Sheria ya ndoa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheria ya ndoa

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Emap Dodeyu, Jan 14, 2012.

 1. E

  Emap Dodeyu New Member

  #1
  Jan 14, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hello jamiiforums, I'm happy to come accross this site, hope it will be the answer of my need. Sheria ya ndoa inahitaji marekebisho kwa Tanzania kwani haiweki wazi kuwa wanandoa wa aina gani wana haki ya umiliki wa mali, haiweki wazi kuwa mwanandoa halali ni yupi yaani wa hali gani; hii ikiwa na maana mfano wanawake, anaweza kuolewa na mwanaume huyu akaachika, akaolewa tena na mume mwingine hata mara mbili tatu au zaidi. Mwisho wa siku kila alikoolewa alizaa watoto, kwa mume aliko sasa amezaa tena na alienda na watoto kadhaa wa alikoachika. Alikoolewa, kaolewa mke wa pili ikimaanisha kaingilia nyumba ya mke mwingine nasema hivi kwa maana kwamba ameolewa mke wa pili kwenye ndoa ya kikristo, na yeye mwenyewe ni mkristo na anaelewa fika kuwa dini ya kikristo hairuhusu ndoa za wake wengi. Kwa maana hiyo hawatafunga ndoa ila watakuwa na ndoa ya dhana ya ndoa kwa kuwa wataishi pamoja kwa zaidi ya miaka miwili au zaidi. Hatimaye aliyekuja kuingilia ndoa ya mwingine anamrubuni mumewe na mke mkubwa ananyimwa haki ya umiliki wa mali za urithi walizopewa na wakwe walipooana na zile walizochuma pamoja. Alipoolewa mke mdogo alikuta huyu mume ameshazaa watoto 12 na mke mkubwa, sasa watoto wa mke mkubwa waliokuwa wadogo kipindi hicho wanapodai urithi wao hasa eneo la kujenga au shamba mke mdogo anapinga na kusema yale mashamba ni yake, wakati aliyakuta na hajazalisha chochote kipya cha kusema hiki ni kile alichozalisha akiwa na mzee wake. Hii ni haki? Hivi sasa kesi iko mahakamani, na sioni kama haki inatendeka. Nisaidieni jamani.
   
Loading...