Shetani aliamua kuasi au aliumbwa kuwa muasi?

Mfano tu wa Baba Na mwana
Baba akinunua kisu
Ana mwambia mwanaye mwanangu
Usicheze Na kisu icho kitakukata

Je siku ikitokea mtoto kakatwa Na kisu Kile
Je utasema Baba alijua kuwa mwanaye kisu kile kitamkata?
Jibu ni apana but alijua kisu ni kibaya

Na ndivyo ilivyo kuwa kwa Mungu Na shetani
Mungu alimuumba shetani akutegea shatani kama ana weza Kuja kumsaliti au kumkosea
Yaani makosa Na mema ni kama sheria za Mungu ana jua ukifanya ivi utakuwa you Will Make him to be happy but if you Do this utakuwa umemkosea
Sasa shetani alifanya vile ambavyo Mungu apendi ndo maana Mungu alimtupa Chini

Kwa iyo shetani akuumbwa ili akosee apana Bali tamaa zake ndizo zilizo mfanya kuwa mkosaji kwa Mungu Wala si mpango wa Mungu

Na kuhusu Adam Na Eva Mungu aliwaumba Na akawapa Na sheria kuwa ukila tunda ili utakuwa umenikosea

Mungu alijua kuwa kukosa kupo
Ila akupanga wa kosee Bali tamaa Zao ndizo zilizo waponza wakala wa kashindwa kuheshimu walicho ambiwa Na Mungu

Apo vipi utasema Mungu alipanga wa kosee angelikuwa amepanga wa kosee asingeli wa ambia kuwa wa kila tunda ilo watakufa au watamkosea
Si mpango wake kwanini wa Sasa awambie

Kila kinacho kifanya mwanadamu kilipangwa Na Mungu Bali akupanga
Yaani mabaya Na Mazuri Na kizuri zaidi Mungu ana tuambia Kabla ujakosea una ambiwa ukifanya uzinzi ni kosa lakini wewe unafanya utasema aje apo Mungu ndiye aliye panga wewe kufanya uzinzi?

Kwa iyo ndivyo ilivyo Mambo ya Mungu ivyo
Alifanya mabaya kwa Mazuri
Pili akakuonyesha mabaya Na Mazuri kuwa ukifanya iki ni kosa Na ukifanya iki ni kizuri Na cha mwisho akakupa Na Akili kabisa ya kuhelewa ubaya Na uzuri

Ila sorry kama nime kosea nilitaka kuwaonyesha wale wanao sema
Kila kitu kimepangwa Na Mungu
Kuwa ukikosea ni Mungu ndiye aliye panga kitu ambacho si Kweli
Hivi kazi ya lile tunda ambalo Mungu aliwaambia Adam na Hawa wasilile ilikuwa ni nini?

Hakukuwa na mahali pengine pakuuweka ule mti mpaka akauweka bustanini?
 
Kwanza naanza kwa masikitiko makubwa sana kwa kuto nitag na umeenda kuwatag watu wasio na uelewa wa mambo haya,labda umaarufu wao humu jf.
Ila niseme tu alichofanya yesu ndicho kile alichofanya shetani. Kuishi,kutenda n.k. kwa ajiri ya wengine.
 
Kwaiyo unamaanisha Mungu hajui yajayo yan na yeye anaishi kama sisi tu kwa kuhisi ila sio kwa kujua future nini kitatokea ili tukifanyie marekebisho kabla hakijatokea?
Kama anajua basi jua kabisa shetani aliumbwa "purposely" kabisa ili kuwepo pande mbili zinazojua nini zinafanya kwa makubaliano maalumu kabisa 😂😂 Yani ni kama muvi vile, DIRECTOR anapanga kila kitu, nani atacheza kama 'Starring' nani acheze kama 'Adui' lakini wote wanajua kabisa kwamba hii ni filamu, 😂😂
 
Kwanza naanza kwa masikitiko makubwa sana kwa kuto nitag na umeenda kuwatag watu wasio na uelewa wa mambo haya,labda umaarufu wao humu jf.
Ila niseme tu alichofanya yesu ndicho kile alichofanya shetani. Kuishi,kutenda n.k. kwa ajiri ya wengine.
Binadamu tuna mapungufu yetu mkuu.

Tusameheane.

Haya tujadili mada
 
Hivi kazi ya lile tunda ambalo Mungu aliwaambia Adam na Hawa wasilile ilikuwa ni nini?

Hakukuwa na mahali pengine pakuuweka ule mti mpaka akauweka bustanini?
Tukupe muda uwasiliane na Mungu kwa maombi aweze kukupa jibu la hili swali?
 
Maandiko ya Biblia ni zaidi ya mawazo ya binadamu.

Kumbuka waandishi wengi hawakuwahi kuonana na hata hawakuweza kusoma maandiko ya kila mmoja wao ingawa ufananio wake wa maandiko ni wa kiwango kikubwa na kushangaza.

Turudi kwenye mada ya shetani kwa sababu seems naye anapambana asijadiliwe
mkuu maandiko kwa sehemu kubwa aliyanajisi shetani ili apate kuutawala ulimwengu
 
Kuna mambo magumu kuyaelewa,

Mungu anapanga kuwaokoa Wana wa Israel na janga la njaa kwa kumpeleka yoseph misri,

Yoseph anauzwa utumwani na ndugu zake, kitendo cha kumuuza ndugu yao ni dhambi au siyo dhambi maana mungu ndiyo kapanga yoseph aende misri,

Mke wa potifa anataka kumbaka yoseph anatupwa jela, je yule mwanamke kafanya dhambi au hana dhambi maana mungu ndiye kapanga yoseph aende gerezani akapate ufunuo,

Mfano hai unaweza kuwa nao wewe, umeuona Malaya mkakubaliana utampa 50k, akakupa huduma ukampa chake, kaenda nyumbani mwanae anaumwa anatumia pesa hiyo anamtibu anapona, bila pesa yako huwenda mtoto angefariki, je yule Malaya ana dhambi je mwanaume na wewe unadhambi maana bila Malaya na wewe kutenda dhambi mtoto angekufa,

Kama wewe ni mkristo unayesema umekombolewa na damu ya yesu kristo kama yuda iskariote asinge tenda dhambi ya kuuza yesu, leo hii ungekombolewa kutoka kwenye utumwa wa dhambi?
 
Akili ya Mungu ni kubwa sana haichunguziki lakini ametupa sisi wanadamu akili ya udadisi

Udadisi wetu mpaka sasa umetuletea majibu mengi sana ambayo mengine yanatutoa knock out kabisa kwenye mstari wa imani kwa Mungu.

Lakini mimi Msanii, ninawashuhudia nyie mnaosoma hapa kuwa kupitia matendo na ufahamu wangu nimeuona ukuu wa Mungu na haya Upendo wake kwangu.

Nimetafuta kwenye maandiko aliyotupatia (Biblia kwa upande wangu) sijaona mahala ambapo tumekatazwa kujadili kuhusu Mungu na yote yanayomhusu. Nifahamucho ni kwamba, hatutaweza kufikia ukomo wa tafakuri kuhusu Mungu.

Mwanzo 3:1
Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya BWANA Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani?

Mstari huu ndipo kwenye Biblia panaanza kutajwa shetani...... hii Biblia yangu ya mtandaoni inaonekana kukwepa jina hilo.

Najua hapa jukwaani kuna wabobezi wa masuala ya Imani na historia yake. Je tunawezaje sasa kumdadavua shetani.

Kutokea kuumbwa ulimwengu, lini aliasi? Aliasi kabla au baada ya binadamu kuumbwa?

Je, shetani aliyetengenezwa kwa moto na utukufu mwingi, aliandaliwa kuja kuwa jaribu la viumbe (binadamu) wa Mungu?

Je, shetani aliwezaje kushawishi theluthi ya malaika wakaungana naye wakati Malaika wanajua kabisaa Aliyewaumba ana uwezo mkuu usio na mipaka?

Je, kuna uwezekano huyu shetani ni among titans?

Naomba elimu kupitia posts zenu.

CC
Mzito Kabwela
zitto junior
Kiranga
Mshana Jr
Pascal Mayalla
Kwanza hakuna kitu kigumu cha kutafakari historia yake kama masuala ya ki- Mungu. Kulingana na imani ya Kikristo ni kwamba Mungu yeye alikuwapo tangu milele yote, yaani hana mwanzo wala mwisho, hakuanza wala hatakwisha.

Naamini Mungu yupo, huenda Mungu sio jina lake ila naamini hizo Nguvu. Kwa ufupi Mungu hana origin yaani hakujioriginate kutoka kwa kitu chochote. Yeye ndio anajua ilikuwaje.
 
😊Yooote ilikuwa n mipango ya Mungu, kwahyo lolote lililotokea linalotokea na litakalotokea n mipango iliyokwshapangwa tayar.

Kuna sehem kwny biblia skumbuki kitabu gani "........Mungu anawajua walio wake" sasa hii inaonesha hata swala la watakaoona pepo(mbingu) au watakaochomwa kwny jehanam ya moto, woote wanajulikana hata kabla ya kuzaliwa kwao.

Yoote tunayopitia n yamekwshapangwa, na kilichopangwa hakipanguki hata ukijitahdi hahahhahahah hapa kama n wa motoni hata ukitenda mema sku unakaribia kufa unashangaa umemtukana nurse hahahahhahah, na ndyo unajikuta kwny moto.
 
Sheatani alikua ni kiumbe namba mbili pendwa kwa Mungu baada ya Yesu, hua anaitwa Left hand of God while Yesu ni right hand of God.
Dini zote zenye asili ya ibrahim zinaelezea kwamba shetani alitamani free will ya binaadamu aipate nayeye.
Ila ukweli kabisa Lucifer anaitenda kazi ya Mungu najua hamtanielewa. Ila jueni Lucci anashirikiana na Mungu kufanya kazi zake.

Kama unanibishia Je Unadhani watu wangemtegemea Mungu au kumkubali Mungu bila uwepo wa Shetani??? Mtu akipinga haya maelezo yangu anakua kakufuru maaana anakua anakaa zike sifa tatu za Mungu kwamba anaweza,anajua yote
Hayo maelezo ya shetani yamefunga mjadala na iyo free will aliyokuwa anaitaka ndio ilisababisha akafukuzwa huko mbinguni ila akapewa mamlaka ya kutawala viumbe visivyoonekana huko baharini(jini)...

Lucifer hata majini wenyewe wanamuogopa
 
Akili ya Mungu ni kubwa sana haichunguziki lakini ametupa sisi wanadamu akili ya udadisi

Udadisi wetu mpaka sasa umetuletea majibu mengi sana ambayo mengine yanatutoa knock out kabisa kwenye mstari wa imani kwa Mungu.

Lakini mimi Msanii, ninawashuhudia nyie mnaosoma hapa kuwa kupitia matendo na ufahamu wangu nimeuona ukuu wa Mungu na haya Upendo wake kwangu.

Nimetafuta kwenye maandiko aliyotupatia (Biblia kwa upande wangu) sijaona mahala ambapo tumekatazwa kujadili kuhusu Mungu na yote yanayomhusu. Nifahamucho ni kwamba, hatutaweza kufikia ukomo wa tafakuri kuhusu Mungu.

Mwanzo 3:1
Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya BWANA Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani?

Mstari huu ndipo kwenye Biblia panaanza kutajwa shetani...... hii Biblia yangu ya mtandaoni inaonekana kukwepa jina hilo.

Najua hapa jukwaani kuna wabobezi wa masuala ya Imani na historia yake. Je tunawezaje sasa kumdadavua shetani.

Kutokea kuumbwa ulimwengu, lini aliasi? Aliasi kabla au baada ya binadamu kuumbwa?

Je, shetani aliyetengenezwa kwa moto na utukufu mwingi, aliandaliwa kuja kuwa jaribu la viumbe (binadamu) wa Mungu?

