Sheria za nchi yetu zinaruhusu kuwachapa viboko watu wazima hadharani?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,695
6,398
Najua kuna Jamii zenye taratibu za kuadhibiana kwa viboko kwa mujibu wa taratibu zao, pale inapotokea mwanajamii wao kakiuka taratibu walizokubalina.

Vipi kwa upande wa viongozi wa Serikali, kuna kifungu cho chote cha Kisheria kinachowapa mamlaka ya kutoa adhabu ya viboko kwa "wakosaji"?


 
nimetazama izo video zote,iyo video ya Moshi uyo mfiraji alitakiwa afunguliwe mashtaka apewe adhabu kubwa zaidi ya viboko.
 
kuna kifungu cho chote cha Kisheria kinachowapa mamlaka ya kutoa adhabu ya viboko kwa "wakosaji"?
Ndio

Kanuni ya Adhabu (Penal Code)

Kifungu

28. Kwa kuzingatia masharti ya Sheria ya Kima cha Chini cha Adhabu, pale katika kanuni hii inatamka kwamba mtu yeyote atahukumiwa adhabu ya viboko, adhabu hiyo, kama itatolewa, itatekelezwa kwa mujibu wa masharti ya Sheria ya Adhabu ya Viboko.
 
Kuna sheria ndogo ndogo kweny ngazi za chini kama serikali za vijiji na mitaa...Hizo ni sheria za kimaadili watu wanachapwa fresh tu unakileta nyodo ...Kila sehemu kuna sheria zake ndogo ndogo.
 
Mtu isipomfaa akili yake, utamdhuru ujinga wake.

Hayo tunayoshuhudia ni matokeo ya UJINGA wetu, kuwaacha viongozi wafanye wanavyotaka.

Acha tu bakora zitembee ili akili itukae sawa.
 
Utoto wangu wote shuleni Hamna mwalimu alinichapa,ni mamaangu pekeyake nayeye alikua anafundisha hapo nnasoma.
Ila wengine ngumi fimbo ,karate zitahusika hunipigi kibwege.
Nashangaa midume mizima inaenda kuweka matako yachapwe fimbo.
Yaani mi kwa hasira zangu tungekua tushazika.
 
Kuna sheria ndogo ndogo kweny ngazi za chini kama serikali za vijiji na mitaa...Hizo ni sheria za kimaadili watu wanachapwa fresh tu unakileta nyodo ...Kila sehemu kuna sheria zake ndogo ndogo.
Sheria imemruhusu DC au Waziri kuchapa raia waliokosea huku akichukuliwa video?

Wa kwa Sadaka ni sawa kwa sababu ni Sheria zao. Lakini DC na Waziri walipaswa kuwapeleka watuhumiwa kwenye vyombo vya Kisheria.
 
Back
Top Bottom