Shibuda: "Hakuna chama kama CCM" akitoa Semina elekezi MaRC na MaDC Dodoma

Kwa ufupi Shibuda (Kibudu) ameshindwa kazi hata kama alitumwa kuifanya....Waliomtuma walishindwa kumpa guidelines za maana. In short ameshindwa na wale waliomtuma wameangukia pua!

Hata hivyo, kauli za Kibudu (Shibuda) ni sawa na pole zinazotolewa kwenye msiba.. na kwa sasa ndio kitu ambacho CCM wanakihitaji sana. Zinawapa faraja ya kutosha kusubiria hukuma yao mwaka 2015!!

Asiyeamini asubiri kidogo.....ila maandiko ukutani yanasomeka vizuri sana labda kwa kipofu tu!

Babu DC!!
 
Asemeje na cdm washa mpuuza?
atalalama sana kutafuta pa kudondokea!lol
 
MBUNGE wa Maswa Mashariki, John Shibuda (Chadema) ameibuka na kusema kuwa kama angekuwa na uwezo, angehakikisha kuwa chama chenye kauli za uchochezi kinashikishwa adabu na kwamba hadi sasa hajaona chama chenye nguvu mithili ya CCM.

Amekifananisha chama hicho tawala kuwa na nguvu sawa na mngurumo wa ndege ya kivita (Airforce). Alisema kuwa, mfumo wa sasa wa vyama vingi umezaa hasira kwa sababu CCM inataka kutawala, ilihali wapinzani nao wanaitaka nchi ili waitawale.

Shibuda aliyasema hayo jana mjini hapa, alipokuwa akitoa mada ya Demokrasia na Siasa wakati wa mafunzo elekezi ya Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya yanayoendelea hapa. Alikuwa akiwasilisha mada hiyo iliyoandaliwa na Mpango wa Kutathimini Utawala Bora Afrika (APRM).

Alisema kuwa gazeti moja la kila wiki mapema wiki hii lilikuwa na habari iliyokuwa na maneno `CCM yakaribia kuaga Ikulu’, lakini akasema kamwe hajawahi kuona chama chenye mngurumo wa Airforce kuweza kuizidi CCM na kushika nchi.

“Ningekuwa na uwezo mara ninaposikia kuna uchochezi sitamkamata mtu aliyetoa maneno ya uchochezi, bali nitakipiga faini chama chake kwa lengo la kuhakikisha kuwa kinabadili lugha zake, kwani chama chenye uchochezi kikipigwa faini mara nyingi kitakuwa na nguvu tena?” alihoji Shibuda.

Alisema kuwa, fitna mara nyingi zimekuwa malighafi za kisiasa kutokana na maneno matamu, lakini APRM ni chujio na kuwa mfumo wa vyama vingi huzaa wawindaji.

“Kiongozi anayekaa ofisini hawezi kujua kiu ya wananchi wake, ni lazima kujisahihisha na kujitathimini, kwani Serikali na siasa ni kama mapacha, lakini cha muhimu ni kujiuliza vipi tutalinda mitaji yetu? Kwani kuna vishawishi vya kuacha mema na kukumbatia upumbavu, lakini matunda matamu hutambulishwa na mbegu za kuzaa matunda matamu,” alisema.

Aliongeza kuwa, siasa za sasa zimejaa unafiki mfano wa malezi ya machokoraa (watoto wasio na makazi maalumu) ambayo hayakupata malezi ya baba na mama.

“Mfumo wa vyama vingi unazaa hasira kwa sababu tunataka kuwakomoa wapinzani na CCM inasema inataka kuwamaliza wapinzani, lakini ukimaliza mazalia ya mbu malaria haitakuwepo,” alisema.

Alisema kuwa, Rais Jakaya Kikwete ni mwanasiasa na bila siasa hakuna kilainishi cha kuongoza na kutawala .

“Wakoloni walitumia machifu wa Kisukuma kutawala, wanaweza kukushangilia ukajua wanafurahia kumbe wanatafuta mwanya wa kukuadhibu,” alisema Shibuda. Alisema kuwa mwanzoni alikuwa CCM na sasa yuko upinzani, hivyo ana taswira ya nchi inakoelekea.

Aliongeza: “Najiuliza, naacha urithi gani kwa wadogo zangu waliochaguliwa kuwa Wakuu wa Wilaya?”.

Shibuda aliwataka viongozi wa Serikali kuhakikisha wanatunza vizuri historia ya nchi akisisitiza historia inahifadhiwa, lakini kama mtoto ni chokoraa, hatakuwa na uwezo wa kutunza historia.

Aliongeza kuwa, siasa ni daraja la maoni kwa ajili ya kuongoza umma na kila chama kimekuwa kikishindana kwa lengo la kuhakikisha kuwa kinashinda uongozi.

Aidha, Shibuda alitumia fursa hiyo kukishukuru CCM kutokana na uelewa wake, huku akisema hataki chama hicho kife, kama ambavyo pia hataki Chadema ife.

Mafunzo hayo elekezi yanayofanyika mjini Dodoma yanahudhuriwa na Wakuu wa Mikoa 24, Makatibu Tawala wa Mikoa 25 na Wakuu wa Wilaya 133.