Je, shetani aliwezaje kushawishi theluthi ya malaika wakaungana naye wakati Malaika wanajua kabisaa Aliyewaumba ana uwezo mkuu usio na mipaka?

Je, kuna uwezekano huyu shetani ni among titans?

Naomba elimu kupitia posts zenu.

CC
Mzito Kabwela
zitto junior
Kiranga
Mshana Jr
Pascal Mayalla
Shetani ni sifa si kiumbe wa aina fulani. una Binaadam shetani pia kuna Jinni shetani.
 
Hapana sio kweli kua shetani alipenda freewill ya binadamu, kwasababu shetani ndiye aliyekuja kumpa binadamu freewill kwa kumwambia ale lile tunda la ujuzi wa mema na mabaya

Kwa hiyo kabla ya kula tunda, adam hakuweza kujua lipi jema lipi baya

Ewe binadamu unamchukia shetani kwa lipi, wakati hata huu utashi ulionao saizi umetokana na yeye kuku-inspire kula tunda?

Kumbuka lengo la mungu lilikua binadamu aishi kama zuzu, mungu ndio aliyetaka tuwe blind fooled kwa kutunyima maarifa ya kuweza kutambua mema na mabaya, lengo la mungu ni kutuepusha na maarifa imagine wakina adamu walikua wakiishi uchi karne nyingi lakini hawakuwahi kujua mpaka pale aalipopewa maarifa na shetani

Sasa kwa wale ambao mmekua mkitetea hoja ya problem of evil kwa kusema evil imetokana na utashi ambao mungu ametupa, kumbukeni ya kua huo utashi hamkupewa na Mungu, ni shetani ndio aliye wapa maarifa ya kujua mema na mabaya kwa kuwaambia wale tunda la ujuzi wa mema na mabaya

Someni vizuri vitabu vyenu mtagundua upande aliopo shetani ndio upande wa mungu, mungu ndio aliyepaswa kuchomwa moto wa jehanamu
Aiseee umewaza kitu ambacho sijawahi hata kuwaza.......kwa ulichoandika hapa unamuabudu nani Mungu au Shetani..
 
Kuna mambo magumu kuyaelewa,

Mungu anapanga kuwaokoa Wana wa Israel na janga la njaa kwa kumpeleka yoseph misri,

Yoseph anauzwa utumwani na ndugu zake, kitendo cha kumuuza ndugu yao ni dhambi au siyo dhambi maana mungu ndiyo kapanga yoseph aende misri,

Mke wa potifa anataka kumbaka yoseph anatupwa jela, je yule mwanamke kafanya dhambi au hana dhambi maana mungu ndiye kapanga yoseph aende gerezani akapate ufunuo,

Mfano hai unaweza kuwa nao wewe, umeuona Malaya mkakubaliana utampa 50k, akakupa huduma ukampa chake, kaenda nyumbani mwanae anaumwa anatumia pesa hiyo anamtibu anapona, bila pesa yako huwenda mtoto angefariki, je yule Malaya ana dhambi je mwanaume na wewe unadhambi maana bila Malaya na wewe kutenda dhambi mtoto angekufa,

Kama wewe ni mkristo unayesema umekombolewa na damu ya yesu kristo kama yuda iskariote asinge tenda dhambi ya kuuza yesu, leo hii ungekombolewa kutoka kwenye utumwa wa dhambi?
Hii ngoma DEEP sana aisee.
 
Kwanza hakuna kitu kigumu cha kutafakari historia yake kama masuala ya ki- Mungu. Kulingana na imani ya Kikristo ni kwamba Mungu yeye alikuwapo tangu milele yote, yaani hana mwanzo wala mwisho, hakuanza wala hatakwisha.

Naamini Mungu yupo, huenda Mungu sio jina lake ila naamini hizo Nguvu. Kwa ufupi Mungu hana origin yaani hakujioriginate kutoka kwa kitu chochote. Yeye ndio anajua ilikuwaje.
Kuhusu uwepo wa Mungu ni unqueationable.

