Sheria za Tanzania zina double standard, hazina makali kwa watawala, zimeandaliwa kwa wananchi wa kawaida, Rais Samia unayo nafasi ya kuweka legacy

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,049
4,904
Salaam nyingi wana JF

Hili suala la kujiwekea kinga kwa watawala ni ishara ya kujitengenezea mamlaka isiyojali haki za binadamu, mamlaka isiyojali misingi ya sheria na utawala Bora, mamlakana ya kidikteta iliyojawa viongozi wenye viburi, jeuri na wasio wasikivu, ambao wanaweza kufanya kitu Cha hatari zaidi kwa taifa letu huku wakijua kua hakuna atakaewapeleka kokote Wala kuwafanya lolote tofauti Kama ingetokea kwa mwananchi mwingine wa kawaida!

Sasa, sisi wote ni binadamu wa kawaida tofauti ni vyeo tu, katiba inasema hakuna mtu yoyote aliye juu ya sheria, wote tuko sawa mbele ya sheria, kwa nini kuwepo na hizo double standard?

WITO WANGU KWA MAMA SAMIA SULUHU HASSAN
Rais wetu wa JMT, unayo nafasi ya kuweka legacy, kwa kuondoa hili suala la KINGA kwa viongozi wakubwa, ili iwape hofu na utawala uendeshwe kwa mujibu wa sheria, huku watekelezaji wa sheria hizo mkiwa ninyi viongozi wa ngazi za juu, na sio wavunjaji Kama ilivyo Sasa.
 
Hakuna cha wito tuandamane kuondoa hizi sheria kandamizi haraka.
Mfano Sheria ya Utumishi wa Umma (The Public Service Act) haina kosa hata moja la mwajiri (serikali) bali makosa yote katika sheria hiyo ni ya mtumishi. Yaani kwa sheria hiyo, Serikali kama mwajiri haikosei hata siku moja ila mtumishi tu ndiye anayekosea huku Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini inayotumika kwa Sekta Binafsi ikiwa na makosa kwa wote mwajiri na mwajiriwa. Matokeo ya Sheria ya Utumishi wa Umma kuwa ya upande mmoja ndio kama vile kusimama kwa nyongeza za mishahara, serikali kugoma kupandisha madaraja kwa zaidi ya miaka 5 nk bila woga maana hakuna kosa kisheria.
 
Mfano Sheria ya Utumishi wa Umma (The Public Service Act) haina kosa hata moja la mwajiri (serikali) bali makosa yote katika sheria hiyo ni ya mtumishi. Yaani kwa sheria hiyo, Serikali kama mwajiri haikosei hata siku moja ila mtumishi tu ndiye anayekosea. Matokeo ndio kama vile kusimama kwa nyongeza za mishahara, serikali kugoma kupandisha madaraja kwa zaidi ya miaka 5 nk
Sheria kandamizi za kipumbavu sn
 
Madudu ni Mengi mno, Sijui nani atamfunga paka kengele, sheria zetu zinatakiwa kuwa na uwiano, sio kuegemea upande mmoja!
 
Huyu mama hawezi kwenda kinyume na CCM hata dak moja
ANAWEZA.
KAMA ameamua kuijenga haki na uhuru zaidi katika nchi yake, atapeleka mswada wa kufanya mabadiliko anayoyataka.
Bunge likiukataa kwa mujibu wa katiba, litavunjwa na uchaguzi mkuu unaitishwa upya.
Kutakuwa na mgawanyiko mkubwa ndani ya lichama; kundi la kwanza ni la wazalendo wa kweli (walio upande wa Rais wa sasa) na la pili la waigizaji (masalia wa Jiwe na mashabiki wa ukandamizaji wake).
Kilicho bora ni kuwa ujio wa Mama Samia ambao umeanza kuwafanya hata watz waliopotoshwa na kutishwa, kufumbuka macho, uoga wao sio tu utawapungua BALI watakuwa pia na ujasiri wa kuhakikisha kuwa wawademkaji wote waliopo akiwamo Ndugai, Tulia; hawatarudi.
Hili wote wanalielewa vizuri. AMEN
 
hakuna jipya
 
Back
Top Bottom