Source: Habari Leo
Poor Shibuda; anatafuta huruma ya sisiemu
 
TIMUA VICHAA CDM.

makosa yalifanyika kumkubali ktk chama makini. tuwe makini kupokea magamba kama haya.
hili limeeleweka nadhani tuache tena kutupa threads za SHIDA KUBWA hapa jamvini.
mhesh. Mbowe piga sindano hili virus.
 
Attention Defficiency Disorder (ADD)
 
Debe tupu haliachi kutika! Unaamini kitu hiki halafu unahubiri tofauti. Lazima uwe chizi fulani
 
Kwa ufupi Shibuda (Kibudu) ameshindwa kazi hata kama alitumwa kuifanya....Waliomtuma walishindwa kumpa guidelines za maana. In short ameshindwa na wale waliomtuma wameangukia pua!

Hata hivyo, kauli za Kibudu (Shibuda) ni sawa na pole zinazotolewa kwenye msiba.. na kwa sasa ndio kitu ambacho CCM wanakihitaji sana. Zinawapa faraja ya kutosha kusubiria hukuma yao mwaka 2015!!

Asiyeamini asubiri kidogo.....ila maandiko ukutani yanasomeka vizuri sana labda kwa kipofu tu!

Babu DC!!

Kweli!
 
Yani mpaka MSEKWA anamshangaa uku viongozi wenzake wa CCM wakikenua bila ya kujua ni huyu SHIBUDA aliekua anamwaga matusi ya kumtukukana KIKWETE kwenye kampeni za urais zilizoisha....Huyu kalibia atavaa chupi kichwani kwani sio mzima na hajui hao CDM ndo wamempa ulaji kwa sasa...mtu mzima anakua ndumilakuwili yani si CCM wala CDM wanaomuelewa labda mke wake tu ndo anaemuelewa nadhani ata watoto wake hawamuelewi huyu mtu
 
Lakini kwanini hakusema hayo 2010 walipoliondoa Jina Lake kugombea Ubunge? au alijua sasa Ulaji basi ngoja nirukie CHADEMA kwanza nipate Ulaji halafu nitafanya ukiritimba wangu wowote ule.

Anyways Politicians are like diapers. They both need changing regularly and for the same reason we will need to change this one in 2015...
 
Yani mpaka MSEKWA anamshangaa uku viongozi wenzake wa CCM wakikenua bila ya kujua ni huyu SHIBUDA aliekua anamwaga matusi ya kumtukukana KIKWETE kwenye kampeni za urais zilizoisha....Huyu kalibia atavaa chupi kichwani kwani sio mzima na hajui hao CDM ndo wamempa ulaji kwa sasa...mtu mzima anakua ndumilakuwili yani si CCM wala CDM wanaomuelewa labda mke wake tu ndo anaemuelewa nadhani ata watoto wake hawamuelewi huyu mtu

Soon jimbo lake analoliwakilisha litakuwa wazi, hapo ndipo atakapotambua nguvu ya umma itakavyomsimamisha asiye na jina kama Arumeru Mashariki amtoe povu jingi na kisha Shibuda akishaambulia patupu atakumbuka General Tire alikokuwa anafanya kazi awali kama nafasi bado ipo.
 
Yani mpaka MSEKWA anamshangaa uku viongozi wenzake wa CCM wakikenua bila ya kujua ni huyu SHIBUDA aliekua anamwaga matusi ya kumtukukana KIKWETE kwenye kampeni za urais zilizoisha....Huyu kalibia atavaa chupi kichwani kwani sio mzima na hajui hao CDM ndo wamempa ulaji kwa sasa...mtu mzima anakua ndumilakuwili yani si CCM wala CDM wanaomuelewa labda mke wake tu ndo anaemuelewa nadhani ata watoto wake hawamuelewi huyu mtu

Inabidi watu waujue ukweli kwamba Kibudu (Shibuda) siyo mzima...

Ni kichaa pekee anayeweza kulikata tawi la mti ambalo kalikalia....Na watu wote wanaoweza kumshangilia kichaa wa namna hiyo lazima ama wana matatizo kama ya huyo kichaa au hata wamemzidi!!
 
Huyu mkweree nae wa kupima akili kwani ni huyu huyu Shibuda aliyekuwa anamtukana na eti leo anamkubatia; waingerza wanamsemo kuwa ukiona adui yako anakusifia ujue wewe ni mjinga!! Leo Shibuda anamsifu Mkweree na ccm!!!
 
kwa nini shibuda anawatukana watoto wa mitaani?kuwaita chokoraa maana yake nini?
BONGOLALA maana ya Chokoraa ni wanasiasa Uchwara sawa na wale watoto wa mitaani ambao wakiamka hawajui waanzie wapi (serikali ya majimbo au kupata nchi ya Meru au Katiba au Uraia wa nchi 2 ) huyu Shibuda ni mara nyingi ana msimamo kumbuka wenzake walitoka Bungeni na sasa hawatamkubali
 
Back
Top Bottom