Daisy Llilies
JF-Expert Member
- Apr 19, 2019
- 1,017
- 2,154
Kaka mmoja alikuja mkoani kwetu kwa barua kutoka Wizarani, aliletwa pale kama Ofisa wa Serikali. Ule mkoa una neema sana, ndani ya miaka miwili yule kaka aliweza kujenga ghorofa pale mjini.
Siku ya ufunguzi wa ghorofa lile, alitualika watumishi wenzake, viongozi wa dini na mama yake mzazi tuliambiwa atafika na basi la saa saba mchana hivyo dua zimsubiri mgeni huyu muhimu.
Tulifika saa 12 asubuhi kusaidia shughuli, tulikata vitunguu na kupika pilau, tulikata kachumbari na tulitengeneza salad ya matunda. Wali maharage na wali kuku havikukosekana.
Basi la saa saba likawasili, mwenye sherehe akaenda kumpokea mgeni wa muhimu. Kufika kule wanamkuta mama amekauka kwenye kiti cha basi. Alifariki saa ngapi ni siri ya Mungu. Basi chakula cha sherehe kiligeuka kuwa cha msiba.