Sheria mpya ya mifuko ya hifadhi ya jamii,Wafanyakazi wa umma na wasio wa umma kufa masikini

kama kweli kuna huo mswaada na ukipelekwa bungeni naamini utapita tu kwa vyovyote vile, maana mambo mengi bungeni huamliwa kwa kura ya ndiyo, na miswaada kandamizi na ya kipuuzi kama hii wabunge wa CCM huwa wamepewa somo na kujipanga kuipitisha kwa manufaa ya serikali yao na wao wenyewe bila kuangalia wananchi wataathirika vipi na huo muswaada. Pia sie wafanyakazi wa Tanzania wa serikali au private sectors hatuna ushirikiano wa kuweza kupinga huu mswaada kama utapitishwa, tutabaki kulalamika tu huku pembeni bila kuchukua hatua sahihi kuonyesha kutuokubiana na hii dhuluma.
 
Hii inalenga kupunguza mahitaji ya ulipaji mafao ambayo inaonekana yamekuwa tabu kwa mifuko kutokana na fedha wachangazo wafanyakazi kwa lazima, kukopwa na serikali ama kuwekwa katika miradi isiyo na tija kwa wana mafao.

Michango yote inayokusanya, na investments ambazo mifuko hiyo inafanya, haikkupaswa kuwa na shida yae fedha za kulipa mafao na isitoshe Interest wanayolipa kwenye michango ya wafanyakazi ni aibu!!!!!

Hii inayotafutwa hapa ni njia ya kuzidi kuwaua wafanyakazi ambao pia wanalipa kodi kubwa kuliko mtu yeyote Tanzania.
 
Serikali imekopa kwenye mifuko ya kijamii had I imebaki haina kitu tena.

Huko bungeni yuko Zitto Kabwe; @ tindu lissu na John Mnyika naamini watapinga hilo.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: prs
Nilidhani wanapeleka Mswada wa kutaka mifuko ya jamii itoe mikopo (bila kupitia saccos ambako kuna urasimu na riba kubwa) kwa wanachama wake, mikopo ya investments ya muda mrefu ili iwape maandalizi mazuri kabla ya kustaafu.

Dhamana iwe ile michango plus something ili iwe imedhaminiwa kwa 100%.

Kwamba waajiri wao wa guarantee repayments kwenye mishahara ili wanapowakilisha michango ya kila mwezi wawakilishe na marejesho ya mikopo.

Hakuna mfanyakazi atatoroka aache kazi na mafao yake ya hifadhi.

Na pia waruhusu hifadhi hizi ziwadhamini wanachama wake mikopo mikubwa ya mabenki kwa kutumia akiba zao ambazo kwa ongezeko la kila mwezi, risk inapungua na ukijumlisha na marejesho, hakuna risk kubwa kwa hifadhi hizi.

Ajabu, hawafikirii constructively, wanachokiwaza ni namna gani mfanya kazi azidi kuumia akiwa kaizini na akistaafu afe mapema kwa frustration.

Wafanya kazi kataeni muswada huu wa kifisadi na kiuaji. Badala yake, andaeni muswada wenu juu ya haya ninayowwaambia ili watu mnufaike.
 
Hatuna historia ya kupinga mambo ya kidhalimu.
Wataanzisha propaganda za kivyama na wataipitisha kwa wingi wao na sisi tutabaki kulalamika tu kwenye mitandao. Tz nchi nyepesi sana kuongoza,wananchi wake hawako serious na mambo ya muhimu. Kama waliweza kupitisha ile rasmu na tukakaa kimya unatarajia nini?

Sio nnchi nyepesi bali ni nchi inayoongozwa kwa kutumia nguvu za Giza...kwahiyo wa Tz wanarogwa saana kila kukicha....hivi walivyo wa Tz ni kwasbabu ya kurogwaaaa...na ndio maana ni nnchi peke ambayo mchawi au mganga wa kienyeji anatoa matamko au uatabiri wakiserekali na kutishia wengine maisha na serikali ipo kimya......kumbuka ulinzi usioonekana!!!!!!...uliokuwa unatolewa na .....yule mzee aliyetangulia....
 
