Sheria ya ajira kwa wazalendo inasemaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheria ya ajira kwa wazalendo inasemaje?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by CodeMaster, Sep 15, 2008.

 1. CodeMaster

  CodeMaster Member

  #1
  Sep 15, 2008
  Joined: Sep 15, 2008
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbona hawa wakenya sasa hivi wapo kila mahali,sasa hivi hata mfagiaji ni mkenya. Imekwenda wapi sheria ya ajira kwa wazawa,na sisi mbona tukienda kwao hatupati nafasi hii. Kibaya zaidi akiingia mkenya mmoja basi baada ya mezi sita watakuwa watatu. Historia ya elimu zao n i utata mtupu wengi wana degree za education na wengine diploma. Vipi hakuna watanzania wenye sifa hizi. AU TULIANZISHE LA SOUTH AFRICA,KUDAI HAKI ZETU ZA KUZALIWA NDANI YA NCHI HII NA HAKI YETU YA NAFASI ZETU ZA KAZI?????
   
 2. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #2
  Sep 15, 2008
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kwa kuwa waliojuu hawalitambui ilo cha msingi ni kulianzisha zali kama la SA imagine kuna makampuni mtx wanafika mpaka sita.
  Ivi izi work permit wanazitoa wapi,ili hali juzi tuu mfanyakazi mwenzetu kapewa shavu kwenda nje permit imesumbua kisa expert walizidi watatu?
  Tz we need to be serious once more,hatuwezi ruhusu mpaka wafagiaji watoke nje mbaya zaidi nenda kwao tena na hata degree uone mziki wake.
  Ivi kila kitu hatuo serious tutakuwa serious on what sasa??????????!!!!!!!!!!!!!!!!
  Mungu irehemu Tz na watu wake na uwapatie mwanga viongozi wetu waweze kufanya mabo kwa maslai ya nchi na uwapatilize wale wote wanaoleta ubinafsi kwenye nationa interests.
   
 3. m

  mgirima Member

  #3
  Sep 15, 2008
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sio Wakenya tu, Wanyasa + Wakongo + Warundi wapo kibao. Mpaka kwenye ofisi za serikali.
   
 4. Lasthope

  Lasthope Senior Member

  #4
  Sep 15, 2008
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 149
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Jamani hii ishu ni serious sana, tena nakushukuru sana we uliye anzisha mada hii, yaani napofanya kazi mimi robo tatu ya wafanyakazi wote ni wakenya.wabongo ni macleaners na housekeepers kasoro wachache wetu ambao hatufiki hata kumi. yaani hadi ofisi assistant wanawatoa kenya, working permit za kumwaga wanapewa tu, i dont know whats wrong with us. nangoja tu mtu atakayekuwa serious na ufatiliaji wa hii ishu ani pm nimpe ishu lote.
   
 5. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #5
  Sep 15, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Kuna watu wanasema tusione tabu, kwani hawa wageni hupewa tu zile kazi rahisi rahisi kama za marketing na administration. Sio shughuli kama engineering.

  Ila mimi naona bado kuna tatizo la msingi hapa, mojawapo ikiwa ni ukiukwaji wa taratibu zetu. Nchi inapoongozwa na raisi kama Kikwete, wananchi inabidi tuchukue hatua sisi wenyewe maana hatuwezi kuendelea kuwa shamba la bibi kwa kila kitu. Vinginevyo tutaja korofishana na majirani zetu bure! Mbaya zaidi tunawavunja moyo viongozi wanajali.
  Si mlimsikia Magufuli akieleza kuhusu kiwango cha samaki kinachovunwa kienyeji na wageni ndani ya mipaka ya bahari yetu?  .
   
 6. Tonga

  Tonga Senior Member

  #6
  Sep 15, 2008
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 175
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Na ukiangalia sana hawa wa Kenya hakuna wanachotuzidi chochote wengine watasema labda hiyo English yao yenye accent isiyo na ladha,kwanza kwa kuforge vyeti ndio wenyewe hao ni wanigeria wa East Africa, nimesoma nao but I don't apprecciate them, period.
  Wanajua kupenya kila palipo na mwanya na huwa wanasema wanapenda kufanya kazi Tz coz tunawaabudu na kuwalipa vizuri, sheria za ajira zibadilike na pia Tz tuamke kulinda maslahi yetu madogo angalau yanufaishe wananchi; ina maana kweli hatuna wasomi kiasi hiki? lets be serious with this issue tunapoenda sio pazuri.
   
