Shibuda: "Hakuna chama kama CCM" akitoa Semina elekezi MaRC na MaDC Dodoma

John Shibuda + Adam Chagulani ni janga ndani ya cdm,wapigwe chini wakaunde chama chao, full stop!
 
Na mimi naomba CCM isife. Maana CCM ikifa hakutakuwa na upinzani. Japo kiuhalisia ccm wanachungulia kaburi. Mpaka shibuda anatoa semina elekezi kwa serikali ya ccm bado tunasema ccm iko hai?
 
Sina shida na kauli za Shibuda kwa sababu najua he is a loose canon. Tatizo langu ni kwa serikali ya CCM na hata NEC ya CCM kuona kuwa Shibuda anafaa kutoa mafunzo kwa wakuu wa Mikoa na Wilaya!

Nilitegemea kuona watu kama Prof Shivji, Kamishna wa tume mipango -Hazina, mtu toka ESRF au REPOA, CAG wawe wanatoa mafunzo. Wakuu wa mikoa na wilaya wanawakilisha serikali (executive) kwenye maeneo yao.

Serikali inatakiwa itekeleze Vision 2025, sasa Shibuda anajua nini kuhusu vision 2025? Badala ya kutumia huo muda vizuri kujua priorities za nchi ni zipi, dira ni ipi, na wanatakiwa kufanya nini hawa wateule, CCM wanaona wamlete Shibuda kuimba ngonjera. Na hapa ndipo naona CCM wamefikia mwisho. Hivi kwa mtindo huu kweli Tanzania tunaweza kushindana na nchi jirani kama wakufunzi ni Shibuda na wakuu wenyewe wa Wilaya na mikoa ndio hao wachovu?

Tangu lini kocha wa timu ya mpinzani ukamwita kuja kufunza mbinu za ushindi kwa timu yako? Hata haiingii akilini. Vinginevyo umeshamnunua kocha huyo na hatarudia timu yake, vinginevyo hakuna kianchoeleweka hapa.

Hakuna vigezo vya ubora wa Shibuda kwenda kuendesha au kutoa mada semina elekezo ya wakuu wa mikoa, wilaya na makatibu wakuu, kwani kinachoendelea ni kielelezo wazi cha uchovu wa uongozi wa CCM. Tunachotazamia kutoka kwa wakuu wa mikoa, wilaya na makatibu wakuu ni hii upopo wa Shibuda Kikwete kaamua kueneza sumu hiyo kwa wateule wake.
 
Shibuda anatoa semina 'elekezi' kwa waliomfukuza! Umeshawahi kuona kondoo aliefukuzwa akarudi kuelekeza kondoo wa zizini njia sahihi ya kupita? Na hichi ndio kisa chenu, clowns circus!
Nyinyi hamjui watu wanaendashaje nchi siku hizi na wanafanyaje maamuzi, siku hizi watu hawakisii, wanafanya kweli, hata maamuzi yanapotoka huna cha kusema wala kulalamika. Nyie bakini viwanja vya Jangwani mkawapoteze zaidi kondoo waliopotea. Ushaona kondoo aliepotea akamchunga kondoo aliepotea? hicho ndio kisa chenu.
 
Shibuda?
Hahahahaaa!!!

Yani ccm badala ya kuongea issues wanaongea Shibuda,

Kwao wao, shibuda ni jambo la kuongelea.

Tuwaache wapate raha kwa kuongelea hili!
Sisi tupo Lindi na Mtwara tunachapa kazi!!

Wakishamaliza kuongea kuhusu shibuda watagundua kumekucha na kimeshanuka!!
 
MBUNGE wa Maswa Mashariki, John Shibuda (Chadema) ameibuka na kusema kuwa kama angekuwa na uwezo, angehakikisha kuwa chama chenye kauli za uchochezi kinashikishwa adabu na kwamba hadi sasa hajaona chama chenye nguvu mithili ya CCM.

Amekifananisha chama hicho tawala kuwa na nguvu sawa na mngurumo wa ndege ya kivita (Airforce). Alisema kuwa, mfumo wa sasa wa vyama vingi umezaa hasira kwa sababu CCM inataka kutawala, ilihali wapinzani nao wanaitaka nchi ili waitawale.

Shibuda aliyasema hayo jana mjini hapa, alipokuwa akitoa mada ya Demokrasia na Siasa wakati wa mafunzo elekezi ya Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya yanayoendelea hapa. Alikuwa akiwasilisha mada hiyo iliyoandaliwa na Mpango wa Kutathimini Utawala Bora Afrika (APRM).

