Sheria ya Uchaguzi ni mbovu! Kuendelea kuitumia sio Ujinga? Kuwabebesha masikini gharama za Uchaguzi sio Dhambi?

Ndg zangu,

Kama Mimi Moblaze, ningetoa amri ya kurudia uchaguzi Wa Madiwani na Wabunge wote nchini kabla ya 2020 kisha tuanze kuhesabu upya miaka mitano yao!

Maana ya hoja yangu: Tusipoteze hela nyingi za Serikali katika hizi chaguzi ambazo tunatumia kodi za wananchi.

Tufanye uchaguzi Wa Uraisi tu 2020!

Inatucost sana kurudia sehemu moja moja!

Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania. Tunakuomba utudumishie Uhuru na umoja! Amen
 
good analysis mzalendo mwenzangu! Nadhani taifa letu sasa linageuka kuwa taifa la wehu! sijajua sababu ni nini haswa!

Akili za wananchi wenzetu zinaenda kinyume, technology inaongezeka mataifa mengine wanakimbia kwenda mbele na technology yao sisi waTanzania tumegeuka tuna kimbilia nyuumaa!
kuna mtu amechora jiwe limepanda farasi kwa kujigeuza yaani uso unaangalia nyuma mgongo mbele
 
Mkuu hili jambo ukiachilia mbali kuwa kero kubwa ya gharama ambazo ni kodi za wananchi, pia linaleta AIBU kubwa sana..
Ukimwambia ambae hajawahi kulisikia ni fedheha kubwa kwa Tanzania.
MENGELENII Na tabiru kwamba Siku za usoni atatokea kiongozi mzalendo kweli kweli awe wa upinzani au hata wa. ccm atawafatilia hawa watu wanachezea hela za wavuja jasho wanchi hii ,na kutupa lupango .
 
MENGELENII Na tabiru kwamba Siku za usoni atatokea kiongozi mzalendo kweli kweli awe wa upinzani au hata wa. ccm atawafatilia hawa watu wanachezea hela za wavuja jasho wanchi hii ,na kutupa lupango .
Mkuu umesema kweli..
Ila naona kama Kiongozi wa namna hiyo anachelewa sana Mkuu.
 
Wanabodi,

Declaration of Interest.
Mimi ni miongoni mwa Watanzania wazalendo wa nchi yangu, ambaye sio mwanachama wa Chama chochote cha siasa, kwa sababu siasa za vyama za Tanzania, tunaziona kama ni ujinga Fulani hivi, hivyo nawaomba sana univumilie, ninapoita siasa za ujinga ujinga, hii ni opinion yangu, everybody has the right to his/her own opinion, hivyo tukitofautiana kwenye hili, tutofautiene kwa hoja, mimi nimeleta hoja zangu kuwa siasa zetu kwenye maeneo Fulani Fulani zikiwezo siasa za uchaguzi ni ujinga ujinga kwa hoja, naomba tubishane kwa hoja.

Watanzania Tufanye Siasa za Ukweli, Tuachane na Siasa za Ujinga Ujinga.
Tufike mahali sisi Watanzania, wazalendo, wenye nia njema na maendeleo ya taifa hili letu masikini, hatuwezi kukaa kimya kwa kuendelea kukumbatia sheria mbovu, bad laws, za uchaguzi, na kuendelea kuwawabesha masikini wa Tanzania, mzigo wa gharama za uchaguzi wa marudio, kwa sababu za kijinga jinga kabisa, zinazotokana na siasa za ujinga ujinga!. Kitendo hiki cha masikini wa kutupwa wa Tanzania, wanaoishi kwenye lindi la umasikini uliotopea wa kipato cha chini ya dola moja kwa siku, halafu kuja kubebeshwa mzigo wa kugharimia chaguzi za marudio kutokana na sababu za kisiasa za ujinga ujinga, na sababu zenyewe kuwa ni sababu za kijinga kabisa, its not only ni nonsense, but also ni dhambi kwa Mungu, kuwabebesha masikini hawa gharama hizi za ziada kutokana na ujinga tuu wa watu fulani in the name of politics!..

Kwa Nini Sheria Yetu ya Uchaguzi ni Sheria Mbovu, Bad Law.
Kifungu 21 cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kinatoa haki ya kila Mtanzania mwenye sifa, kuwa huru kushiriki katika siasa kuanzia serikali za mtaa hadi serikali kuu, bila ubaguzi wowote.

Uhuru wa kushiriki shughuli za umma Sheria ya 1984 Na.15 ib.6 Sheria ya 1994 Na.34 ya ib.4
21.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 5, ya 39 na ya 67 ya Katiba hii na ya sheria za nchi kuhusiana na masharti ya kuchagua na kuchaguliwa, au kuteua na kuteuliwa kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao, kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria.

Lakini kukatokea kikundi Fulani cha wajinga Fulani, wakaipindua katiba kwa sababu Fulani za kijinga kabisa, wakainyofoa haki hiyo ya raia kwa kulazimisha, ili mtu ugombee nafasi yoyote ya uongozi wa umma, ni lazima udhaminiwe na chama cha siasa!, kiukweli kabisa na ki haki, this is nonsense!.

Rev. Mtikila alikipinga kifungu hiki na Mahakama Kuu ikatamka bayana kipengele hicho ni batili na kinakiuka katiba ya JMT. Wajinga wale, wakaamua kuihalalisha batili ile, kwa kukipenyeza kipengele hicho batili kwenye katiba, ili kuuhalalisha ujinga wao!.

Japo Lengo la Kudhaminiwa na Chama ni Nini, Huu Sii Ujinga Tuu?!.
Katiba katiba ilisema kila Mtanzania ana haki ya kushiriki uongozi, hili sherti la kudhaminiwa na chama lilitoka wapi, na kwa kwa nini watu walazimishwe kuwa wanachama wa vyama ili wadhaminiwe, ndipo waweze kugombea?. Mfano mimi, sina chama kwa sababu naziona siasa za vyama kwa ni ujinga Fulani hivi, ikitokea nina uwezo wa kuwatumikia wananchi wa eneo langu na kuwaletea maendeleo bila kupitia chama chochote, kwa nini nizuiliwe?!. Kiukweli kabisa, huu ni ujinga, it is nonsense, Watanzania tusikubali ujinga huu uendelee hadi 2020!, tupiganie milango ya wagombea binafsi ifunguliwe, 2020, watu wenye nia ya kugombea, tuwaletee wananchi maendeleo, bila kupitia hizi nonsense za vyama tuingie, tushindane kwa hoja na sio kushindana kuhonga, kama hali inavyoendelea sasa!.


Kiongozi Akiishachaguliwa, Anakuwa ni Kiongozi wa Watu, na Sio Kiongozi wa Chama, Kwa Sababu Anachaguliwa na Watu na Sio Chama!.
Ujinga mwingine mkubwa kabisa ni huu, hata kama mgombea amedhaminiwa na chama cha siasa kugombea, akiishapitishwa na Tume ya Uchaguzi kuwa Mgombea, japo anatambulika kama ni mgombea wa chama Fulani, lakini akiishachaguliwa, mwenyekiti wa mtaa, diwani, mbunge au rais, anakuwa sio kiongozi wa chama kilichomdhamini, bali anakuwa ni kiongozi wa wananchi. Mfano baada ya rais Magufuli kuchaguliwa kuwa rais kwa tiketi ya CCM, lakini hakuchaguliwa na wana CCM, amechaguliwa na Watanzania, na sio kiongozi wa CCM bali kiongozi wa Watanzania wote, vivyo hivyo kwa wabunge, madiwani na viongozi wa serikali ya mtaa, kitendo cha kujitoa chama na kupoteza ubunge, udiwani au uongozi wa umma, ni ujinga ambao haupaswi kuvumiliwa. Nini muhimu kati ya umma na chama?. Kuukosesha umma kiongozi waliemchagua kwa sababu za chama, sio tuu sio haki kwa wananchi waliomchagua, bali ni ujinga uliopitiliza, halafu kuja kulipisha wananchi hawa ngarama za uchaguzi wa marudio ni ujinga mwingine na dhambi juu yake ukizingatia kiwango cha umasikini wa nchi yetu.

Nini Kifanyike, A Way Forward.
Kama nilivyowahi kushauri humu, ukosoaji wenye kujenga, huandamana na ushauri wa nini kifanyike kurekebisha kasoro hizi ili kuundoa ujinga huu unaoendelea nchini mwetu kwa sasa.
  1. Iwekwe faini maalum kwa kila kiongozi wa umma, atakayejiuzulu nafasi yake kwa sababu za kijinga jinga, ikiwemo kukatwa mafao yake na ikibidi kufilisiwa ili kugharimia gharama za uchaguzi wa marudio kwa kulitia hasara taifa.
  2. Viongozi wote wanaojiuzulu, wasiruhusiwe tena kugombea nafasi walizojiuzulu, kama sababu za kujiuzulu mimi nimeziita ni za kijinga, tusiwakubalie wajinga hawa kugombea tena, ili wasije kutuletea tena ujinga ule ule na kutugharimisha masikini sisi kugharimia uchaguzi wa marudio.
  3. Tubadili sheria yetu ya uchaguzi, kwa kufuta chaguzi zote ndogo, na tuanzishe proportional representation kwa mwenye kura nyingi ndiye mshindi, lakini likitokea lolote, akasita kuwa rais, mbunge au diwani, yule aliyemfuatia katika uchaguzi uliopita ndio anatangazwa mbunge, kama hayupo anachuliwa mtu wa tatu, hadi wa mwisho, kama wote hawapo, ndipo uchaguzi mdogo unafanyika.
  4. Kile kipengele cha kudhaminiwa na chama kiishie kwenye uteuzi tuu, kiongozi akiishachaguliwa, anakuwa kiongozi wa watu, anaweza kuhama chama bila kupoteza uongozi wake kama ilivyo nchini Kenya.
  5. Tubadili sheria yetu ya uchaguzi, kwa kuondoa kipengele cha kudhaminiwa na vyama ili kila Mtanzania mwenye sifa za kugombea uongozi wa nafasi yoyote, aruhusiwe, ila kwenye urais, tuweke vigezo vya ziada, ili asijetokea tajiri mmoja mwenye ukwasi wa kuwanunua watanzania wote, tukajikuta tuna rais wa kununuliwa. Ila kwenye ubunge, udiwani na serikali za mtaa, kila mtu awe free kugombea, hivyo tuwe na wagombea huru, na hili likifanyika hata sisi tusio na vyama tutashiriki, mfano mimi, naweza kabisa kugombea jimbo fulani na kulitwaa kama kuokota embe dodo lililojiangukia, ambapo mbunge wa hapo, nitamsukuma kama nimesukuma mlevi!.
Hitimisho.
Tanzania is too poor spend billions on by elections for foolish and nonsense reasons, nikimaanisha nchi yetu Tanzania ni masikini wa kutupwa, kuhalalisha matumizi ya mabilioni ya fedha kuendesha chaguzi ndogo kwa sababu za kijinga. Ili Taifa letu lipate maendeleo ya kweli, ni lazima sisi Watanzania tukubali kuwa wakweli toka ndani ya nafsi zetu, tusikubali ujinga huu wa kuhama vyama, uendelee kutugharimisha sisi masikini wa kutupwa, tunaishi kwenye lindi la umasikini uliotopea, halafu kuendelea kugharimishwa na wajinga Fulani kwa sababu za ujinga wao!.

Nawatakia Furahi Dei Njema.

Paskali
Rejea.
Rev. Mtikila ashida kesi ya kuruhusu mgombea binafsi mahakama ya ...
Mtikila: Shujaa wa Demokrasia, Mwanamapinduzi halisi na Shujaa ...
Mgombea binafsi Tanzania: Tatizo ni nini? | Page 9 | JamiiForums ...
Swali kwa Wana UKAWA: Is UKAWA for Real or Just A Marriage of ...
watu wa aina yako msitegemee ukuu wa wilaya mchawi wa maendeleo ya afrika ni mwanasiasa
 
Wadau habari za asubuhi.
Nakerwa na siasa za Tanzania, kuna umuhimu gani wa kurudia uchaguzi kama MTU ameamua kujiuzulu mwenyewe,huu ni mwendelezo wa sheria mbovu,
Nilifikiri sheria ingeweka criteria za kurudia uchaguzi kama MTU kufariki au kushindwa ketekeleza majukumu yake kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake.
Mheshiwa rais ulipoingia madarakani ulikuja na sera ya kubana matumizi.
Sasa kwa hili la kurudia uchaguzi kisa mtu kajiuzulu ni sawa kweli au ni kuendelea kuliingiza taifa hasara?
 
Mimi nawaonea huruma watanzania maisha yao magumu lkn kila miezi 3 wanafanya chaguz za watu wanaohama, kwanini hizo hela za uchaguzi msiwasaidie wananchi wenu? Watz nawaonea huruma kwa kweli
 
Tunatumia hela ya kusambaza maji vijijini visivyo sahihi.

Naomba dhambi hii iwafike wahandisi wa hili kwa njia yoyoooote Mungu inayoona inawafaa!!
 
Mimi nawaonea huruma watanzania maisha yao magumu lkn kila miezi 3 wanafanya chaguz za watu wanaohama, kwanini hizo hela za uchaguzi msiwasaidie wananchi wenu? Watz nawaonea huruma kwa kweli
Hizi pesa za uchaguzi katika kata na majimbo, zingeelekezwa miradi ya Mae deleo, yaani afya, elimu na maji nchi hii sehemu kubwa nchi zingekuja kujifunza maendeleo ya watu at grass root. Leo ni siasa tu all the days na uchumi wa watu na nchi at Large umesinyaa mpaka huruma!!!! Mimi hata sielewi!!! Mwelekeo Kama nchi ni positive au negative???? God bless us.
 
Kuna hali ya wananchi Wa eneo ambalo Mbunge anajiuzulu kisha anagombea tena kwa chama kingine.
Wananchi Wa eneo husika hawasikii uchungu kwa sababu gharama zinatoka katika fuko kuu LA taifa hivyo hawasikii maumivu.
Utaratibu ungekuwa chaguzi kama hizi fedha zichotwe kutoka katika fedha za miradi yao ya maendeleo kwenye eneo husika tuone kama huyo mgombea kama kuna MTU hata kumsalimia atamsalimia.
Mfano Ukonga, kama gharama ni billion moja kwa uchaguzi zinachotwa kwenye fedha za miradi ya barabara au Maji kwa Ukonga.
Hayo maumivu yangewafanya wananchi wamchukie huyo MTU daima.
 
Unaomba kura, unachaguliwa, unakuwa mbunge, unajiuzulu ubunge, unamuunga mkono Rais, unarudi tena kuutaka ubunge kupitia chama kingine, ubunge ambao ulijiuzulu. kuna sababu ya msingi ya kutokukufananisha na "WAHUJUMU UCHUMI?" Unapaswa kuwa mahabusu. I wish i could be president!
 
Hawa ndio hoja wanazojijenga. Anashindwa kuongelea Tume ya Uchaguzi ambayo viongozi wanachaguliwa na Rais na wapo pale kwa discretion ya Rais kitu ambacho kinapelekea kuwa na mgongano wa maslahi.
.
Mkuu Rufiji karibu mitaa hii.
Hoja ya wateule wa rais, haina mashiko kwa sababu hata majaji wote ni wateule wa rais na wanatoa haki kwa wote .

Kwenye tume, mimi nimeshauri iwe inclusive
P

Wanabodi,

Declaration of Interest.
Mimi ni miongoni mwa Watanzania wazalendo wa nchi yangu, ambaye sio mwanachama wa Chama chochote cha siasa, kwa sababu siasa za vyama za Tanzania, tunaziona katika baadhi ya maeneo kama ni ujinga fulani hivi, hivyo nawaomba sana univumilie, ninapoita siasa zetu ni siasa za ujinga ujinga fulani kwa baadhi ya vyama na baadhi ya wanasiasa, na nasisitiza, nimesema baadhi, nikimaanisha sii wote!.

Tubishane kwa Kutoa Hoja kwa Hoja, Kupangua Hoja kwa Hoja, na Sio Hoja Kwa Viroja!.
Hii ni opinion yangu tuu, and everybody has the right to his/her own opinion, hivyo tukitofautiana kwenye hili, tutofautiane kwa hoja, mimi nimeleta hoja zangu kuwa siasa zetu kwenye baadhi ya maeneo fulani fulani, likiwemo eneo la siasa za uchaguzi, kiukweli ni ujinga fulani, na zinavyoendeshwa, kuna maeneo zinaendeshwa kwa ujinga ujinga. Hivyo naomba usisome hoja zangu, ili tukitofautiana, tutofautiane kwa hoja, pangua hoja zangu na ama kutetea ama kuleta hoja mbadala, nikiwasisitiza na kuwaomba tubishane kwa hoja na kushindanisha hoja kwa hoja, kupangua hoja kwa hoja mbadala na sio watu tumeleta hoja humu, halafu mtu anakuja kuibishia kwa viroja!.

Ili Tuendelee, Watanzania Lazima Tufanye Siasa za Ukweli, Tuachane na Siasa za Ujinga Ujinga!.
Nashauri kama ni kweli Tanzania tunataka maendeleo ya kweli ya taifa letu, ni lazima tufike mahali tufanye siasa za ukweli, the real politics na sio hizi siasa za blah blah tunazoendelea nazo. Tufike mahali, sisi Watanzania, wazalendo wa kweli wa nchi hii, wenye nia njema na ya dhati ya maendeleo ya kweli ya taifa hili letu masikini, hatuwezi kukaa kimya na kunyamaza kwa kuendelea kukumbatia sheria mbovu za uchaguzi ambazo Makama Kuu ya Tanzania imeziita kuwa ni "bad laws" na kushauri, zifutwe, "scraped" kutoka katika vitabu vya sheria!, lakini kwa vile sheria hizo mbovu, zinakinufaisha chama fulani, then tunaendelea kuzing'ang'ania sheria hizo mbovu za uchaguzi, hata kama matumizi ya sheria hizo mbovu, ni kuwawabesha masikini wa Tanzania, mzigo mkubwa wa gharama za uchaguzi wa marudio, kwa sababu za kijinga jinga tuu kabisa, zinazotokana na siasa za ujinga ujinga!. Kitendo hiki cha masikini wa kutupwa wa Tanzania, wanaoishi kwenye lindi la umasikini uliotopea wa kipato cha chini ya dola moja kwa siku, halafu kuja kubebeshwa mzigo wa gharama za kugharimia uchaguzi za marudio, kutokana na diwani mmoja au mbunge mmoja kuhama chama hiki na kuhamia chama kile kwa sababu za kisiasa tuu, hizi ndizo siasa mimi ninazo ziita ni "siasa za ujinga ujinga!", na sababu zenyewe zinazowafanya wabunge na madiwani hao kuhama chama kimoja kwenda chama kingine, naziita kuwa ni sababu za kijinga jinga na nyingine ni za kijinga kabisa!. Kwa maoni yangu, this, its not only ni nonsense, but also ni dhambi kwa Mungu, kuwabebesha, Watanzania masikini hawa wa kutupwa, gharama hizi za ziada za uchaguzi wa marudio, kutokana na wawakilishi wao kuhama vyama kwa sababu tuu za hizi siasa zetu za ujinga ujinga, mimi nauita huu pia ni ujinga fulani in the name of politics!.

Kwa Nini Sheria Yetu ya Uchaguzi ni Sheria Mbovu, Bad Law.
Kifungu 21 cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kinatoa haki ya kila Mtanzania mwenye sifa, kuwa huru kushiriki katika siasa kuanzia serikali za mtaa hadi serikali kuu, bila ubaguzi wowote.

Uhuru wa kushiriki shughuli za umma Sheria ya 1984 Na.15 ib.6 Sheria ya 1994 Na.34 ya ib.4
21.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 5, ya 39 na ya 67 ya Katiba hii na ya sheria za nchi kuhusiana na masharti ya kuchagua na kuchaguliwa, au kuteua na kuteuliwa kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao, kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria.

Lakini kukatokea kikundi fulani cha watu, naomba kuwaita ni "wajinga fulani", wakaipindua katiba kwa sababu fulani za kijinga kabisa!, wakainyofoa haki hiyo ya raia kushiriki uongozi kwa uhuru kabisa, na badala yake, kulazimisha ili mtu ushiriki uongozi fulani, au ugombee nafasi fulani fulani ya uongozi wa umma, ni lazima kwanza udhaminiwe na chama cha siasa!, kiukweli kabisa na ki haki, huu ni ujinga!, this is nonsense!. Katiba yetu haikusema hivyo!.

Rev. Mtikila (Mungu amuweke pema peponi) alikipinga kifungu hiki na Mahakama Kuu ya Tanzania, ikatamka bayana kuwa kipengele hicho ni batili na kinakiuka katiba ya JMT hivyo kifutwe kwenye sheria, kila Mtanzania awe huru kugombea nafasi yoyote ya uongozi wa umma, au kwa kupitia vyama vya siasa, au bila kupitia chama chochote. Lakini wajinga wale, wakaamua kuihalalisha batili ile, kwa kukipenyeza kipengele hicho batili ndani ya katiba yetu, ili kuuhalalisha ujinga wao!, hivyo shurti la kudhaminiwa na chama sasa ni la kikatiba!.

Jee Lengo la Kudhaminiwa na Chama ni Nini?, Huu Sii Ujinga Tuu?!.
Katiba ilisema kila Mtanzania yuko huru na ana haki ya kushiriki uongozi, toka serikali za mtaa hadi serikali kuu bila kuwa na chama chochote. Hili sherti la kumlazimisha kudhaminiwa na chama lilitoka wapi?!, na kwa kwa nini watu walazimishwe kuwa wanachama wa vyama ili wadhaminiwe, ndipo waweze kugombea?!. Mfano mimi, sina chama kwa sababu naziona siasa za vyama kama ni ujinga fulani hivi, ikitokea nina uwezo wa kuwatumikia wananchi wa eneo langu na kuwaletea maendeleo bila kupitia chama chochote, kwa nini nizuiliwe?!. Kiukweli kabisa, huu ni ujinga, it is nonsense!. Watanzania tusikubali ujinga huu uendelee hadi 2020!, tupiganie milango ya wagombea huru na wagombea binafsi ifunguliwe, 2020, watu wenye uwezo wa uongozi, na wenye nia ya kugombea, ili kuwaletea wananchi maendeleo, bila kupitia hizi nonsense za siasa vyama waingie, and you never know hata sisi tusio na vyama kama mimi, tuingie, tushindane kwa hoja na sio kushindana kuhonga, kama hali inavyoendelea sasa!.

Kiongozi Akiishachaguliwa, Anakuwa ni Kiongozi wa Watu, na Sio Kiongozi wa Chama, Kwa Sababu Anachaguliwa na Watu na Sio Chama!.
Ujinga mwingine mkubwa kabisa wa siasa zetu za vyama, ni ujinga ni huu, hata kama mgombea amedhaminiwa na chama cha siasa kugombea, akiishapitishwa na Tume ya Uchaguzi kuwa Mgombea rasmi, japo anatambulika kama ni mgombea wa chama fulani, lakini anachaguliwa kwa kura za wananchi wa eneo lile wote wakiwemo wanachama wa chama chake, akiishachaguliwa, mwenyekiti wa mtaa, diwani, mbunge au rais, sasa anakuwa ni kiongozi wa umma na sio kiongozi wa chama kilichomdhamini, bali anakuwa ni kiongozi wa wananchi wa eneo lile waliomchagua, wasio mchagua hata wasiopiga kura, huyu sasa anakuwa ni kiongozi wa wote na sio kiongozi wa chama chake hata kama alidhaminiwa na chama fulani.. Mfano baada ya rais Magufuli kuchaguliwa kuwa rais kwa tiketi ya CCM, lakini hakuchaguliwa na wana CCM pekee, amechaguliwa na wananchi wote na Watanzania wote, na sasa sio kiongozi tuu wa CCM. kwa sababu ndie Mwenyekiti wao, bali rais Magufuli ni kiongozi wa Watanzania wote,wa vyama vyote, wa watu wote!. Hali ni vivyo hivyo kwa wabunge, madiwani na viongozi wa serikali ya mtaa, kitendo cha kiongozi wa umma, kujitoa chama kilichomdhamini na kupoteza uongozi wa umma, ubunge, udiwani au uongozi wa umma, ni ujinga ambao haupaswi kuvumiliwa na kuendelea kukumbatiwa!. This nonsense must stop!. Nini muhimu zaidi kati ya umma na chama?. Kuukosesha umma kiongozi waliemchagua kwa sababu za chama, sio tuu sio haki kwa wananchi waliomchagua, bali ni ujinga uliopitiliza!, halafu wananchi masikini wa Tanzania, kuja kulipisha gharama za kugharimia uchaguzi wa marudio, sio tuu ni ujinga mwingine, bali ni dhambi kuwagharimisha wananchi hawa gharama za kurudia uchaguzi kwa sababu fulani amejiuzulu chama hiki na kitu cha ajabu kabisa, huyo huyo fulani aliyejiuzulu, ndio anakuja kugombea tena kupitia chama kinhine!. This is nonsense!.

Nini Kifanyike, A Way Forward.
Kama nilivyowahi kushauri humu, ukosoaji wenye kujenga, huandamana na ushauri wa nini kifanyike kurekebisha kasoro hizi ili kuundoa ujinga huu unaoendelea nchini mwetu kwa sasa.
  1. Iwekwe faini maalum kwa kila kiongozi wa umma, atakayejiuzulu nafasi yake kwa sababu za kijinga jinga, ikiwemo kukatwa mafao yake na ikibidi kufilisiwa ili kugharimia gharama za uchaguzi wa marudio kwa kulitia hasara taifa.
  2. Viongozi wote wanaojiuzulu, wasiruhusiwe tena kugombea nafasi zile zile walizojiuzulu, kama sababu za kujiuzulu mimi nimeziita ni za kijinga, tusiwakubalie wajinga hawa kugombea tena, ili wasije kutuletea tena ujinga ule ule na kutugharimisha masikini sisi kugharimia uchaguzi wa marudio!.
  3. Tubadili sheria yetu ya uchaguzi, kwa kufuta chaguzi zote ndogo, na tuanzishe mpango wa succession plan mgombea wa chama fulani aliyeshinda, tujenge hoja kuwa huyo aliyeshinda ameshinda kwa sababu ya chama c alichogombea hivyo wananchi wamekipa chama ridhaa, hivyo akijiuzulu, akisita kuwa mbunge, diwani, rais kwa sababu zozote zile, chama chake kiteue mwanachama mwingine kushika nafasi ile!. Hili likifanyika, amini usiamini, hatutasikia tena kiongozi anajiuzulu kwa sababu za kijinga jinga!.
  4. Kama tunaamini aliyechaguliwa ni mtu na sio chama, then tuanzishe kitu kinachoitwa "a proportional representation" kwa mwenye kura nyingi ndiye mshindi, lakini likitokea lolote, akasita kuwa rais, mbunge au diwani, yule aliyemfuatia kwa wingi wa kura katika uchaguzi uliopita ndio anatangazwa mbunge, diwani, rais, na kama hayupo anachukuliwa mtu wa tatu, hadi wa mwisho, kama wote hawapo, ndipo uchaguzi mdogo unafanyika.
  5. Kile kipengele cha kudhaminiwa na chama kiishie kwenye uteuzi tuu, kiongozi akiishachaguliwa, anakuwa kiongozi wa umma. kiongozi wa watu, anaweza kuhama chama bila kupoteza uongozi wake kama ilivyo nchini Kenya.
  6. Tubadili sheria yetu ya uchaguzi, kwa kuondoa kipengele cha kudhaminiwa na vyama ili kila Mtanzania mwenye sifa za kugombea uongozi wa nafasi yoyote, aruhusiwe, ila kwenye urais, tuweke vigezo vya ziada, ili asijetokea tajiri mmoja mwenye ukwasi wa kuwanunua Watanzania wote, tukajikuta tuna rais wa kununuliwa. Ila kwenye ubunge, udiwani na serikali za mtaa, kila mtu awe free kugombea, hivyo tuwe na wagombea huru, na hili likifanyika hata sisi tusio na vyama tutashiriki, mfano mimi, naweza kabisa kugombea jimbo fulani na kulitwaa kama kuokota embe dodo lililojiangukia, ambapo mbunge wa hapo, nitamsukuma kama nimesukuma mlevi!.
Hitimisho.
Tanzania is too poor spend billions on by elections for foolish and nonsense reasons!, nikimaanisha nchi yetu Tanzania ni masikini wa kutupwa, kuhalalisha matumizi ya mabilioni ya fedha kuendesha chaguzi ndogo marudio kwa sababu za kijinga ni ujinga!. Ili Taifa letu lipate maendeleo ya kweli, ni lazima sisi Watanzania tukubali kuwa wakweli toka ndani ya nafsi zetu, tusikubali ujinga huu wa kuhama vyama, uendelee kutugharimisha sisi masikini wa kutupwa, tunaoishi kwenye lindi la umasikini uliotopea, halafu kuendelea kugharimishwa na wajinga fulani kurudia uchaguzi kwa sababu tuu za kisiasa zilizosababishwa na ujinga fulani, yaani ujinga wao. usituumize sisi masikini wa Mungu ambao we have nothing!.

Nawatakia Furahi Dei Njema.

Paskali
Rejea.
Rev. Mtikila ashida kesi ya kuruhusu mgombea binafsi mahakama ya ...
Mtikila: Shujaa wa Demokrasia, Mwanamapinduzi halisi na Shujaa ...
Mgombea binafsi Tanzania: Tatizo ni nini? | Page 9 | JamiiForums ...
Swali kwa Wana UKAWA: Is UKAWA for Real or Just A Marriage of ...
 
Kwa nini wasibezwe wakati wanalisababishia taifa hasara ya mamilioni? Nenda kawaambie watu wa Ukerewe ambao wamepoteza ndugu zao simply kwa kuwa waokoaji walikosa taa za kuokolea usiku kwamba hawa watu wasibezwe. Watoto wengi hawana madawati, wakinama wanajifungulia kwenye sakafu halafu huyu mla rushwa anataka turudi uchaguzi...
Mkuu Rufiji,kinachosababisha hasara ya kurudia uchaguzi nimekizungumza hapa, uchaguzi sio wahamaji bali ni sheria mbovu ya uchaguzi. Mbunge huchaguliwa na watu, aliopaswa kuwa huru kuhama na ubunge wake kama Kenya.
Rushwa ya ahadi kwenye sheria zetu sio kosa.
P
 
Kutokuwa na sheria kama Kenya hakuhalalishi hawa watu kufanya huu ujinga. Tanzania ni nchi maskini tuna matatizo mengi ya msingi yanayohitaji kila senti tunayoyapata. Haingii akilini kutumia mamilioni ya shilingi kufanya uchaguzi wakati watoto wetu wanasoma kwenye mazingira magumu.
Mimi huu nimeita ujinga na
ndicho nilichokisema katika bandiko hili

P.
 
Hili ndio swali ambalo kila mtu mwenye akili timamu anapaswa kujiuliza maana teyari ameshatuthibitishia kuwa hana huruma wala uchungu na kodi zetu.

Sasa tujiulize kama anafanya haya wazi wazi, nyuma ya pazi atakuwa anatupiga kiasi gani ukizingatia hajali na wala hana uchungu?

Wabongo mkija kushituka, jamaa teyari bilionea.
 
Word!
Hili ndio swali ambalo kila mtu mwenye akili timamu anapaswa kujiuliza maana teyari ameshatuthibitishia kuwa hana huruma wala uchungu na kodi zetu.

Sasa tujiulize kama anafanya haya wazi wazi, nyuma ya pazi atakuwa anatupiga kiasi gani ukizingatia hajali na wala hana uchungu?

Wabongo mkija kushituka, jamaa teyari bilionea.
 
Hili ndio swali ambalo kila mtu mwenye akili timamu anapaswa kujiuliza maana teyari ameshatuthibitishia kuwa hana huruma wala uchungu na kodi zetu.

Sasa tujiulize kama anafanya haya wazi wazi, nyuma ya pazi atakuwa anatupiga kiasi gani ukizingatia hajali na wala hana uchungu?

Wabongo mkija kushituka, jamaa teyari bilionea.
Hahahaaaa.... Kamanda Ryoba kakupagawisha!
 
Back
Top Bottom