 7. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #7
  Sep 15, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135

  THE IMMIGRATION ACT, 1995, Part IV, Sect. 17, Subsect. 1, and 3 (c)


  There is hereby established a Board to be known as the Alien Immigrant Board.

  The functions of the Board shall be:

  to advise the Director and other relevant authorities on whether or not the business or imployment vacancy in which an alien immigrant proposes to be engaged cannot be gainfully filled in by citizens of Tanzania.


  THE TREATY FOR THE ESTABLISHMENT OF THE EAST AFRICAN COMMUNITY, 2000
  ARTICLE 77, Sect. 4 and ARTICLE 78, Sect. 1

  Measures to Address Imbalances Arising from the Application of the Provisions for the Establishment of a Common Market

  For purposes of this Article, the Partner States shall within the framework of the Protocols provided for under Articles 75 and 76 of this Treaty, take measures to address imbalances that may arise from the application of the provisions of this Treaty. (ARTICLE 75, 76: Establishment of a Customs Union, and of a Common Market).

  ARTICLE 78, Sect. 1
  Safeguard Clause


  In the event of serious injury occurring to the economy or a Partner State following the application of the provisions of this Chapter, the Partner State concerned shall, after informing the Council through the Secretary General and the other Partner States, take necessary safeguard measures.
   
 8. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #8
  Sep 15, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kama hamna sheria, hamna ajira, na wala hamna wazalendo, kutakuwa na maana kuwa na "Sheria ya ajira kwa wazalendo"?
   
 9. W

  WembeMkali JF-Expert Member

  #9
  Sep 15, 2008
  Joined: Jun 16, 2007
  Messages: 282
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nadhani kabla ya kuulaumu uongozi uliopo tuanze kujilaumu sisi wenyewe wapiga kura.Wengi wetu tumekuwa tukiwapa free ride hawa jamaa kwa kuwachagua na kuwaweka madarakani bila ya kujali matendo au maamuzi yao.

  Ni wazi kabisa JK na serikali yake hawajali haya.Hawako serious kwenye rushwa,hawako serious kwenye utawala wa sheria,hawako serious kwenye maswala ya ajira,elimu,afya,kilimo na mambo mengine mengi tu.

  Halafu cha kushangaza utasikia kuna mimtu bado inaandamana eti kusifia hotuba zake.Na sitashangaa bado kuna watu ambao ni masikini wa kutupwa wataendelea kuchagua viongozi wabovu! sasa hapa sijui tatizo ni education au macho ya kuona kuwa hali ni mbaya.

  Wembe.
   
 10. Sam GM

  Sam GM JF-Expert Member

  #10
  Sep 16, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 536
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nakubaliana na Wembemkali, tatizo kubwa liko katika uongozi, viongozi wetu hawana mipango ambayo inaendana na wakati, utahsangaa kwa sasa hivi wanapanga mambo ya uchaguzi na jinsi watakavyorudi madarakani cha ajabu ukitakak kujua wana strategy gani ya miaja mitano katika wizara au sehemu wanafanya kazi inakuwa ni porojo tu!
   
 11. deny_all

  deny_all JF-Expert Member

  #11
  Sep 16, 2008
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 428
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Wewe kama muhusika ndani ya ofisi nenda katoe taarifa uhamiaji, kuwa unahisi kuna mchezo mbaya unachezwa ndani ya ofisi yenu, uone kama hatua zitachukuliwa au vipi? Inabidi Wa-tz tubadilike na kuwa na courage ya kufanya mambo sio kubaki kulalamika tu.
   
 12. Tonga

  Tonga Senior Member

  #12
  Sep 16, 2008
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 175
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hivi hujui kwamba UJINGA ni mzigo mkubwa sana na ndicho kinachotusibu watz tulio wengi, tunatakiwa tufanye kazi ya ziada kuwaelimisha hawa wapiga kura ambao they are always taken for a ride after every 5 yrs, what a shame na wananunuliwa kwa bei rahisi sana ahadi za uongo, pombe, doti ya kanga na tisheti na kwa bei hiyo wanauza utu wao na kuwapa watu ulaji na kuishia kuwa maskini wa kutupwa......ni lini tutakuwa na uchungu na maisha haya ya ufukara na kufanya maamuzi yasiyo tuletea majuto ya milele......
  Kuna haja ya kuanza kuwafikia hawa wapiga kura na kuwaamsha usingizini kwa swali rahisi sana; ni kitu gani cha maendeleo serikali iliyoko madarakani imefanya so far?maendeleo ambayo yanakugusa wewe as an individual. HAKUNA ni blah blah tu, kama kawaida yetu waswahili.
   
 13. Lasthope

  Lasthope Senior Member

  #13
  Sep 16, 2008
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 149
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hao uhamiaji unakosema tukatoe taarifa ndo wanakopewa work permit hata office assistants sasa huoni kama ntakuwa napoeza muda wangu? Kama wanashindwa kusema no in justification kwamba tanzania hatujachoka kiasi cha kushindwa kuprovide office assistant, huoni nchi ina ugonjwa mkubwa sana?
   
 14. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #14
  Sep 16, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135


  Tusikate tamaa, tuangalie mbele badala ya nyuma. Kumlaumu mpiga kura ni moja kati ya mambo 10 tunayoweza kufanya.


  Kila mmoja huwalaumu wapiga kura - hii haitusaidii. Na mara nyingi mtu anapotaja neno "sisi" humaanisha "wao" walioichagua sisiemu. Kwa nini tusianze kujilaumu kwa kushindwa kushinikiza walioko madarakani kujiuzulu au kufukuzwa, hasa hata baada ya kushuhudia uozo uliokithiri? Tujaribu kufanya kilicho kigumu zaidi (badala ya kukwepa) ambacho mwananchi wa kawaida kule kijijini hana upeo wa kukifikiri. Tupeane mawazo katika mtizamo huo.  .
   
 15. ThinkPad

  ThinkPad JF-Expert Member

  #15
  Sep 16, 2008
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,851
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Viongozi kushindwa kuwajibika ndio tatizo kama kila idara ikiwajibika hakuna mgeni atafaidika hapa Bongo bali sisi ndio tutawafaidi wageni,yaani mgeni njoo wenyeji wapone,Duh! yaani mgeni anapeta hapa bongo mpaka mimi namuonea "donge" jamani wakati hapa ndio home.

  kama sisi tukishindwa kutetea haki yetu basi Mungu ndio atakae tutetea.
  Viongozi hawafanyi kazizao wamegeuza maana nzima ya Uongozi yaani ukishakuwa kiongozi wewe ni kula tuu pesa hautoi huduma yoyote wakati sisi tunawapa uongozi ili watupe huduma.

  Hakika mtu mwenye highest IQ anafaa kuwa kiongozi sio kufika tu! chuoni hiyo haitoshi angalia aliyofanya Nyerere maana alikuwa ana upeo mkubwa wa akili jamani sio kila mtu anafaa kupewa madaraka jamani ndio maana wakenya wanapeta tu hakuna anae wauliza , yaani Viongozi wa uhamiaji mapolisi sijui wanafanya nini?,

  Angalia tena waliofanya wazee wakijapani walio jenga Japan walikuwa wanapenda japan ndio maana wakaijenga kwa nguvu zote matunda yao mpaka sasa raia wa Japan wanaheshimu Nchi yao Sio hapa kwetu kila mtu anataka apakimbie hadi viongozi wenyewe. hiyo ni picha halisi dunia inabadilika sana.

  Ukweli utabaki palepale Mungu awezi kukuangalia wewe unatumia pesa ya walipa kodi ambao ni fukara kwa kujinufaisha wewe mwenyewe na familia yako,

  Kumbuka hiyo pesa ingeingia kwenye Shule za msingi watoto mapacha ambao wametangazwa leo redioni kuwa wameangukiwa na kifusi labda hiyo pesa ingesaidia shule na wasinge kufa Damu ya watoto hao waliokufa na iwe juu ya mafisadi wezi na juu ya watoto wa mafisadi na familia zao.
  Watanyanyasa na kuwaibia watanzania lakini wakumbuke Tanzania ipo Duniani na Dunia ni ya Mungu na kila kilichopo duniani ni cha Mungu.

  Mungu wakumbushe viongozi wetu nini maana ya kiapo.Amina
   
Loading...