Alisema kuwa gazeti moja la kila wiki mapema wiki hii lilikuwa na habari iliyokuwa na maneno `CCM yakaribia kuaga Ikulu’, lakini akasema kamwe hajawahi kuona chama chenye mngurumo wa Airforce kuweza kuizidi CCM na kushika nchi.

“Ningekuwa na uwezo mara ninaposikia kuna uchochezi sitamkamata mtu aliyetoa maneno ya uchochezi, bali nitakipiga faini chama chake kwa lengo la kuhakikisha kuwa kinabadili lugha zake, kwani chama chenye uchochezi kikipigwa faini mara nyingi kitakuwa na nguvu tena?” alihoji Shibuda.

Alisema kuwa, fitna mara nyingi zimekuwa malighafi za kisiasa kutokana na maneno matamu, lakini APRM ni chujio na kuwa mfumo wa vyama vingi huzaa wawindaji.

“Kiongozi anayekaa ofisini hawezi kujua kiu ya wananchi wake, ni lazima kujisahihisha na kujitathimini, kwani Serikali na siasa ni kama mapacha, lakini cha muhimu ni kujiuliza vipi tutalinda mitaji yetu? Kwani kuna vishawishi vya kuacha mema na kukumbatia upumbavu, lakini matunda matamu hutambulishwa na mbegu za kuzaa matunda matamu,” alisema.

Aliongeza kuwa, siasa za sasa zimejaa unafiki mfano wa malezi ya machokoraa (watoto wasio na makazi maalumu) ambayo hayakupata malezi ya baba na mama.

“Mfumo wa vyama vingi unazaa hasira kwa sababu tunataka kuwakomoa wapinzani na CCM inasema inataka kuwamaliza wapinzani, lakini ukimaliza mazalia ya mbu malaria haitakuwepo,” alisema.

Alisema kuwa, Rais Jakaya Kikwete ni mwanasiasa na bila siasa hakuna kilainishi cha kuongoza na kutawala .

“Wakoloni walitumia machifu wa Kisukuma kutawala, wanaweza kukushangilia ukajua wanafurahia kumbe wanatafuta mwanya wa kukuadhibu,” alisema Shibuda. Alisema kuwa mwanzoni alikuwa CCM na sasa yuko upinzani, hivyo ana taswira ya nchi inakoelekea.

Aliongeza: “Najiuliza, naacha urithi gani kwa wadogo zangu waliochaguliwa kuwa Wakuu wa Wilaya?”.

Shibuda aliwataka viongozi wa Serikali kuhakikisha wanatunza vizuri historia ya nchi akisisitiza historia inahifadhiwa, lakini kama mtoto ni chokoraa, hatakuwa na uwezo wa kutunza historia.

Aliongeza kuwa, siasa ni daraja la maoni kwa ajili ya kuongoza umma na kila chama kimekuwa kikishindana kwa lengo la kuhakikisha kuwa kinashinda uongozi.

Aidha, Shibuda alitumia fursa hiyo kukishukuru CCM kutokana na uelewa wake, huku akisema hataki chama hicho kife, kama ambavyo pia hataki Chadema ife.

Mafunzo hayo elekezi yanayofanyika mjini Dodoma yanahudhuriwa na Wakuu wa Mikoa 24, Makatibu Tawala wa Mikoa 25 na Wakuu wa Wilaya 133.

Source: Habari Leo
 
gamba at work

[h=2]Shibuda afananisha upinzani na chokoraa[/h]

Na Sharon Sauwa

27th May 2012

email.png

B-pepe

printer.png

Chapa

comment_bubble.png

Maoni

Wakati Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kikiendelea kutafakari kauli ya Mbunge wa Maswa Magharibi (CCM), John Shibuda, kumtaka Rais Jakaya Kikwete awe mpiga kampeni wake, jana alizua jambo tena baada ya kuvifananisha vyama vya upinzani nchini na machokoraa.

