instagramboy
JF-Expert Member
- Oct 16, 2014
- 1,521
- 343
Huwa wanafanya uhakiki kila baada ya miezi 6,kwenye uhakiki anatakiwa aende muhusika,asipotokea ndio itakula kwake.
Uhakiki ni kila baada ya mwaka kwa sasa
Huwa wanafanya uhakiki kila baada ya miezi 6,kwenye uhakiki anatakiwa aende muhusika,asipotokea ndio itakula kwake.
Mleta hoja naomba urudi kwa aliekutuma mwambie akupe taarifa sahihi lkn icho unachofanya ni kupotosha umma wa watanzania!!!
Kuhusu suala la kupeleka muswada wa sheria mpya ya mafao bungeni sio kweli kabisa nimekomfirm na vyanzo sahihi wamenithibitishia hilo, lakini kwa kukusaidia tu serikasli haikulupuki kupeleka miswaada bungeni , ili kufanya ivyo inawashirikisha wadau wote
Kuhusu kanuni mpya, hizi zilitolewa mwaka jana na kuanza kazi julai 1st. na zilitolewa na kuidhinishwa na wadau wote wa sekta ya Hifadhi ya Jamii, ambapo vikao vilifanyika, walialikwa kwenye vikao na kutoa maoni yao kabla ya kanuni hizi hazijatolewa.
na Fomula hiyo ipo ivi: 1/580 ya mafao kujumuisha na miezi ya mwanachama aliyochangia kujumuisha na annual penshanable emoluments zidisha na miezi 12.5 zidisha na asilimia 25. hivyo hiyo lugha ya 1/4 ya mafao ni upotoshaji wa makusudi kabisa
Mkuu una basic ya 2M kwa mwezi unajiita mlalahoi? tafadhali banaMkuu hebu nipigie mahesabu mimi mlalahoi mwenye basic ya milioni 2 nikistaafu leo nitapata kiasi gani?
Serikali ya Tanzania imekusudia kupeleka muswada bungeni utakaoleta utaratibu mpya wa jinsi ya kulipa mafao kwa wastaafu wote walio jiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii,kupitia sheria hiyo ambayo serikali inataka itumike kulipa mafao ya wastaafu itakuwa hivi.
Kila mstaafu wa umma au binafsi atapewa robo ya kile anachotakiwa kupewa baada ya kustaafu kazi, yaani kama anatakiwa apewe millioni 100 basi yeye atapewa million 25,halafu baada ya malipo hayo kufanyika ni kwamba mstaafu atakuwa anapewa kila mwezi nusu ya basic salary yake aliyokuwa anapata kabla ya yeye kustaafu,malipo hayo atakayo kuwa anapata mstaafu yatakoma pindi tu atakapo fariki.
Ikumbukwe kwamba kujiunga na mfuko wa hifadhi ya jamii ni lazima kwa mwajiriwa yoyote na umri wa kustaafu kwa mujibu wa sheria ni miaka 60.
Msimamo wa vyama vya wafanyakazi:
Vyama vya wafanyakazi vimepinga muswada unaotaka kupelekwa bungeni na serikari, mara zote tatu vyama vya wafanyakazi walipo kutana na wawakilishi wa serikali huko mbeya,dodoma na hata mara ya mwisho arusha walipokutana hasira zilijitokeza kupinga jambo hilo kwani ni unyonyaji uliokithili unaotakiwa kuletwa,kwa mujibu wa mnyetishaji wangu mkutano wa mwisho kati ya wawakilishi wa serikali na vyama vya wafanyakazi unatarajiwa kufanyika Dar kabla ya bunge kuanza mwishoni mwa mwezi huu,ili ikiwezekana muswada huo upelekwe kujadiliwa na wabunge wa wakilishi wa wananchi.
Inasemekana kwanba muswada huu wa sheria ulitakiwa kupelekwa bungeni tangu mwezi Novemba ktk bunge lililopita,ilishindikana kutoka na suala la escrow kuchukua muda mwingi zaidi.
Wachache wafanyakazi nilio sikia maoni yao wamesikitika na wanaona kama sheria hiyo ikipita basi waajiriwa wengi watakufa maskini kwani mtu wa miaka 60 kwa Tanzania anakuwa na muda mchache sana wa kuishi,ukizigatia wengi wao wanategemea pesa za kustaafu ili wajenge nyumba nzuri na kuanzisha vitega uchumi tofauti...!!
NB: Serikali imeikopa sana mifuko hii ya hifadhi ya jamii kiasi kwamba inashindwa kujiendesha vizuri,hivyo inatafuta namna ya kuiokoa na balaa la kufilisika.Chuo kikuu cha Dodoma ni fedha za mifuko hii hadi leo bado hazijarudi!
Mleta hoja naomba urudi kwa aliekutuma mwambie akupe taarifa sahihi lkn icho unachofanya ni kupotosha umma wa watanzania!!!
Kuhusu suala la kupeleka muswada wa sheria mpya ya mafao bungeni sio kweli kabisa nimekomfirm na vyanzo sahihi wamenithibitishia hilo, lakini kwa kukusaidia tu serikasli haikulupuki kupeleka miswaada bungeni , ili kufanya ivyo inawashirikisha wadau wote
Kuhusu kanuni mpya, hizi zilitolewa mwaka jana na kuanza kazi julai 1st. na zilitolewa na kuidhinishwa na wadau wote wa sekta ya Hifadhi ya Jamii, ambapo vikao vilifanyika, walialikwa kwenye vikao na kutoa maoni yao kabla ya kanuni hizi hazijatolewa.
na Fomula hiyo ipo ivi: 1/580 ya mafao kujumuisha na miezi ya mwanachama aliyochangia kujumuisha na annual penshanable emoluments zidisha na miezi 12.5 zidisha na asilimia 25. hivyo hiyo lugha ya 1/4 ya mafao ni upotoshaji wa makusudi kabisa
Sawa kama vyanzo vyako ndio vimekwambia hivyo,mbona hawaja kueleza ni jinsi gani pesa zilizochukuliwa kutoka katika mifuko hii ya hifadhi ya jamii zitarudishwa? Hadi leo pesa kibao zilitumika kujenga UDOM kutoka mifuko tofauti ya hifadhi ya jamii na sasa hivi pia daraja la kigamboni linajengwa na fedha hiz,ktk ukaguzi uliofanywa na CAG alionyesha ni jinsi gani itasumbua kurudisha fedha zilizojenga udom kutokana na kutokuwa na mkataba wenye kueleza namna fedha zitakavyorudi,naomba ukaulize na hilo pia..!!
Pia nakushauri jitahid kupitia ile sheria iliyopitishwa miaka miwili iliyopita ambapo ilikuwa inazuia mtu kuchukua mafao yake hadi pale atakapo timiza umri wa miaka 55,hii ilipitishwa kinyemela tena bila kelele za wabunge,na kusababisha wafanyakazi wa migodini wagome na kuandamana kwani wao hawawezi kufanyakazi hadi kufikia umri huo wa miaka55 wakiwa kazini, ndipo wakaona aibu na kuitoa hiyo sheria,kama utakaa na kutafakari hayo ndio utagundua ni jinsi gani pesa za mifuko ya hifadhi ya jamii zinatakiwa na serikari kwa mambo tofauti lakini sio kwa kutunufaisha sisi wafanyakazi wake....!! Ya kuambiwa changanya na yako...!! PSPF mfuko wa serikali mbona unakataa kumpa mfanyakazi mkopo wa nyumba eti hadi angalau afikishe umri wa miaka 50,mkopo wa elimu tu hawataki kutoa kwa mfanyakazi anayetaka kujiendeleza wakati ni jasho lake..!! Ila wao serikali wakizitaka fedha za mifuko hii wanachukua kiulaini tu..!!
Kama wamepima upepo ndio maana wamekupa majibu hayo!!!
Mkuu hebu nipigie mahesabu mimi mlalahoi mwenye basic ya milioni 2 nikistaafu leo nitapata kiasi gani?
Nilibahatika kusoma mfumo huu mpya wa kucalculate mafao.. Asehhh ni noma sana bonge la panga.... Yan aliyestahili kiinua mgongo cha milion 120 ataamblulia milion 30 Kama sheria mpya ikipita
ahahahahaha wafanyakaz wakichemka hili.. Bas kwisha habari yao... Na mbunge atakayetetea muswada huu basi ni yule aliyeuchoka ubunge wake....