Vunjabei anatumia nguvu kubwa sana kushinikiza apitishwe kinguvu na wengine wanadiriki kusema CCM isipomtisha CCM itashindwa.
CCM haiwezi kushindwa kipindi hiki kwa nguvu kubwa iliyonayo, ni kubwa mno mpaka inatisha.
Historia ya CCM ni muujiza unaoishi na kama ingekuwa kufa ingetakiwa kuwa 2015 Lowassa alipokatwa kwa sababu kuu mbili
1. 2015 CCM haikujiandaa kuondoka kwa Lowassa kwenda upinzani na kitendo hiko Cha ghafla kiliweza kustahilika na CCM kushinda
2. CCM imefanya mabadiliko mengi katika ya kuondoa ukuu wa mtu na kujenga ukuu wa Chama na hivyo kufanya wanachama wote waone hakuna nafasi nyingine nje ya CCM.
Hizo sababu ndizo zimeweza kuimarisha CCM hivi ilivyo Leo, CCM sasa kimejiandaa kwa yeyote kukihama Chama na Bado kikawa na uhakika wa ushindi ndio maana Leo CCM hakihofii kuchukua aliyekuwa wa mwisho kura za maoni.