Hatuna historia ya kupinga mambo ya kidhalimu.
Wataanzisha propaganda za kivyama na wataipitisha kwa wingi wao na sisi tutabaki kulalamika tu kwenye mitandao. Tz nchi nyepesi sana kuongoza,wananchi wake hawako serious na mambo ya muhimu. Kama waliweza kupitisha ile rasmu na tukakaa kimya unatarajia nini?

Umenena vema, kuna tatizo kubwa sana kwa wananchi wenyewe, ndiyo maana Wata wala(yaani Watawakula au Watawala) na Wana wa siasa(Wanasiasa) wanajiamulia mambo ya udhalimu na kuyatekeleza watakavyo! And nobody cares! Lazima tujitafakari how we've come to this!? Tufanyeje? Utawala wa HAKI uko wapi? Kwa nini viongozi 'wengi' na utawala wao unawaza udhalimu tu?
 
Hivi Kwa nini inakuwa vigumu kuitoa hii serikali madarakani kupitia kura?

Vinginevyo mtapiga kelele tu na hakuna msaada.
 
Msinipopoe mawe...ila niwaulize swali..nani asiyejua kuwa watu wengi baada ya kustaafu maisha huwa magumu Sana na wengi hutegemea kutunzwa na watoto wao...mimi Ni mfanyakazi pia ila ninachofikiri mimi Ni kuwa tufight tulipwe 60-75 percent halafu hy nyingine ndio ilipwe kama formula yao inavyosema..
 
Msinipopoe mawe...ila niwaulize swali..nani asiyejua kuwa watu wengi baada ya kustaafu maisha huwa magumu Sana na wengi hutegemea kutunzwa na watoto wao...mimi Ni mfanyakazi pia ila ninachofikiri mimi Ni kuwa tufight tulipwe 60-75 percent halafu hy nyingine ndio ilipwe kama formula yao inavyosema..

Na bado mtakatwa kodi asilimia 30 ya gratuity. Yani hela za kwako mwenyewe, uhifadhi kwa miaka nenda rudi, siku ya kuzichukua wanakata 30%.Wafanyakazi wa TZ kweli MAJUHA.

Hivi mnakubali vipi kuendeshwa namna hii??TRA wanawa-double tax kila kona.

Samahani kwa lugha kali.
 
Walitupiga NBC tulifanya nini??
Walitupiga KIWIRA tulifanya nini??
Walitupiga EPA tulifanya nini??
Kakatupiga RADA tulifanya nini??
Wakatupiga ndege ya Rais tulifanya nini??
Wakatupiga RICHMOND tulifanya nini??
Wakachakachua KATIBA mpya tulifanya nini??
Wametupiga ESCROW tumefanya nini??

Hii ya Hifadhi ya jamii wakiamua watatupiga pia na hatutafanya lolote zaidi ya kubwabwaja na mwishoe tutaishia kumsifu raisi kwa kuwa kiongozi boooooooora.

Watz tunakasoro,, sisi siyo watu timamu. TUNA MTINDIO MAHALI.

Huko walipotupiga hakuna direct impact kwa mfanyakazi ila kwenye hiyo mifuko ina impact direct kwa mfanyakazi,waache wafanye yao kisha wataiona gondo.
 
Yaani Nifanye Kazi Kwa Miaka Let Say 35, Ktk Mil100 Unipe Mil 25 Kama Nimestaafu Na Mshahara Wa Laki8 Inamaana Unanipangia Niwepo Dunini Kwa Miaka 78 Tu?

Umekosea, Kama umechangia 100M, TRA wanakata 30M kama kodi, wanajua wenyewe ni kodi ya nini, then unabakiwa na 70, hiyo unachukua 25% ambayo ni 17.5M kwa kufuata utaratibu mpya.

Kazi mnayo, Huu ni utumwa mambo leo.
 
Nimecheki vikokotoa vyao hawa PPF ndio wauaji kuliko wote. DUH

Old Age Benefits
Period Contributed (MONTHS)500
Average Best Salary of Three Years (TZS)3,000,000.00
Monthly Pension (TZS)1,939,655.17
Pension Gratuity (TZS)96,982,758.62


Yani mtu amefanya kazi miaka zaidi ya 30, amemaliza na mshahara wa miaka 3 iliyopita average ya 3M, kiinua mgongo ni 96M?WTF?hivi mnakubali vipi kufanywa mazoba kiasi hiki?na hiki?

tena hiyo average ya 3M kwa serikalini ni kiwango cha mkurugenzi.

kwa maafisa wa chini na kada zenye bahati mbaya kama waalimu.wanachezea around 1M

Old Age Benefits
Period Contributed (MONTHS)500
Average Best Salary of Three Years (TZS)1,000,000.00
Monthly Pension (TZS)646,551.72
Pension Gratuity (TZS)32,327,586.21

30 years of service halafu unalipwa 32M??that's 1M every year you have toiled hard.Sasa kama sio utumwa huu ni nini?PPF mnapeleka wapi hela za hawa wazee?
 
Mleta hoja asante kwa taarifa.
Ila naona kama vile hii Hoja haiwezekani kabisaaaaaaa! kwamba utumikie miaka yote, halafu ukiwa ma miaka 55/60 ulipwe robo, na nusu ya mshahara halafu kwa maisha haya mtu anakufa baada ya muda mfupi hivyo uwe umeambulia robo tu ya mafao yako! HAIWEZEKANI!
HII LAZIMA ILETE VITA!
Haiwezekani kuleta hoja kama hii wakati huu wa uchguzi unakuja! kwa hasira kabisa kabisa mi naona haiwezekani hili jambo halipo!!
 
Sijajua kwanini watu tunazungumzia umri wa kustaafu ni miaka 60. Ninavyoelewa mimi huo umri ni maximum age. Kuna baadhi ya waajiri wana minimum time ya kufanya kazi kabla ya kustaafu, regardless your age. Pia kwa hii mifuko kuna minimum serving time ili u-qualify kulipwa pension ambayo ni miezi 180 (15 yrs). Bahati mbaya wafanyakazi wengi hatulijui, elimu itolewe kwanza
 
Nimecheki vikokotoa vyao hawa PPF ndio wauaji kuliko wote. DUH

Old Age Benefits
Period Contributed (MONTHS)500
Average Best Salary of Three Years (TZS)3,000,000.00
Monthly Pension (TZS)1,939,655.17
Pension Gratuity (TZS)96,982,758.62


Yani mtu amefanya kazi miaka zaidi ya 30, amemaliza na mshahara wa miaka 3 iliyopita average ya 3M, kiinua mgongo ni 96M?WTF?hivi mnakubali vipi kufanywa mazoba kiasi hiki?na hiki?

tena hiyo average ya 3M kwa serikalini ni kiwango cha mkurugenzi.

kwa maafisa wa chini na kada zenye bahati mbaya kama waalimu.wanachezea around 1M

Old Age Benefits
Period Contributed (MONTHS)500
Average Best Salary of Three Years (TZS)1,000,000.00
Monthly Pension (TZS)646,551.72
Pension Gratuity (TZS)32,327,586.21

30 years of service halafu unalipwa 32M??that's 1M every year you have toiled hard.Sasa kama sio utumwa huu ni nini?PPF mnapeleka wapi hela za hawa wazee?
Ni muhimu kujua umechangia kiasi gani katika hiyo miaka 30, au mnataka pesa itoke wapi? Kama mshahara wa mwisho ni 3M maana yake ulipoanza kuchangia ulikuwa ni mdogo zaidi.
 
Back
Top Bottom