Kinacholeta ukakasi ni huyu muasi anayetajwa kutaka kumpindua Mungu.

Nahisi hata serikali za dunia zimeweka tendo la Uhaini kama kosa la juu kabisa dhidi ya Jamhuri. Kwanini isiwe kosa la kuua?
 
Mfano tu wa Baba Na mwana
Baba akinunua kisu
Ana mwambia mwanaye mwanangu
Usicheze Na kisu icho kitakukata

Je siku ikitokea mtoto kakatwa Na kisu Kile
Je utasema Baba alijua kuwa mwanaye kisu kile kitamkata?
Jibu ni apana but alijua kisu ni kibaya

Na ndivyo ilivyo kuwa kwa Mungu Na shetani
Mungu alimuumba shetani akutegea shatani kama ana weza Kuja kumsaliti au kumkosea
Yaani makosa Na mema ni kama sheria za Mungu ana jua ukifanya ivi utakuwa you Will Make him to be happy but if you Do this utakuwa umemkosea
Sasa shetani alifanya vile ambavyo Mungu apendi ndo maana Mungu alimtupa Chini

Kwa iyo shetani akuumbwa ili akosee apana Bali tamaa zake ndizo zilizo mfanya kuwa mkosaji kwa Mungu Wala si mpango wa Mungu

Na kuhusu Adam Na Eva Mungu aliwaumba Na akawapa Na sheria kuwa ukila tunda ili utakuwa umenikosea

Mungu alijua kuwa kukosa kupo
Ila akupanga wa kosee Bali tamaa Zao ndizo zilizo waponza wakala wa kashindwa kuheshimu walicho ambiwa Na Mungu

Apo vipi utasema Mungu alipanga wa kosee angelikuwa amepanga wa kosee asingeli wa ambia kuwa wa kila tunda ilo watakufa au watamkosea
Si mpango wake kwanini wa Sasa awambie

Kila kinacho kifanya mwanadamu kilipangwa Na Mungu Bali akupanga
Yaani mabaya Na Mazuri Na kizuri zaidi Mungu ana tuambia Kabla ujakosea una ambiwa ukifanya uzinzi ni kosa lakini wewe unafanya utasema aje apo Mungu ndiye aliye panga wewe kufanya uzinzi?

Kwa iyo ndivyo ilivyo Mambo ya Mungu ivyo
Alifanya mabaya kwa Mazuri
Pili akakuonyesha mabaya Na Mazuri kuwa ukifanya iki ni kosa Na ukifanya iki ni kizuri Na cha mwisho akakupa Na Akili kabisa ya kuhelewa ubaya Na uzuri

Ila sorry kama nime kosea nilitaka kuwaonyesha wale wanao sema
Kila kitu kimepangwa Na Mungu
Kuwa ukikosea ni Mungu ndiye aliye panga kitu ambacho si Kweli
Nauliza maswali kulingana na maelezo yako...
1_ Baba anaponunua kisu na kumwambia mtoto wake asikichezee tambua kwamba yeye anatoa tahadhali tu kwa mtoto na hajui baada ya tahadhali hiyo kama mtoto atachezea ama hatachezea....unafikiri kama angejua mtoto ni lazima atachezea angenunua? Ni wazi kwamba asingenunua... Mungu anajua kila kitu, nafikiri alijua wazi kwamba uwepo wa shetani ni lazima utawafanya watu wamuasi....why bado alimruhusu aendelee kuwepo?

2_kwa maelezo yako unasema Mungu hakutegemea kama shetani atakuja kusaliti, unamaanisha Mungu hajui mambo yajayo? Uasi wa shetani ni kitu ambacho Mungu hakujua kama kitatokea?

3_ Mungu wakati anawaambia Adam na Hawa wasile tunda hakuwa anajua kwamba watakula? Kama hakujua inamaanisha kuna mambo ambayo Mungu hayajui? Kama alijua, ni dhahili kwamba Mungu alifanya jambo hilo kimakusudi ili ionekane Adam na Hawa hawajamtii
 
Back
Top Bottom