Shetani akizeeka anakuwa malaika

Shetani akizeeka anakuwa malaika

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,602
Reaction score
830,313
1472365564674.jpg
ni siku nyingine njema siku ya Jumapili siku ya kumwabudu Mungu na kutubu, wengine ilikuwa jana wengine ilikuwa juzi nknk! Kila mtu ana siku yake ya kuabudu kwa imani yake!ni siku maalum kwa waamini na waaminio
Ulaya ya leo ni ngumu mno kukuta vijana kwenye nyumba za ibada! Waende kufanya nini wakati hawajazeeka? Kwao kanisani ni kwa wazee na kwakweli makanisani kule utakuta vikongwe tuu.. (mashetani ya zamani? )
Kuna kisa cha kweli kabisa cha yule jambazi wa zamani ambaye sasa ni mtu mzima kaokoka anampenda Yesu na ni mhubiri! Shetani kazeeka?!
Nakumbuka zamani kule vijijini kulikuwa na watu watemi hasa magangwe wanaoogopeka kupita kiasi ni watemi mtaa kwa mtaa kijiji kwa kijiji ! Siku hizi ukiwakuta wale ambao bado wako hai ni watu wazima wanaotegemewa mno na jamii wengi ni viongozi wa kidini kwa imani zao ! Wapole kweli kisha wanyenyekevu! Huwa najiuliza hivi huyu ndo yule wa kipindi kile kweli? Ama kwa hakika shetani akizeeka anakuwa malaika
Wengi wetu wiki hii kwa imani zao wameshindwa kabisa kwenda kufanya ibada kwa imani zao kwa visingizio mbalimbali lakini kiuhalisia ni sababu za kutunga, ni vishetani ambavyo havijazeeka ujana mwingi ujuaji mwingi.. miti kwa sana tuu....ila kumbuka fainali uzeeni zitabaki story za Aah mimi enzi zangu!
 
mshana jr asante kwa elimu ngumu uliyotupa Jumapili ya leo, unaonaje ukiongezea maelezo kidogo ukiambatanisha na vimifano hai ili niifaidi zaidi elimu hii?
 
Hili ni la kweli kabisa, Mtu akishafika kwenye uzee anaona yupo jirani na kifo hivyo anaanza kujiweka karibu na Mungu wake ili aweze kusamehewa yote aliyoyafanya alipokuwa Shetani(kijana).

Vijana wengi maisha yetu ni ya kishetani tu(starehe kwenda mbele) huwa hatukumbuki kabisa kama kifo, kifo tunakikumbuka tayali tukiwa wazee au tukiwa wagonjwa.
 
mshana jr asante kwa elimu ngumu uliyotupa Jumapili ya leo, unaonaje ukiongezea maelezo kidogo ukiambatanisha na vimifano hai ili niifaidi zaidi elimu hii?
Odili mifano ni mingi sana hata wewe unaweza kuwa na michache unayoijua! Kuna watu wengi ujanani walikuwa moto wa kuotea mbali kwenye mambo ya kishetani lakini ukiwaona leo ni kama mazezeta! Wao na dini dini na wao
Umesoma habari za mzee Yusuph?
Unapofikia hatua ya uzee unakuwa umeshapitia maisha mengi sana unakuwa unajua kila kitu kwahiyo hakuna jipya tena kwako yote yanakuwa ya kawaida ila Mungu hubaki Mungu..ndio yule yule Mungu wa ujanani! Mungu ni yule yule jana leo na hata milele amina
Ukiona mzee anafanya mambo ya ujanani ujue huyo hiyo stage ilimruka au aliiruka
 
Leo ndo nimeelewa hii sentensi ya shetani akizeeka kuwa malaika, asante sana mkuu
 
Mkuu mshana jr naona unanipa elimu kwa njia shirikishi. Hutaki kabisa kunilisha matilio moja kwa moja. Umegusia mzee Yusufu ni kweli kuna mahala nilisoma inadaiwa eti kaacha taarabu kamrudia Muumba wake.
 
