Sheria kuhusu Ndoa za Utotoni

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Ndoa za utotoni ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu kwa wasichana. Sheria ya Elimu nchini Tanzania, ya mwaka 1978 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2016 inapiga marufuku ndoa za wanafunzi; hata hivyo, Sheria haijasema lolote kuhusu wasichana ambao hawako shuleni na kwa umri wao wangepaswa kuwa katika mfumo wa Elimu. Sheria ya ndoa bado inaruhusu mtoto wa kike kuolewa na umri wa miaka 15.

Tanzania bado haijafanya mapitio ya Sheria ya Ndoa ili kutoa ulinzi dhidi ya ndoa za utotoni, ingawa iliashiria kwamba itafanya hivyo. Pia, mipango kazi ya serikali ya kushughulikia ukatili dhidi ya wanawake na watoto haiweki mikakati ya kina kukabiliana na ndoa za utotoni.

Takwimu za Utafiti wa Idadi ya Watu na Afya (TDHS), 2015-2016 zilionyesha kuwa asilimia 36 ya mabinti wenye miaka 20 hadi 24 waliolewa kabla hawajatimiza umri wa miaka 18. Kwa mujibu wa Utafiti wa Demografia ya Afya nchini (TDHS) wa mwaka 2010 mikoa yenye viwango vikubwa vya ueneaji wa ndoa za utotoni hapa nchini ni Shinyanga (59%), Tabora (58%), Mara (55%) na Dodoma (51%).

Hii ni sawa na kusema kuwa kwa wastani, wasichana wawili kati ya watano huolewa kabla hawajatimiza umri wa miaka 18.
 
Back
Top Bottom