Shibuda aliyasema hayo wakati alipokuwa akitoa mada katika mafunzo elekezi ya wakuu wa mikoa, makatibu tawala na wakuu wa wilaya nchini yanayoendelea mjini Dodoma.
Shibuda ambaye ni mjumbe wa Mpango wa Kujitathimini Utawala Bora kwa Bara la Afrika (APRM) alikuwa akitoa mada kuhusu ‘chimbuko, maudhui na mfumo wa uendeshaji’ katika mkutano huo.
Kwa mara ya kwanza jana waandishi wa habari waliruhusiwa kusikiliza mada katika mafunzo hayo ambayo Mwenyekiti wake, alikuwa ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
“Wanakuwa kama machokoraa, wanakuwa na mfumo wa machokoraa ambao hawakupata ulezi wa baba na mama, nayasema haya kwa sababu nilikuwa CCM leo hii niko upinzani…nchi yetu inakwenda wapi?” Alihoji.
Alisema ujana unaruhusiwa kufanya makosa lakini ukiwa mkubwa ukafanya makosa unaitwa mtu mzima ovyo.
Alisema CCM inasema inataka kuwaliza wapinzani lakini kinachotakiwa kumalizwa ni matatizo yanayowakabili wananchi, “no (hapana) maliza kwanza mazalia ya mbu.” Akiongea kwa kutumia nahau nyingi kama kawaida yake, Shibuda alisema kamwe haiwezekani kumtenganisha Rais Kikwete na siasa kwa sababu Serikali na siasa ni mapacha.
Alisema hakuna king’amuzi cha kuongoza na kutawala na kwamba wakoloni walikuwa wanawatumia machifu wa kisukuma kwenda kuwasiliana na wananchi kwa sababu kila mahali pana mazingira yake.
Aliwataka viongozi wa Serikali kupambana na wale wote wana momonyoa historia ya nchi na kuhakikisha kuwa historia inahifadhiwa.
“Kila mtu anapaswa kuilinda historia yake…lakini kama mtoto ni chokoraa atatunza historia ya nani ?” alihoji huku akirudia rudia mara kadhaa sentensi hiyo.
Alisema yeye angekuwa ni sehemu ya Serikali, akisikia kuna siasa za uchochezi mahali, hatamkamata mwanasiasa bali atakipiga faini chama chake ili kuweka mfumo mzuri.
Alisema wakati mwingine wanasiasa wanaweza kuwa wanasema hayo ni maneno ya mtu fulani kumbe ni wao ndio waliyoyasema. Alihoji kama chama kitakosa mtaji wa kupata fedha, kitashindwaje kufanya ufisadi wa shughuli za chama.

Alisema wao (wakuu wa wilaya na mikoa ) ni waajiriwa wa CCM ambao wanatakiwa kufikiria ni jinsi gani watapata hisia na matakwa ya watu na kufikiria ni wapi wanapokosea kabla ya kujisahihisha ili kupata imani ya umma.
Alisema mfumuko wa bei huzaa mfumuko wa propaganda na kuwaomba wasivunje ndoa ya chama hicho ambacho Mungu alikijalia kuwa na historia kwa maslahi ya umma.
Hata hivyo, Shibuda alisema kamwe hataki CCM ife wala Chadema kwa sababu vyama hivyo ni kama timu za mpira za Yanga na Simba.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

anagalieni hapo palipoandikwa na wimwekundu!
 
Anajipendekeza!!!!!!!!!!!!!!1 Hana vision wala hana confidence ni mropokaji huyo!!!!!!!
 
Jamani wa Maswa mashariki, nafikiri ni wakati muafaka kuandaa kijana makini kuchukua jimbo lenu. Huyu ki**a**zi alibebwa na CHADEMA sasa ananyea kambi. Ameshasahau kama nchi ndo tumeanza kuiteka sijui ataficha wapi aibu yake.
 
Ifike wakati watu kama hawa tuwapige mawe kwani ni wanafki. Nakumbuka wakati ule anaomba kura alikuwa anasema 'HALELUYAA, YESU ATUONGOZE' nilikuwa naogopa kuona kama ataleta imani ya kidini vile. Leo huyuhuyu anasema vyama vina ubaguzi. SHIBUDA KAMA HUTAKI TOKA CDM RUDI CCM ACHA UNAFKI TUMEKUCHOKA. Sema namuheshimu Mwanao ni mskaji wangu ila ningeku>>>>.
 
Pia shibuda Elewa watoto wa mitaani hawakuomba kuwa hivyo. leo kwake kesho kwako.
 
Wadau sina imani na John magale shibuda kama inaitakia mema chadema.Niunge mkono hapa
 
Kikwete-right-greets-Maswa-West-MP-John-Shibuda.jpg

MBUNGE wa Maswa Mashariki, John Shibuda (Chadema) ameibuka na kusema kuwa kama angekuwa na uwezo, angehakikisha kuwa chama chenye kauli za uchochezi kinashikishwa adabu na kwamba hadi sasa hajaona chama chenye nguvu mithili ya CCM. Amekifananisha chama hicho tawala kuwa na nguvu sawa na mngurumo wa ndege ya kivita (Airforce). Alisema kuwa, mfumo wa sasa wa vyama vingi umezaa hasira kwa sababu CCM inataka kutawala, ilihali wapinzani nao wanaitaka nchi ili waitawale.

Shibuda aliyasema hayo jana mjini hapa, alipokuwa akitoa mada ya Demokrasia na Siasa wakati wa mafunzo elekezi ya Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya yanayoendelea hapa. Alikuwa akiwasilisha mada hiyo iliyoandaliwa na Mpango wa Kutathimini Utawala Bora Afrika (APRM). Alisema kuwa gazeti moja la kila wiki mapema wiki hii lilikuwa na habari iliyokuwa na maneno `CCM yakaribia kuaga Ikulu’, lakini akasema kamwe hajawahi kuona chama chenye mngurumo wa Airforce kuweza kuizidi CCM na kushika nchi. “Ningekuwa na uwezo mara ninaposikia kuna uchochezi sitamkamata mtu aliyetoa maneno ya uchochezi, bali nitakipiga faini chama chake kwa lengo la kuhakikisha kuwa kinabadili lugha zake, kwani chama chenye uchochezi kikipigwa faini mara nyingi kitakuwa na nguvu tena?” alihoji Shibuda.

Alisema kuwa, fitna mara nyingi zimekuwa malighafi za kisiasa kutokana na maneno matamu, lakini APRM ni chujio na kuwa mfumo wa vyama vingi huzaa wawindaji. “Kiongozi anayekaa ofisini hawezi kujua kiu ya wananchi wake, ni lazima kujisahihisha na kujitathimini, kwani Serikali na siasa ni kama mapacha, lakini cha muhimu ni kujiuliza vipi tutalinda mitaji yetu? Kwani kuna vishawishi vya kuacha mema na kukumbatia upumbavu, lakini matunda matamu hutambulishwa na mbegu za kuzaa matunda matamu,” alisema.

Aliongeza kuwa, siasa za sasa zimejaa unafiki mfano wa malezi ya machokoraa (watoto wasio na makazi maalumu) ambayo hayakupata malezi ya baba na mama. “Mfumo wa vyama vingi unazaa hasira kwa sababu tunataka kuwakomoa wapinzani na CCM inasema inataka kuwamaliza wapinzani, lakini ukimaliza mazalia ya mbu malaria haitakuwepo,” alisema.

Alisema kuwa, Rais Jakaya Kikwete ni mwanasiasa na bila siasa hakuna kilainishi cha kuongoza na kutawala . “Wakoloni walitumia machifu wa Kisukuma kutawala, wanaweza kukushangilia ukajua wanafurahia kumbe wanatafuta mwanya wa kukuadhibu,” alisema Shibuda. Alisema kuwa mwanzoni alikuwa CCM na sasa yuko upinzani, hivyo ana taswira ya nchi inakoelekea. Aliongeza: “Najiuliza, naacha urithi gani kwa wadogo zangu waliochaguliwa kuwa Wakuu wa Wilaya?”.

Shibuda aliwataka viongozi wa Serikali kuhakikisha wanatunza vizuri historia ya nchi akisisitiza historia inahifadhiwa, lakini kama mtoto ni chokoraa, hatakuwa na uwezo wa kutunza historia. Aliongeza kuwa, siasa ni daraja la maoni kwa ajili ya kuongoza umma na kila chama kimekuwa kikishindana kwa lengo la kuhakikisha kuwa kinashinda uongozi.

Aidha, Shibuda alitumia fursa hiyo kukishukuru CCM kutokana na uelewa wake, huku akisema hataki chama hicho kife, kama ambavyo pia hataki Chadema ife. Mafunzo hayo elekezi yanayofanyika mjini Dodoma yanahudhuriwa na Wakuu wa Mikoa 24, Makatibu Tawala wa Mikoa 25 na Wakuu wa Wilaya 133.

ukitaza picha hii vizuri utaona mwenye hakili pale ni msekwa tu analitazama li shibuda kua linahakili sawa sawa lakin walio baki...mungu anajua
 
who is shibuda by the way?si yule aliyeitukana ccm alipopokelewas cdm?tunamrudisha ccm na tutaplay video clips za matusi yake kwa ccm kwenye you tube na kila m4c inapopita.
 
Hiyo ndiyo 'true colour' ya Mamluki Shibuda. CDM watch out!
 
huyu jamaa anapenda nyama kuliko maelezo,kama una kasherehe kako kadogo weka konyagi na nyama mwalike huyu jamaa.
ila akilewa anakojoa popote.
 
Back
Top Bottom