Any way I am trying to stay far from politics kwa kweli!
   
 13. M

  Mtanganyika mweusi Member

  #13
  May 27, 2012
  Joined: Apr 26, 2012
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Keshajua anatemwa anatafta kwa kurudia hana lolote mchumia tumbo
   
 14. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #14
  May 27, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Source habari leo la leo Jumapili.

  Naomba wale wote wanaomsapoti Shibuda na wako CHADEMA watoe na maoni yao kuhusiana na hili la shibuda.
   
 15. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #15
  May 27, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145

  Wapi W, B, M, JS, K, na wale wote wanaomsapoti Shibuda ili watuambie tena kuhusu hili la Shibuda.
   
 16. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #16
  May 27, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Mbowe anena kuhusu Shibuda: "Sikuja hapa kumng'oa mtu…Tumng'oe?" Alihoji Mbowe na kuongeza: "Ngoja nitoe kauli ya chama. Chama chetu hakitayumbishwa na mtu yeyote msaliti. Tutatumia vikao vya chama. Tuzungumze mambo yenye maslahi ya taifa, siyo mtu mmoja mwepesi. Kama mtu hajui moto auchezee."
   
 17. R.B

  R.B JF-Expert Member

  #17
  May 27, 2012
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 6,166
  Likes Received: 1,101
  Trophy Points: 280
  NILIVYOKUWA NAMFIKIRIA MWANZO BAADA YA KUSIKIA VYOMBO VYA HABARI ; TOFAUTI KABISA NI MTU ANAYETAKA TANZANIA KWANZA (TUNAYOITAKA); Km anatoa semina na anitwa NGO kubwa km hii ; anabusara za kutosha ;
   
 18. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #18
  May 27, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hata Slaa alitemwa au umesahau.
   
 19. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #19
  May 27, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kwa msimamo huu ni dalili tosha ya kuonyesha ukomavu katima masuala ya siasa na uongozi. Utumiaji majukwaa katika kutolea maamuzi si busara na ni hatari sana. Hali kadhalika suala la mtu mmoja si la kujenga hoja ya kuumiza vichwa katika zana nzima ya mikutano ya movement for change.

  Suala la Shibuda dogo sana na ipo siku atajutia kuburuzwa na wanaomtumia. Yuko wapi Masumbuko Lamwai? Kaburu? Shitambala? nawengineo? Historia ni mwalimu.
   
 20. theophilius

  theophilius Senior Member

  #20
  May 27, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 151
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  kama toilet paper!
   
Loading...