Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Nurdin Bilal Ally Juma, maarufu kama Shetta, amejiunga rasmi na mchakato wa kisiasa kwa kuchukua fomu ya kutia nia ya kugombea nafasi ya Udiwani katika Kata ya Mchikichini, Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Shetta alikabidhiwa fomu hiyo na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa CCM Kata ya Mchikichini, Bi. Hellen Madanganya, katika ofisi za chama hicho leo, hatua inayomuweka rasmi kwenye mbio za kuwania nafasi ya uongozi katika uchaguzi mkuu wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.