Shetta: Mimi ni chawa kwa matajiri

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
shetta.jpg

Msanii Shetta
Msanii Shetta ametaka watu wasimuhisi kuwa anajishughulisha na biashara za madawa na badala yake watambue yeye ni mtu anayetumia fursa kila aonapo na ndio maana ana marafiki wengi matajiri ambao wanamsaidia.

Akizungumza kwenye Planet Bongo East Africa radio, Shetta amesema kwamba yeye hajishughulishi na biashara hizo za madawa na wala hana pesa za kutisha kama jinsi watu wanavyomfikiria.

"Mimi sina fedha nyingi kama watu wanavyodhani, sema nina fedha za kutosheleza maisha yangu. Ningekuwa nina pesa nisingwekuwa nawaganda matajiri. Mimi ni chawa kwa matajiri nikiwa nashida namcheki boss Mo, au matajiri ambao nimetengeneza ukaribu nao na mwisho wa siku mambo yangu yanaenda," Shetta.

Katika hatua nyingine Sheta amesema yeye ni mtu ambaye anapenda vitu vizuri na ndiyo sababu watu wengi wamekuwa wakimfikiria vibaya

'Ningekuwa nauza madawa ningekuwa na mimi kwenye ile orodha iliyowahi kupelekwa pale polisi. Mimi ni mtu ambaye napenda vitu vizuri na nikikitaka nitakipata. Kwa hali ya kawaida ukiangalia kazi tunazozifanya huwa zinatulipa, kwa hiyo mimi kuwa na vitu nilivyonavyo vinaendana na kipato ninachokifanya. Yapo matangazo mengi na nimekuwa balozi wa makampuni mbalimbali na yote hayo yananilipa na siyo siri maana watu wanatambua" - aliongeza.

Kwa sasa Shetta anatamba na ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la 'Wale wale' baada ya kukaa muda mrefu kimya.
 
Hivi mtu kama huyu mkewe akimsikia anajisifia hivyo atamfikirije...Hao matajiri nao wakiwa chawa kwa mkewe atasema au..
Mwanaume kamili hawezi zungumza kauli kama hizo.
 
Hiyo kauli ya kusema umetengeneza urafiki na matajiri,kwa mwanaume mtafutaji hawezi kutamka maneno hayo

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata nchi kama hii ya tanzania inatengeneza urafiki na nchi tajiri ili ipate msaada... Kwa hiyo watz wote ni chawa tu...

Kama amepata watu wa kumpa sapoti sidhani kama ni shida hatujajua makubaliano yao.....

Hata mwanaume kama Mengi anakopa benki pia.....

So hatujui wanawekeana namna gani za mutual benefits kwa kila mmoja...

Labda akipigika huwa anawakopa marafiki zake ambao wanaweza kumsaidia hivyo sioni jambo baya jamani.

Kwani kuna mtu ambaye hajawahi kopa kwa ndugu au rafiki yake? Kama yupo nitashangaa sana maana hata duka la mtaani tu unapoishi lazima kuna siku utakopa si kwa sababu tu unakuwa huna hela ila mazingira yanaweza kukufosi ukakopa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika wasanii ambao huwa najiuliza vipato vyao na vile wanavyovimiliki kutokuwa kwenye uwiano ni huyu na mwenzie mwenye "vishimo".
 
Back
Top Bottom