Sheria za kufunga bar saa tano zakolea moto

lendila

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
5,806
4,370
Sheria ya kufunga bar saa tano zakolea moto.

Juzi kuna baadhi ya bar zilichukuliwa hatua kali za kisheria kwa makosa ya kufunga bar saa saba kama sheria inavyokataza. Kama sheria hii ikifanyiwa kazi vizuri bila upendeleo itapunguza walevi wengi sana ndani ya nchi yetu.

Sheria yenyewe ni nzuri lakini watekelezaji sheria wanatakiwa wajitahidi kutekeleza sheria hii vizuri ili kuepusha mashaka ya upendeleo wa kutekeleza sheria na kuondoa mashaka ya rushwa kwenye utekeleza wa sheria yenyewe
 
Last edited:
Hata kama sheria hii isipotumika kwasasa wale waliokuwa wanafanya kufuru bar hawana ukwasi kwishilia mbali.
 
mashaka yangu kwenye utekelezaji wa sheria hii ni kwa siku za mipira
mipira mingi inachezwa saa tano usiku na kuendelea
itabidi sheria ivunjwe kutokana na matukio ya mipira
 
Sheria ya kufunga bar saa tano zakolea moto.

Juzi kuna baadhi ya bar zilichukuliwa hatua kali za kisheria kwa makosa ya kufunga bar saa saba kama sheria inavyokataza. Kama sheria hii ikifanyiwa kazi vizuri bila upendeleo itapunguza walevi wengi sana ndani ya nchi yetu.

Sheria yenyewe ni nzuri lakini watekelezaji sheria wanatakiwa wajitahidi kutekeleza sheria hii vizuri ili kuepusha mashaka ya upendeleo wa kutekeleza sheria na kuondoa mashaka ya rushwa kwenye utekeleza wa sheria yenyewe

Hao wenyewe wenye kusimamia hiyo sheria utakuta ndiyo wanywaji namba moja
 
Attachments

  • index.jpg
    index.jpg
    13.2 KB · Views: 23
Ingetakiwa Bar zifungwe saa mbili Usiku......

Hata matokeo ya DNA yanachangiwa na Wanaume wengi kukesha Bar.....

Bar zifungwe Mapema mrudi nyumbani mkalee Familia zenu..
 
Wafunge na viwanda vyote vya TBL maana hilo nalo ni jipu, watu warudi kwenye vinywaji vya tamaduni zetu kama vile kindi, lubisi, kibuku na siku hizi naona mitaani kuna nzagamba; vinywaji vya kitamaduni kama hizi watu huwa hawafikishi hata saa 4 usiku, yaani mida ya saa mbili hadi tatu mteja hana hamu tena ya kuendelea na mchezo. Lakini hizi za TBL jitu likata maji hadi majogoo hata haliwezi kufikiria kuwa linatakiwa ofini saa mbili asubuhi.
 
Ingetakiwa Bar zifungwe saa mbili Usiku......

Hata matokeo ya DNA yanachangiwa na Wanaume wengi kukesha Bar.....

Bar zifungwe Mapema mrudi nyumbani mkalee Familia zenu..
Ushindwe na ulegeee saaa mbili?
 
sio kila kitu cha kushabikia kimaandaz tu, mnajua kodi TBL na viwanda vya pombe inazolipa? bar zina create ajira nyingi sana hapa nchin, pombe ndio inaendesha uchumi wa bongo kwa msio faham hili sio jipu tena tunatakiwa tuwe makin sana na mambo ya kushabikia kimaanda maandaz kama hili, bar zifunge hata saa 12 asbui so that people can spend money na kuongeza consumption ambacho ni kitu muhim ktk uchum wowote ule dunian
 
Ingetakiwa Bar zifungwe saa mbili Usiku......

Hata matokeo ya DNA yanachangiwa na Wanaume wengi kukesha Bar.....

Bar zifungwe Mapema mrudi nyumbani mkalee Familia zenu..
sk mipira inachezwa itakuwaje?
 
Back
Top Bottom