Shibuda asisitiza yeye ni Rais 2015

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
931
Mhe. John Maghale Shibuda Mbunge wa Maswa kwa Tiketi ya chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amesikika mara kadhaa akijinadi yeye ni Rais ajae wa Tanzania kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema.

Awali ilionekana kama anatania lakini leo tarehe 5.06.2012 akiwa ana changia katika kikao cha tisa cha Wadau wa Pamba kilichofanyika Chuo cha Benki Kuu Mjini Mwanza amesikika tena kwa msisitizo zaidi ya mara moja akiwataka wabunge, wakuu wa Mikoa na wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya wawe makini sana katika kusimamia zao la pamba nchini kwani kushindwa kwao kutakuwa ni tiketi ya kuanguka kwa Serikali ya CCM na kumpa fursa yeye kushinda wa Urais mwaka 2015 kwa tiketi ya chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Kikao hicho kilichohudhuriwa na wadau mbalimbali wa tasnia ya pamba nchini ikiwemo Wakuu wa Mikoa,Wakuu Wilaya, Watendaji wa Halmashauri za Wilaya na Wabunge wanaotoka mikoa inayolima pamba akiwemo Mhe. John Cheyo, Dr. Dalali Kafumu, Vincent Nyerere,Dk Charles Tizeba, Lembeli, Kingwangwala na wabunge wengine watokao maeneo ya kanda ya ziwa kilikuwa na mvutano mkali sana miongoni mwa wabunge hao hasa baada ya Mbunge wa Mwibara Kangi Lugola (CCM) kutoa kauli za kuwatuhumu wabunge wenzake kuwa na maslahi kwenye sekta ya pamba ambayo yanania ya kuwanyonya wakulima akiwamo Hamis Kingwangwala ambae ana kampuni ya ununuzi pamba lakini kwa wakati huo huo anadai kuwa anawatetea wakulima.

Kauli ya Lugola ilimgusa pia Bw. Zizi ambae ni Mwenyekiti wa Chama cha wakulima wa Pamba (TACOGA) ambae nae anadaiwa kujihusisha na ununuzi wa pamba wakati huo huo akidai kuwa yeye ni mkulima na ana simama maslahi ya wakulima..


Katika hali isiyo ya kawaida, Mhe. Shibuda ambae aliwahi kuungana na baadhi ya wabunge wenzake toka maeneo yanayolima pamba kuitaka Serikali kumchukulia hatua Mkurungenzi wa Bodi ya Pamba Bw. Maiko Mtunga kuhusika na matumizi mabaya ya bilioni 2 zilizotolewa ili kuwafidia wakulima kutokana na mdororo wa uchumi (stimulus package) kufuatia ripoti Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma chini ya uongozi wa Mhe. Cheyo ambayo ilipendekeza kuvunjwa kwa Bodi ya Wakurugenzi ya Pamba na kuwachukulia hatua watendaji wake, leo ameonyesha kumhurumia kwa kiasi kikubwa Mkurugenzi wa Bodi hiyo kwa kile alichodai hajatendewa haki kwa kusimamishwa na Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika.

Alieleza kuwa labda kauli yake Mkurugenzi huyo za kuwadhalau wadau ndio yamemponza na sio suala la upotevu wa kiasi hicho cha fedha ambacho kama ndivyo, basi ilipaswa hata mwenyekiti wa Bodi hiyo Mhe. Dr. Festus Limbu nae asimamishwe.

Shibuda alisisitiza kuwa Mkurugenzi huyo ameonewa na kwamba Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) anapaswa tena kufanya ukaguzi makini (forensic audit) kwenye Bodi ya Pamba kabla ya Serikali kuchukua uamuzi wa kumsimamisha Bw. Mtunga au mtu yeyotekutokana na taarifa ambazo huenda hazina ukweli kuhusu suala linalohusishwa na Mkurugenzi Mkuu huyo wa Bodi..

Mkutano huo wa Mwaka wa Wadau wa Sekta ya Pamba ulihudhuriwa pia na Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mhandisi Christopher Kajolo Chiza, Naibu wa Waziri, Adam Kigoma Malima, Naibu Waziri wa TAMISEMI Jumanne Kassim Majaliwa, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga (Mtumishi wa Mungu) ambae akimwakilisha.

