Sheria inasemaje kuhusu hili?

Mlanga

JF-Expert Member
Jun 7, 2014
1,023
467
MSAADA WA KISHERIA DPP ,AG ,MAJAJI, MAHAKIMU,MAWAKILI NA WADAU WENGINE WA TAALUMA YA SHERIA.

Wakuu naomba kufahamishwa kwamba sheria ya nchi yetu inasemaje iwapo ikibainika mtu au kikundi cha watu wamebeba silaha na kuvamia eneo kwa nia ya kujichukulia mali.

  1. Je jukumu la kuendesha mashitaka ya aina hii ni la nani?
  2. Kipindi ambacho kesi inaendeshwa mtuhumiwa/watuhumiwa wanakuwa na haki ya dhamana?
  3. Je thamani ya mali iliyochukuliwa ni kigezo cha kufungua shitaka?
 
MSAADA WA KISHERIA DPP ,AG ,MAJAJI, MAHAKIMU,MAWAKILI NA WADAU WENGINE WA TAALUMA YA SHERIA.

Wakuu naomba kufahamishwa kwamba sheria ya nchi yetu inasemaje iwapo ikibainika mtu au kikundi cha watu wamebeba silaha na kuvamia eneo kwa nia ya kujichukulia mali.

· Je jukumu la kuendesha mashitaka ya aina hii ni la nani?

· Kipindi ambacho kesi inaendeshwa mtuhumiwa/watuhumiwa wanakuwa na haki ya dhamana?

· Je thamani ya mali iliyochukuliwa ni kigezo cha kufungua shitaka?

Jamhuri ndiyo yenye jukumu la kushitaki. Lakini kuna kitu kinaitwa private prosecution. hata wewe unaweza kwenda mahakamani kushitaki
 
Jamhuri ndiyo yenye jukumu la kushitaki. Lakini kuna kitu kinaitwa private prosecution. hata wewe unaweza kwenda mahakamani kushitaki

Je private prosecution ni mbadala wa Public prosecution ?
 
Je private prosecution ni mbadala wa Public prosecution ?
Yah Criminal procedure Act inaruhusu mtu kufungua kesi ya jinai
But kama DPP akiitaka ataichukua na kuiendesha au kuamua kutoiendesha CPA inampa mamlaka hayo
 
Je private prosecution ni mbadala wa Public prosecution ?
No, not at all. Mfano si unaona Bashite anakingiwa kufua wakati kuna jinai zinamkabili. Mwananchi unaweza kwenda kushitaki ingawa kuna mizengwe maana DPP anaweza kuamua ku withdraw kesi yako! Sheria inamruhusu!
 
Mkuu umegonga msumari. Kesi iliyozaa maswali yangu ni hiyo ya huyo MTU na genge lake. Jamhuri kama vile inakimbia majukumu, nini kifanyike ? Na nani?
 
Tanzania Hakuna private prosecution
ipo, inaruhusiwa ila haijawai kutokea mtu akaenda mahakamani! Unaripoti polisi wanachukua mashitaka!
Usiwe na tabia ya kukanusha jambo bila uhakika, seems wewe siyo msomi!! read this
Private Prosecution
As part of the recommendations of the Judicial Review Commission in 1977 the right to private prosecution was
retained. Under s. 99 CPA a private citizen may with leave of the Magistrate institute a prosecution in person or through
an advocate. It is an important right provided it does not amount to an abuse of court process, a possible defect curable
by the DPP’s power to take over and discontinue proceedings.
 
Back
Top Bottom