Sheria za Walionacho na Wasionacho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheria za Walionacho na Wasionacho

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by popo, Oct 15, 2008.

 1. p

  popo Member

  #1
  Oct 15, 2008
  Joined: Aug 30, 2008
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  Nchi yetu Tanzania imekumbwa na kashfa nyingi sana hivi karibuni kama vile EPA, Richmond pamoja na mikataba mingi ya ujanjaujanja (Songwe-Kiwira coal mines nk) na pia tumeshuhudia hatua za kisheria zinavyoendeshwa huku msimamizi mkuu wa sheria hizo akiwa wa kwanza kuwalinda mafisadi badala ya kuacha sheria zifate mkondo wake.

  Inasikitisha kuona watu wanafungwa kwa makosa madogomadogo ambapo kama busara ingetumika watu hao wangepewa adhabu za kusafisha mabarabara au mahospitali. Nafahamu sheria zetu zinawabana sana walalahoi kama sio wakesha hoi na kuwaacha Mafisadi wakitanua pamoja na makosa yote waliyoyafanya.

  Je rais wetu anafanya kazi kuhakikisha kanuni na Sheria za nchi zinafutwa? Au ndio yupo pale kwa sababu ya kuwatimizia mabwana wake wanachokitaka, inasikitisha sana kuona hata rais ni arrogance kwenye kuhakikisha sheria za nchi zinafuatwa.

  Nchi yoyote ambayo itazarau au kutokufuata sheria ambazo imejiwekea kamwe haitaweza kupambana zidi ya rushwa na mafisadi.

  Wadau hapo mnasemaje.
   
Loading...