Shibuda aliwataka Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika kuhakikisha kuwa wanawatendea haki wakulima wa pamba nchini kwa kuhakikisha fedha zinazotendwa kwa ajili ya maendeleo ya sekta zinatolewa kama ilivyokubalika vinginevyo yeye anaona njia ya kuupata urais 2015 ni nyeupe kutokana na watendaji wa CCM kutokuwa makini kwa wakulima.
 
Zomba,
Unaona sasa? Kumbe si Zitto peke yake ndani ya Chadema anayetaka urais. Sasa nawashauri hawa wawili wachuane
na wote wabwagwe chini ili Chadema ichague mtu asiyejitangazatangaza kuwania urais kwenye vyombo vya habari.
 
Asubiri aone kama hizo ndoto zake zitatimia...... huyu yuko njozini akiamka atagundua kuwa alikua anaota ndoto ambazo haziwezi kutimia katika maisha yake.
 
Sijui kwanini kamati kuu ya chadema wanamwangalia tu,huyu jamaa mi nadhani anatumiwa na ccm ili ajitangaze na watu wamwekee imani na ikifika 2014 aihame chadema ili ivurugike,wasimpomfukuza sasa watakuja kujutia baadaye,a guy is getting popularity wao wanamwangalia tu
 
Mwanaume hajisifii bali anasifiwa, shibuda na zito nani aliyewaambia kuwa wao ni wazuri hadi wafae kuwa rais?kila mtu kuna kiatu kinachomfaa, hivyo wasubiri hadi muda muafaka
 
Mr Mh. Shibuda ana kauli tata na zenye utashi mbaya kwa jamii. Ebu ona "Awali ilionekana kama anatania lakini leo tarehe 5.06.2012 akiwa ana changia katika kikao cha tisa cha Wadau wa Pamba kilichofanyika Chuo cha Benki Kuu Mjini Mwanza amesikika tena kwa msisitizo zaidi ya mara moja akiwataka wabunge, wakuu wa Mikoa na wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya wawe makini sana katika kusimamia zao la pamba nchini kwani kushindwa kwao kutakuwa ni tiketi ya kuanguka kwa Serikali ya CCM na kumpa fursa yeye kushinda wa Urais mwaka 2015 kwa tiketi ya chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). "
Kama ameona furusa ya yeye kuwa Rais kupitia udhaifu wa wakuu wa miko, wilaya na wakurugenzi wa halmashauri then kuna haja gani ya yeye kuwataka wawe makini?
Sijaelewa ni kejeli gani au ya namna gani Shibuda anaitoa kwa CDM!!! Tadhafadhi kama CDM wameamua kumpuuzia basi waendelee tu kumwacha alivyo ila kama wanadhamira ya kumtoa basi waanze leo na iwe sasa hivi.
 
MKUU JG, kimsingi pamoja na haki aliyokuwa nayo kwa mujibu wa katiba ya sasa ya Tanzania, nadhani Shbda hawatendei haki watz au anadhani sisi ni watu wa mizaha mizaha! enough is enough, Mh Shbda akome kuchezea akili zetu na spins za jinsi hii kana kwamba atafanikiwa kutuPUNZA waliowengi. Nani atakubari kuongozwa na mtu aliyejaa mizaha mizaha tuuuu! Nadhani ajifunze kuwa makini kwa mambo makubwa anayo-aspire otherwise watu watamwona HANA maana na si chochote wala lolote.Hebu soma hii quote kwenye uzi huu....wabunge, wakuu wa Mikoa na wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya wawe makini sana katika kusimamia zao la pamba nchini kwani kushindwa kwao kutakuwa ni tiketi ya kuanguka kwa Serikali ya CCM na kumpa fursa yeye kushinda wa Urais mwaka 2015 kwa tiketi ya chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Kwa maana nyingine hataki na wala hastahili kugombea ila anawaonya nyinyienu kuwa wajitahidi kusahihisha makosa otherwise atachukua nchi! Kauri dhaifu kutoka kwa RAHISI mtarajiwa
Huyu jamaa ni mchekeshaji tu kama marehemu Max lol
 
Back
Top Bottom