DR Mambo Jambo
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 9,006
- 18,627
Mkuu Mawazo yako yaheshimiwe..Pamoja na kwamba ni mara chache wamasai wamekuwa wakizitumia vibaya hizo silaha, lakini bado ukweli ni kwamba wanatembea na silaha.
Unapotembea na silaha huku wengine wakiwa hawana silaha, unawaweka wale wasio na silaha kwenye mazingira hatarishi endapo patatokea hali ya sintofahamu miongoni mwenu, hali ambazo mara nyingi huja pasipo tarajiwa.
Huku bara tumekuwa tukiishi nao kwa mazoea tu, waendelee kutembea na silaha zao, lakini hiyo haina maana kwamba miongoni mwao hawawezi kuja kuleta madhara kwa members wengine wa jamii, hii haina maana kwamba miongoni mwao hawataweza kumdhuru yeyote mbele ya safari, tusisubiri majanga ndio tuamke.
Sioni ubaya wamasai kubaki na hizo alama nyingine za kuwatambulisha ukiondoa sime, rungu, na fimbo, na wala siamini ili huo utambulisho wao ukamilike basi ni lazima sime, rungu, na fimbo, viwepo, kwangu naona ni mazoea tu, suala la kulinda mila na desturi lazima liende sambamba na kulinda usalama wa wengine, hili tukubaliane.
- Huwezi kusema unalinda mila na desturi zako kwa kuweka usalama wa wengine rehani, hizo mila na desturi zako haziwezi kuwa juu ya usalama wa raia wengine, masai sio malaika, wanaweza ghafilika popote, dakika yoyote, tuanze kulia bila sababu.
Mwisho naona tukubaliane pia kwamba, wazanzibari nao wana nchi yao, wana maamuzi yao, na kwasababu miaka yote tumeamua kuwepo kwenye muungano usioeleweka, basi haya ndio matokeo yake, tuyavumilie hata kama wengine hamuyaelewi.
Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Kama silaha haitumiki kutimiza mabaya kwanini itufikirishe?
Tukumbuke kuwa hata wacheza karatee na Masumbwi pia na wenyewe wanayembea na silaha zao ambazo ni viungo vyao na wenyewe tuwakate viungo vyao ili wasio tishio kwa wengine?
Tumezaliwa tumekuta Tamaduni hizo ni kama Tunu kwa Taifa..
Ni tamaduni pekee iliyibaki Africa wazungu na wageni kutoka mbali huja kuiona tamaduni hiyo kujifunza imewezaje kubaki licha ya kuwa na Mabadiliko ya Kitechnolojia..
Halafu kuna waj***a fulani wanataka kuifuta Tamaduni hiyo na wewe unawachekea na kuwasifu?
Ni mpu**** tu anaweza kushabikia huu utoto