Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,023
- 144,381
Badilisheni sheria wahame na ubunge wao na sio mnajifanya wazalendo kumbe ni matapeli tu.Hahahaaaa.... Kamanda Ryoba kakupagawisha!
Badilisheni sheria wahame na ubunge wao na sio mnajifanya wazalendo kumbe ni matapeli tu.Hahahaaaa.... Kamanda Ryoba kakupagawisha!
Sasa tujiulize kama anafanya haya wazi wazi, nyuma ya pazi atakuwa anatupiga kiasi gani ukizingatia hajali na wala hana uchungu
Utaratibu wa kuwaondoa hawa lazima ubadilike maana hatuwezi kuwa tunavumilia tu eti mpaka muda wake uishe.Ipo siku sisiemuu watasema bora tumetoka kule sasa tunaenda sehemu salama hii itakua baada ya jiwe kutokua madarakani
Kwani hawahami na ubunge wao?!!!!!Badilisheni sheria wahame na ubunge wao na sio mnajifanya wazalendo kumbe ni matapeli tu.
Pathetic creature! !Wewe Salary Slip unaonekana unaumia sana kuhusu hii serikali
Yaani sijui umefanywa nini kila siku majungu majungu na chuki.
Wewe kama umeichukia ni wewe usije kuleta kilasiku umbea. Hao wabunge wanahama kwa kuwa CHEDEMA kuna shida na washajua kuwa chama kinakufa 2020 sasa utawalisha wewe.
Wenzio siasa ni kazi na kwa kuwa ni kazi basi huwezi kukaa mahali ambapo unaona panakoelekea ni kufa. Ni sawa na wachezaji wa mpira kuhama club au wafanyakazi kuacha kazi shirika fulani na kwenda shirika lingine.
Utapata tabu sana...........Pathetic creature! !
Kama anaweza kufanya uchafu huu hadharani, then huko, huko kuliko na mtoto wa dada, huko kwa msajili wa hazina, huko BOT kuna nini???????????????????????????????????????Hili ndio swali ambalo kila mtu mwenye akili timamu anapaswa kujiuliza maana teyari ameshatuthibitishia kuwa hana huruma wala uchungu na kodi zetu.
Sasa tujiulize kama anafanya haya wazi wazi, nyuma ya pazi atakuwa anatupiga kiasi gani ukizingatia hajali na wala hana uchungu?
Wabongo mkija kushituka, jamaa teyari bilionea.
Hapa Kaduma amesema kweli,MWANASIASA mkongwe, Ibrahim Kaduma, ameibuka na kutoa kauli nzito kuhusu wabunge wanaojiengua upinzani na kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Amekishauri chama hicho kuwachunguza watu hao kwa miaka miwili hadi mitatu kabla ya kuwapa vyeo au kuruhusu kugombea nafasi yoyote.
Sambamba na hilo, ameshauri kufanyika marekebisho ya Katiba na kuruhusu mgombea binafsi na inapotokea mtu anahama chama, abaki na cheo chake ili kuepusha gharama kubwa za uchaguzi mdogo unaofanyika mara kwa mara.
Mwanasiasa huyo aliyasema hayo juzi wakati wa mjadala wa hali ya kisiasa, uchumi na maendeleo ya Tanzania, uliojumuisha wadau mbalimbali wa vyama vya wafanyakazi wa nchi mbalimbali duniani, ulioandaliwa na shirika la kimataifa la Ujerumani (FES).
Katika mjadala huo, miongoni mwa waliohudhuria ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Hamphrey Polepole, na wabunge kutoka Bunge la Uingereza.
Kaduma ambaye alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa serikali ya awamu ya kwanza, chini ya Mwalimu Julius Nyerere, alisema wanaokwenda CCM si wote wanajua falsafa ya chama hicho bali wanakwenda kuganga njaa.
“Hivi karibuni kumekuwa na wimbi la madiwani na wabunge kuhamia CCM. kwa maoni yangu sioni kama wanahamia kwa vile wanajua na kuipenda falsafa ya CCM bali kwenda kutafuta maslahi na vyeo,” alisema na kuongeza:
“Sijaona sababu za msingi za kuhama kwao, nawaona kama waganga njaa na si kukipenda chama. Nashauri turudi kwenye utaratibu wa enzi za Mwalimu Julius Nyerere ambako unapokuwa mwanachama kabla ya kupewa cheo, unapewa miaka miwili au mitatu ya kuchunguzwa.”
Kwa mujibu wa Kaduma, si sawa mtu kuhamia CCM na siku inayofuata anapewa cheo au anateuliwa kugombea nafasi aliyokuwa nayo kwa tiketi ya chama hicho bila kuulizwa kama anaijua falsafa ya chama na ni mhubiri wa falsafa hiyo.
“Hatuko kwenye kisiwa, wenzetu Ujerumani walishaachana na hili la mtu akihama wanarejea kwenye uchaguzi mdogo. Kwao akihama chama anaendelea na ubunge wake huku akiwakilisha wananchi. Kwa nini tusiige kutoka huko,” alisema Kaduma.
Pia alisema suala la gharama za uchaguzi mdogo ni mzigo kwa Watanzania na ili kuepukana na jambo hilo, ni kuruhusu mgombea binafsi ambaye ameamua kutokukubaliana na falsafa za chama chake lakini bado anaweza kuendelea kuwawakilisha wananchi.
“Hakuna ubishi kuwa gharama za uchaguzi ni mzigo kubwa kwa nchi na unabebwa na Watanzania wote. Ifike mahali tulibadili hili kwa kuepuka uchaguzi mdogo, labda iwe kwa lazima sana na suluhisho ni mgombea binafsi,” alisisitiza