Sheria kandamizi ziondoshwe zidi ya raia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheria kandamizi ziondoshwe zidi ya raia

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kakke, Dec 27, 2011.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Dec 27, 2011
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [h=1][/h]Written by Hassan10 // 27/12/2011 // Habari // No comments

  [​IMG]Marangi vyombo vya ulinzi na usalama huchukuwa sheria kali mikononi mwao zidi ya raia, mambo haya yemezoeleka na vyombo vyetu vya ulinzi kutumia sheria mikononi mwao bila ya muhusika kupelekwa mbele ya Mahkama na kujibu tuhuma.
  Hivi sasa jamii yetu imejenga chuki na vyombo ya usalama kutokana na kukosa kuwa karibu na mapenzi na wananchi kwa vitendo vyao vya kutumia nguvu kupita kiasi.
  Mtuhumiwa kabla ya kupelekwa Mahkamani na kusomewa mashtaka yake kuwa mkosa au laa, basi huko nyuma tayari ameshahukumiwa na vyombo vya usalama kabla ya kufikishwa kwa hakimu na kusibitishwa kosa lake nini?.
  Mambo haya yemezoweleka hapa kwetu na kwa vile serekali iko kimya kuwashukulia hatuwa wahusika wa vyombo vya usalama basi imekuwa ni mazowea kwao kushukuwa sheria mikonono kwao.
  Nilazima Serekali iwape mafunzo na elimu yakutosha kuhusu vyombo vya usalama bila ya hivyo itakuwa nchi haina sheria na mambo yakizidi basi wananchi watakuwa na wao masugu wakujibu mapambono.
  Kazi ya vombo vya usalama nikulinda raia na mali zao sio wao kufanya hujuma zidi ya raia, katika nchi zilizo endelea vyombo vya usalama vinakuwa rafiki na karibu na wananchi ili kujuwa shida zao na kusaidiana katika kazi.
  Lakini hapa kwetu sio hivyo vyombo hivyo vimekuwa Paka na Chuwi na wananchi kutokana na kutunicha misuli yao na kujifanya wababe mbele ya Rais.
  Ni raia wangapi wanakufa kwa kibano kikali ama uraiani au mahabusu bila kufikishwa Mahakamani na kujibu mashtaka ?.
  Mfumo huu umesambaa mpaka katika tasisi nyingine za kazi kama vile Madaktari wazembe kuuwa kwa uzembe wa kazi zao bila kujulikana au kufanyika uchunguzi, yeye akichafanya uzembe huvuta buku la report na kuandika apendavyo yeye na mwisho kuwambia familia washkuru M/mungu jitihada imepita haikufanikiwa.
  Ukiangalia kwa kina kuna kesi nyingi tu za Uzembe wa Vyombo vya Usalama na Madaktari kutumia madaraka yao bila nizamu ya kazi na hufanya hivyo kwa mazowea bila kuguswa .
  Kwa hio tunaiomba Serekali yetu ipitie katika maeneo haya ili kuweza kuwanusuru raia kuwawa kizembe , wengi wa maafa haya ni maskini za Mungu kama hivi mie. Lakini vigogo hukwepwa katika mambo haya.
   
 2. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #2
  Dec 27, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Mh jamani huu si ubinadamu,kwanza hapo utakuta huyo jamaa hata hajabisha ila analazimishwa na kupigwa....mh kazi ipo kwa watanzania jamani.
   
Loading...