Sheria kali za Ndugu zetu Taliban

ksk

JF-Expert Member
Mar 30, 2016
930
1,000
Uko kwenye Quran. Labda wewe hujui kuisoma.

Ukumbuke Quran imeandikwa kiarabu, wale ni waarabu wanaielewa kuliko nyie waarabu kuja.

Hivyo wanachokifundisha Taliban ni 100% islam, purely islamic. Hakuna wanapokosea.
Tofautisha Uislamu na Uarabu. Waarabu unaweza kusema ni kabila. Uislamu ni dini. Na kwa taarifa yako wapo Waarabu wakristu, na juu ya yote taalibani siyo Waarabu bali Waafghanistani (kabila na nchi). Tambua pia Waislamu wengi duniani wako nje ya kule dini ilipoanzania (Uarabuni). Nikukumbushe pia hata wakristu wanatofautiana, huwezi kuwaambia Wakristu eti kinachofundishwa na Walokole ni 100% ukristu.
 

ksk

JF-Expert Member
Mar 30, 2016
930
1,000
Taliban kama wanataka ndevu watu wafuge tu..mbona nyie watumishi wa serikali mnakwangua kidevu mpaka vipele vinatoa machozi...nyie mliwafuata wazungu na wao wanafuata sharia..ila sio lazima katika uislamu kuwa na ndevu maana kuna viumbe hawakujaaliwa ndevu.
Kufuga ndevu siyo utmaduni wa Kiarabu/Kiislamu tu, bali hata Wayahudi Asilia (Orthodox Jewish) hutakiwa kufuga ndevu.
 

Hakimu Mfawidhi

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
3,037
2,000
Tofautisha Uislamu na Uarabu. Waarabu unaweza kusema ni kabila. Uislamu ni dini. Na kwa taarifa yako wapo Waarabu wakristu, na juu ya yote taalibani siyo Waarabu bali Waafghanistani (kabila na nchi). Tambua pia Waislamu wengi duniani wako nje ya kule dini ilipoanzania (Uarabuni). Nikukumbushe pia hata wakristu wanatofautiana, huwezi kuwaambia Wakristu eti kinachofundishwa na Walokole ni 100% ukristu.
Hauwezi kutofautisha uislam na uarabu, hilo haliwezekani. Usidanganywe na mtu yeyote. Uarabu na uislamu ni mate na ulimi, samaki na maji.

Ndio maana uislamu unahubiriwa kiarabu. Huwezi kuondoa uislamu kwenye uarabu, haiwezekani.
 

Kiduila

Senior Member
Jun 22, 2017
162
250
SWALI

:

ufugaji wa ndevu ni suna ya lazima au si ya lazima?

na kama ni yalazima nikufuga ndevu za kwenye kidevu ao machavu?


JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Ndevu baadhi ya Maulamaa wanasema ni Sunnah iliyokokotezwa, lakini Maulamaa wengi wa mwanzo na wa sasa wamesema ni zaidi ya hivyo, yaani ni WAAJIB, na mtazamo huu ni msimamo SAHIHI kwa dalili nyingi. Kuna shahidi nyingi kuthibitisha hilo.

Dalili katika Qur-aan tunaona kwamba hata mitume walikuwa wakifuga ndevu. Hii ni kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kuhusu Haaruun ('alayhis-salaam alipomwambia Musa ('alayhis-salaam) alipomshika ndevu zake baada ya kuwaona wana wa Israaiyl wamepotoka:

((Akasema: Ewe mwana wa mama yangu! Usinishike ndevu zangu, wala kichwa changu. Kwa hakika naliogopa usije sema: Umewafarikisha Wana wa Israil, na hukungojea kauli yangu)) [Twaaha 20:94]

Hapa tunakupa dalili zilizothibitika katika Sunnah:

1. Mtawala wa Yemen, aliyechaguliwa na Mfalme wa Kiajemi Kisraa, alituma majumbe wawili kwa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kumpelekea mwaliko. Wakati hao walipotokezea mbele ya Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), aliwaona hao wamenyoa ndevu na kufuga masharubu (ndevu za mdomo). Kwa hayo yeye alichukizwa kuwatazama hao (kwa sababu ya kuonekana visivyo sawa) na aliwaambia : "Ole wenu ! Je ni nani aliyewaambia kufanya hivyo ?" Wao walimjibu: "Bwana wetu! (wakimaanisha Kisraa)."
Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliwaambia: "Lakini Mola wangu, aliye Mkuu
na Aliyetukuzwa, ameniamrisha mimi kuibakiza ndevu yangu peke yake na kunyoa masharubu yangu." [Imerekodiwa na Ibn Jarra-abar, na al-Albaaniy kuwa ni Hasan (nzuri) ]

2. Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amewaamrisha wanaume wafuge ndevu peke yake. Hadiyth zifuatazo pia zina maana hizi hizi : "Nyoeni masharubu na muziache ndevu".[Al-Bukhaariy na Muslim]

3. Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:"Nyoeni masharubu yenu na muoteshe ndevu zenu. Muonekane tofauti na Wamajusi (wafuasi wa dini ya waabudu moto iliyokuwapo huko Uajemi [Iran]). [Muslim]

4. Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Nyoeni masharubu yenu na kuziacha ndevu zenu peke yake. Muwe tofauti na Ahlul Kitaab (Mayahudi na Manaswara)." [Muslim]

5. Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Muwe tofauti na Mushrikiyn, mnyoe masharubu yenu na kufuga ndevu" [Al-Bukhaariy na Muslim]

Kwa kifupi hizi ni dalili chache kuonyesha Uwajibu wa jambo hilo, na vilevile ni maarufu kuwa Maimam Abu Haniyfah, Maalik, Ash-Shaafi'iy, Ahmad bin Hanbal na wengineo wamesema ni HARAAM kunyoa ndevu.

Na kwa kufahamu kuwa jambo hilo ni baya na ni ukiukwaji wa sheria ambayo imetoka kwa Muumba na kuthibitishwa kimaelekezo na kivitendo kwetu na Mjumbe Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ndio Maimaam hao wakatoa maamuzi yao katika suala hilo.

Amiyr Muadilifu 'Umar ibn 'Abdul-'Aziyz inasemekana katika vyanzo vya kihistoria kuwa alikuwa hakubali katika utawala wake ushahidi wa mtu mwenye kunyoa ndevu! Vilevile tunaona kwenye madhehebu mbalimbali za Kiislam, haruhusiwi mtu kuswalisha ikiwa haweki ndevu kutokana na jinsi walivyofahamu uzito wa jambo hilo na Uwajibu wake.

Na ndevu ni mashavuni na kidevuni, unapaswa kufuga ndevu zote na si kidevuni pekee ambazo zaitwa mzuzu na ukanyoa za mashavuni; utakuwa unafanya makosa; zote hizo ni ndevu, ama zilizoko juu ya mdomo wa juu ambazo ni masharubu, hizo zatakiwa kupunguzwa na zisiwe refu.

Kwa maelezo na faida zaidi bonyeza viungo vifuatavyo:(Kwa hisani ya Alhidaya.com)
 

Ulongupanjala

JF-Expert Member
Apr 9, 2013
4,409
2,000
Talebani wanawataka wanaume msio na ndevu mvae majuba (hijabu)
Ukishindwa kuvaa juba ni marufuku kutembea mtaani jifungie chumbani kwako.
 

Cherenganya

JF-Expert Member
Jan 21, 2018
2,258
2,000
Unaweza ukathibitisha vp kwamba kiongozi huyu ni Muadilifu ilihali kaingia madarakani kwa mtutu wa Bunduki na sio kwa shura?

Bwana Mtume SAW alituachia nn katika hotuba yake ya Mwisho baada ya kuiteka Makka?

Mtu atakosea akisema hizo dalili ni zile za kuokoteza?

Msingi mkuu ikiwa ni "hakuna kulazimishana katika Dini"
 

Cherenganya

JF-Expert Member
Jan 21, 2018
2,258
2,000
Ndio tumewauliza hapo,wenyewe wamesema ni haramu kwa mwanaume kunyoa ndevu. Kwa msisiitizo No dume nyoaling nduvu
Shida yako unaleta masihara katika mambo ya msingi. Ndugu Uislamu hauungwi ungwi kama Dini nyingine hoja zake lazima ziwe na dalili kwa maana Quran na Khadith sahihi (vipo vigezo vya hadithi ipi ni sahihi na ipi ni dhaifu na hapa si mahala pake)
 

Tangantika

JF-Expert Member
Aug 12, 2018
3,069
2,000
Nimekua Muislam muumini kwa takribani miaka 40 sasa sijawahipo kusikia wala kusoma Aya ya Quran au Khadith ya Mtukifu wa Daraja, Bwana Mtume Mohammad S.A.W ikilazimisha jambo lolote bali kupinga kulazimisha.

Huu uislamu wao wanautoa wapi?
Hata mimi nashangaa kama kuna siku ya hukumu(kiama) kwa nini umlazimishe mtu kusali, kuacha zinaa,pombe, kufuga ndefu nk.
Talibani bado ni primitive people ambao wanawaza dunia ya mwaka 1400 .
Nilikaririshwa quran mpaka leo sioni tofauti na yule ambae hajakariri.
Taliban wanawaza kila mtu dunia nzima awe mujahidina ila uwezo wa kutulazimisha wote hawana, ni wapumbavu tu.
 

Tangantika

JF-Expert Member
Aug 12, 2018
3,069
2,000
Taliban kama wanataka ndevu watu wafuge tu..mbona nyie watumishi wa serikali mnakwangua kidevu mpaka vipele vinatoa machozi...nyie mliwafuata wazungu na wao wanafuata sharia..ila sio lazima katika uislamu kuwa na ndevu maana kuna viumbe hawakujaaliwa ndevu.
Hili nalo jambo, ila kulazimishana kukata ndevu kazini haikatazwi.
 

mfianchi

JF-Expert Member
Jul 1, 2009
10,826
2,000
Uko kwenye Quran. Labda wewe hujui kuisoma.

Ukumbuke Quran imeandikwa kiarabu, wale ni waarabu wanaielewa kuliko nyie waarabu kuja.

Hivyo wanachokifundisha Taliban ni 100% islam, purely islamic. Hakuna wanapokosea.
Sio waarabu wote ni waislamu na sio kweli kuwa kwa kuwa ni waarabu basi wanajua quraan, je wazungu kwa kuwa wengi wao ni wakristo wao ndio wanaijua biblia zaidi?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom