Serikali ya Tanzania imekusudia kupeleka muswada bungeni utakaoleta utaratibu mpya wa jinsi ya kulipa mafao kwa wastaafu wote walio jiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii,kupitia sheria hiyo ambayo serikali inataka itumike kulipa mafao ya wastaafu itakuwa hivi.
Kila mstaafu wa umma au binafsi atapewa robo ya kile anachotakiwa kupewa baada ya kustaafu kazi, yaani kama anatakiwa apewe millioni 100 basi yeye atapewa million 25,halafu baada ya malipo hayo kufanyika ni kwamba mstaafu atakuwa anapewa kila mwezi nusu ya basic salary yake aliyokuwa anapata kabla ya yeye kustaafu,malipo hayo atakayo kuwa anapata mstaafu yatakoma pindi tu atakapo fariki.
Ikumbukwe kwamba kujiunga na mfuko wa hifadhi ya jamii ni lazima kwa mwajiriwa yoyote na umri wa kustaafu kwa mujibu wa sheria ni miaka 60.
Msimamo wa vyama vya wafanyakazi:
Vyama vya wafanyakazi vimepinga muswada unaotaka kupelekwa bungeni na serikari, mara zote tatu vyama vya wafanyakazi walipo kutana na wawakilishi wa serikali huko mbeya,dodoma na hata mara ya mwisho arusha walipokutana hasira zilijitokeza kupinga jambo hilo kwani ni unyonyaji uliokithili unaotakiwa kuletwa,kwa mujibu wa mnyetishaji wangu mkutano wa mwisho kati ya wawakilishi wa serikali na vyama vya wafanyakazi unatarajiwa kufanyika Dar kabla ya bunge kuanza mwishoni mwa mwezi huu,ili ikiwezekana muswada huo upelekwe kujadiliwa na wabunge wa wakilishi wa wananchi.
Inasemekana kwanba muswada huu wa sheria ulitakiwa kupelekwa bungeni tangu mwezi Novemba ktk bunge lililopita,ilishindikana kutoka na suala la escrow kuchukua muda mwingi zaidi.
Wachache wafanyakazi nilio sikia maoni yao wamesikitika na wanaona kama sheria hiyo ikipita basi waajiriwa wengi watakufa maskini kwani mtu wa miaka 60 kwa Tanzania anakuwa na muda mchache sana wa kuishi,ukizigatia wengi wao wanategemea pesa za kustaafu ili wajenge nyumba nzuri na kuanzisha vitega uchumi tofauti...!!
NB: Serikali imeikopa sana mifuko hii ya hifadhi ya jamii kiasi kwamba inashindwa kujiendesha vizuri,hivyo inatafuta namna ya kuiokoa na balaa la kufilisika.Chuo kikuu cha Dodoma ni fedha za mifuko hii hadi leo bado hazijarudi!