Ukistaajabu ya Ten Hag na Cristiano, utakutana na ya Capello na Ronaldo

Gang Chomba

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
20,301
4,681
IMG_6400.jpeg
Baada ya vuguvugu la habari zisizo na uaminifu ndani yake, hatimae Ronaldo akihojiwa katika kituo cha Runinga cha FOX chenye matawi yake huko Amerika ya kaskazini na ya Kusini, amesema kuwa kamwe hakutaka kuondoka klabuni Madrid.

De Lima maarufu kama “O fenomeno” ama elgodo ikimaanisha bwanyenye ameweka wazi kuwa hakuwa na furaha wala hakuwa tena na thamani kwa mwalimu wa klabu hio.

Anasema kuwa Fabio Capello alikuwa akimuandama sana kwa kumshambulia kwa maneno na kumuona kama kituko. Njia pekee ya Capello kunifanya nipungue unene aliona ni kunishambulia na kunidhalilisha.

Kwa hayo sikuweza kukasiri, ila mwalimu huyu alikwenda mbali zaidi na kuanza kuniweka benchi na hata kuniacha kwenye kikosi cha Real Madrid.

Hapa Capello alikosea sana, hakufahamu kuwa mimi ni Ronaldo ambae nilimsuta mara kadhaa kwa kuwa kila alipokuwa akinipa nafasi uwanjani basi nilikuwa nafunga magoli pamoja na kilo zangu ambazo zilikuwa zapata 100.

Kwa hio usiku mmoja niliwaza saana mustakabali wangu wa kucheza soka klabuni hapo, kisha nikagundua kuwa mimi ni mwenye hadhi ya juu, hivyo sipaswi kuwa sababu ya kuiyumbisha klabu kubwa kama Madrid kwa kuwa chanzo cha mgogoro klabuno hapo.

Hivyo nikawasiliana na wakala wangu na kumueleza dhamira yangu ya kutimka klabuni hapo…Lakini je ni wapi pa kwenda kabla sijaondoka barani Ulaya?

De Lima kwa furaha huku akicheka anaeleza kuwa alikumbuka Siku alipo waaga washabiki wa Inter kabla ya kuhamia Real kwamba aliwaahidi ipo Siku atarudi Jijini Milan.

Lakini pia alikumbuka ujumbe wa Chuki uliotumwa kwake na mashabiki wa Inter Milan maarufu kama Curva Nord wa kumuita Msaliti anaestahili mabaya kila awapo usingizini au akiwa macho.

Hivyo De Lima akachagua kurudi Jijini Milan kama alivyo ahidi lakini safari hii akatua na kusaini kuichezea AC Milan, klabu ambayo imepitiwa na Nyota wengi mnoo wa Kibrazil ambao walipata mafanikio makubwa kisoka.

De Lima anasema asingeweza kuondoka Ulaya bila kuagwa kwa heshima na washabiki wa klabu yenye historia kuubwa ya Soka Ulimwenguni.

De Lima ambae majuzi tu alitimiza miaka 47 tangu alipozaliwa anasema siku ambayo alipata furaha iliotukuka ilikuwa ni siku alio pokelewa katikati ya msimu na tupsi ya mashabiki wa AC Milan maarufu kama Curva Sud waliokuwa wakiporomosha mapambio na masongi ya kumsifu na kumtukuza.

Anaeleza furaha yake ya kukutana na badhi ya wabrazil klabuni hapo huku akipokelewa na mwalimu mwenye hadhi ya juu kabisa katika mchezo wa Soka Don Carlo ama Carlo Ancelotti.

De lima akiwa klabuni Milan alikutana na nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil Emerson da Rosa Fereirra do Santos ambae alishawahi kusema kuwa “I wasn’t able to see Pelé play, but I’ve seen Ronaldo, and I’ve never seen a player like him. He’s unique, number one in everything”
 
Huyu jamaa ball control yake ilikuwa ya kiwango kikubwa mno, unaweza kudhani kama Mpira utaupata vile ukijaribu anakulamba chenga...hichi ni kipaji halisi, alipokuwa bonge pia aliupiga mwingi vilevile, ila Kwa ujumla brazili huchezea vipaji vyao sana na mazoezi kidogo basi tofauti na ulaya mazoezi mengi, kukariri position Kwa sana na kujitambua kwao ni Kwa Hali ya juu pia.
 
Nesta na ujeuri wake woote alitamka wazi kuwa hakuna mshambuliaji mgumu kumkaba kama De Lima…
1. Ana mwendo
2. Ana chenga
3. Haogopi kiatu
4. Anajuwa kujipanga
5. Ana nguvu

Ila Ronaldo mwenyewe anamuelewa Nesta ni nani. Nesta alikua ni best defender of his time
 
Daaaah unalikumbuka goli la kwanza alipiga upande uleule aliojaa Barthez na goli likaingia, goli la tatu jeee Kocha Vicent del Bosque alishangilia kwa kumwambia Ronaldo ana akili ile anafanyiwa sub mashabiki wa Man U walisimama kumpa heshima yake huyo ndo Ronaldo de Lima!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom