Shemejio kaipenda akiomba kumpa ni dhambi???


P

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Messages
40,011
Likes
8,831
Points
280
P

Pdidy

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2007
40,011 8,831 280
John Terry Anyang'anywa Unahodha Baada ya Kumtia Mimba Shemeji Yake

John TerryFriday, February 05, 2010 9:50 PM
Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Uingereza, Fabio Capello amemnyang'anya unahodha John Terry kufuatia skendo lake la kumtia mimba mpenzi wa mchezaji mwenzake na kisha kuitoa mimba hiyo.Skendo la John Terry kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mpenzi wa mchezaji mwenzake wa timu ya taifa ya Uingereza limefikia hatua nyingine kwa kocha wa Uingereza kumvua unahodha John Terry.

John Terry ambaye ana mke na watoto wawili anashutumiwa kumzunguka rafiki yake Wayne Bridge ambaye walicheza pamoja Chelsea na kutembea na mpenzi wake mrembo wa Ufaransa, Vanessa Perroncel.

Mbali ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Vanessa ambaye amezaa mtoto mmoja na Wayne Bridge, Terry anadaiwa kumtia mimba Vanessa na kisha kuitoa mimba hiyo ili siri ya uhusiano wao isifichuke.

Terry alianza uhusiano na Vanessa mwaka jana baada ya Wayne Bridge kuhama Chelsea ya London na kuhamia mjini Manchester kuichezea Manchester City.

John Terry anacheza nafasi ya kati ya ulinzi katika timu ya taifa ya Uingereza wakati Wayne Bridge naye yumo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza akicheza kama beki wa kushoto.

Akiliongelea suala hilo leo mchana, kocha wa Uingereza raia wa Italia, Fabio Capello alisema kuwa ili kuikoa timu ya taifa ya Uingereza isifanye vibaya kwenye kombe la dunia, ameona ni bora amnyang'anye unahodha John Terry.

Vyombo vya habari vya Uingereza vililishikilia bango skendo la Terry na kutaka anyang'anywe unahodha lakini chama cha soka cha Uingereza kilisema kuwa uamuzi wa mwisho atautoa Capello.

Capello ameamua kumchagua Rio Ferdinand kuwa nahodha mpya wakati Steven Gerrard atakuwa nahodha msaidizi.
 
Ndahani

Ndahani

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2008
Messages
14,745
Likes
2,035
Points
280
Ndahani

Ndahani

JF-Expert Member
Joined Jun 3, 2008
14,745 2,035 280
si umeshasema waliotoka nje ya ndoa waombe msamaha valentine day?
 
drphone

drphone

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2009
Messages
3,561
Likes
94
Points
145
drphone

drphone

JF-Expert Member
Joined Sep 29, 2009
3,561 94 145
ruksa tu mbaya kupindua
 

Forum statistics

Threads 1,250,505
Members 481,371
Posts 29,736,013