Ukiona hivyo ujue anaelekea uzeeni si ajabu ukamkuta siku moja ni bonge la ustadh
 
Siku zote vijana wanakuwa na testosterone nyingi ndio maana wanakuwa majasiri wa ku experiment kila kitu.Vingi ya vitu wafanyavyo kama ulevi, ngono, lugha wanazotumia huonekana ni vitu hatari katika jamii.Wakishakuwa wazee hupungukiwa na hiyo homoni na kuingiwa na wasi wasi, hivyo kujiweka karibu na jamii kuhofia vitisho vya zamani...Hakuna cha shetani hapo!
 
umenitouch pale pale, mh
1472370529142.jpg
hiki ndio anachijifariji nacho shetani na kupotosha wengi
Wakati neno la Mungu likisema nyama kwa nyama na udongo kwa udongo yeye anasema atomi kwa atomi! Ni neno la kujifariji ujanani ambalo huwapa mzuka wa ajabu
Lakini uzeeni huwakuta wote wamepiga magoti wanamuomba Mungu waliyemdhihaki na kumkana maisha yao yote
 
Odili mifano ni mingi sana hata wewe unaweza kuwa na michache unayoijua! Kuna watu wengi ujanani walikuwa moto wa kuotea mbali kwenye mambo ya kishetani lakini ukiwaona leo ni kama mazezeta! Wao na dini dini na wao
Umesoma habari za mzee Yusuph?
Unapofikia hatua ya uzee unakuwa umeshapitia maisha mengi sana unakuwa unajua kila kitu kwahiyo hakuna jipya tena kwako yote yanakuwa ya kawaida ila Mungu hubaki Mungu..ndio yule yule Mungu wa ujanani! Mungu ni yule yule jana leo na hata milele amina
Ukiona mzee anafanya mambo ya ujanani ujue huyo hiyo stage ilimruka au aliiruka
In kweli kabisa mfano pia yule mwana hip hop Saigon sasa ivi sala tano...jamani tukumbuke mungu yupo na pia ametupa miongozo yakufuata ili tuenende vile anapenda...jumapili njema wadau
 
View attachment 389080ni siku nyingine njema siku ya Jumapili siku ya kumwabudu Mungu na kutubu, wengine ilikuwa jana wengine ilikuwa juzi nknk! Kila mtu ana siku yake ya kuabudu kwa imani yake!ni siku maalum kwa waamini na waaminio
Ulaya ya leo ni ngumu mno kukuta vijana kwenye nyumba za ibada! Waende kufanya nini wakati hawajazeeka? Kwao kanisani ni kwa wazee na kwakweli makanisani kule utakuta vikongwe tuu.. (mashetani ya zamani? )
Kuna kisa cha kweli kabisa cha yule jambazi wa zamani ambaye sasa ni mtu mzima kaokoka anampenda Yesu na ni mhubiri! Shetani kazeeka?!
Nakumbuka zamani kule vijijini kulikuwa na watu watemi hasa magangwe wanaoogopeka kupita kiasi ni watemi mtaa kwa mtaa kijiji kwa kijiji ! Siku hizi ukiwakuta wale ambao bado wako hai ni watu wazima wanaotegemewa mno na jamii wengi ni viongozi wa kidini kwa imani zao ! Wapole kweli kisha wanyenyekevu! Huwa najiuliza hivi huyu ndo yule wa kipindi kile kweli? Ama kwa hakika shetani akizeeka anakuwa malaika
Wengi wetu wiki hii kwa imani zao wameshindwa kabisa kwenda kufanya ibada kwa imani zao kwa visingizio mbalimbali lakini kiuhalisia ni sababu za kutunga, ni vishetani ambavyo havijazeeka ujana mwingi ujuaji mwingi.. miti kwa sana tuu....ila kumbuka fainali uzeeni zitabaki story za Aah mimi enzi zangu!
Thats very true.
Pia nimeshuhudia ndugu wanabifu tangu ujanani chui na paka, hawatembeleani, kila mtu akimtakia mabaya mwenzake, hakuna askofu wala mzazi aliyemudu kuwapatanisha , ila wanakuja kupatana uzeeni kwenye death bed wanapatanishwa na kuelewana.

Kama bifu la Joe Fraizer na Mohammad Ali.
 
mshana jr: kama bado ni kijana tumia muda wako vizuri, la kama mtu wa makamo jiandae maisha ya uzeeni (shetani/malaika).

"Graph" ya maisha iliyochorwa na watafiti, kabla ya binadamu kurudi mavumbini, inaonesha kwamba huingia duniana akiwa mtoto (malaika) na kuzeeka akiwa na tabia za kitoto (malaika). Tofauti na utotoni, ambapo binadamu hajui chochote, uzeeni hujutia/ukumbuka maisha ya ujana na ikibidi hubadilika na kuwa malaika tena.

Ushetani/umalaika matendo yetu wenyewe.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom