Sheria ya Ndoa ya 1971 itaweza kurekebishwa?

cutelove

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
3,317
7,509
Kuna mkanganyiko kisheria katika mapambano dhidi ya ndoa za utotoni na ndoa kwa wanafunzi;

1. Sheria ya Ndoa ya 1971 inaruhusu binti wa miaka 14 na 15 kuolewa kwa ruhusa ya wazazi na mahakama. (Tayari Mahakama imeitangaza sheria hiyo kuwa ni batili na kinyume cha Katiba baada ya kesi iliyofunguliwa na mwanaharakati Rebeca Gyumi).

2. Sheria ya Mtoto ya 2009 inasema mtu mwenye umri chini ya miaka 18, ndiye anayehesabika kuwa ni mtoto na anastahili kupewa haki mbalimbali za uangalizi na wazazi na jamii kama mtoto.

3. Sheria ya Kanuni ya Adhabu, inakataza kufanya mapenzi na binti chini ya miaka 18, na kwamba binti huyo hana ridhaa ya kuridhia au kukataa tendo hilo, hivyo yoyote atakayefanya naye atahesabika amebaka.

4. Sheria ya Elimu ya 2019 inakataza kumuoa mwanafunzi wa shule ya msingi na wa shule ya sekondari (kidato cha kwanza mpaka kidato cha 6) bila kujali umri wake umezidi miaka 18 au lah.

Ili kukwepa sheria hii mwanafunzi anayetaka kuolewa hutumia mbinu ya utoro wa zaidi ya siku 90 mfululizo ili afukuzwe shule kwa utoro. Au kama yupo katika darasa la mitihani hujifelisha shule kwa makusudi ili apoteze hadhi ya uanafunzi.

==Mwaka 2016 Mahakama Kuu ilitoa hukumu kubatilisha sheria ya Ndoa inayoruhusu miaka 14 na 15 kuolewa. Serikali haikukubaliana na hukumu hiyo na ikakataa rufaa katika Mahakama ya Rufani.

==Mwaka 2019 Mahakama ya Rufani iliitupilia mbali rufaa ya serikali na kubariki uamuzi wa Mahakama Kuu uliobatilisha sheria hiyo na kuamuru serikali ifanyie marekebisho sheria hiyo.

Miaka minne imepita, Serikali bado haijakamilisha mchakato wa kubadili sheria hiyo huku ikikumbana na maoni kinzani kutoka kwa makundi ya watu wanaoegemea misingi ya;

i) Kiimani, kwamba binti aliyebalehe, na si mwanafunzi wa shule, na yeye na wazazi wake tena mbele ya mahakama wameonesha kuwa wameridhia ndoa, basi si sawa kumzuia.

ii) Kiutamaduni kwamba zipo jamii zinazoamini kuliko binti aliyebalehe na si mwanafunzi aanze kufanya mapenzi kinyemela, na apate ujauzito au magonjwa ya zinaa na iwe fedheha kwa familia ni bora kumruhusu aolewe (Iwapo yeye mwenyewe ataonesha kuwa anataka).

Kuna fukuto na mvutano mkali kimawazo.

#KalamuYaCharles
 
Back
Top Bottom