Shemeji zangu wakurya sasa dunia imebadilika

mtimawachi

JF-Expert Member
Apr 1, 2020
2,017
3,037
Sina nia ya kukashfu wa kutukana kabila la mtu, ila hapa natoa mtazamo wangu mimi kama mtimawachi.

Tukija kwenye baadhi ya vitabu vya dini vinakiri kabisa kuwa mwanamke ni kiumbe dhaifu. Tumeaswa kuwapenda wake zetu, mtume Mohammad ameonya kuhusu kupiga mke akaongeza kama ikibidi mpe pigo jepesi.

Sasa shemeji zangu WAKURYA inakuwaje umpige mkeo kipigo kizito namna hii. Eti unamshikia panga, kisu fimbo hujui kama hiki ni kiumbe dhaifu?

Hakuna sifa yoyote utakayopata eti umepambana na mkeo umeshinda!
NAKUBALI wanawake wa gubu,lakini haina maana kuwadhalili

Mimi mbona dada yenu simpigi na huu ni mwaka wa 16 nipo nae lakini nyie miezi 3 tayari MMEMNYOA na KISU dada yangu.

Ninawaomba mashemeji zangu mmbadilike, hizo habari za kuwajeruhi wake zenu zibakie hadithi tu.

NB: Kama wewe ni Mkurya na haumbughudhi mke huu uzi haukulengi
Na wewe kama siyo Mkurya lakini una tabia tajwa hapo juu ubadilike.

Mwisho nimalizie kwa kusema dada yenu anawasalimia huku anasema anawashukuruni kwa kumuoza kwa dume la KIMAKUWA mtimawachi

NAJUA mkisoma uzi huu mtatamani kunikatakata lakini nilishasoma 'grid reference' ya adui nikajua hamuwezi nifikia
 
Sina nia ya kukashfu wa kutukana kabila la mtu,ila hapa natoa mtazamo wangu mimi kama mtimawachi
Tukija kwenye baadhi ya vitabu vya dini vinakiri kabisa kuwa mwanamke ni kiumbe dhaifu
Tumeaswa kuwapenda wake zetu,mtume Mohamad ameonya kuhusu kupiga mke akaongeza kama ikibidi mpe pigo jepesi.
Sasa shemeji zangu WAKURYA inakuwaje umpige mkeo kipigo kizito namna hii.Eti unamshikia panga,kisu fimbo hujui kama hiki ni kiumbe dhaifu? hakuna sifa yoyote utakayopata eti umepambana na mkeo umeshinda!
NAKUBALI wanawake wa gubu,lakini haina maana kuwadhalili
Mi mbona dada yenu simpigi na huu ni mwaka wa 16 nipo nae lakini nyie miezi 3 tayari MMEMNYOA na KISU dada yangu
Ninawaomba mashemeji zangu mmbadilike,hizo habari za kuwajeruhi wake zenu zibakie hadithi tu

NB:kama wewe ni mkurya na haumbughudhi mke huu uzi haukulengi
Na wewe kama siyo mkurya lakini una tabia tajwa hapo juu ubadilike
Mwisho nimalizie kwa kusema dada yenu anawasalimia huku anasema anawashukuruni kwa kumuoza kwa dume la KIMAKUWA mtimawachi
NAJUA mkisoma uzi huu mtatamani kunikatakata lakini nilishasoma 'grid reference' ya adui nikajua hamuwezi nifikia
Usi mention kabila ya mtu cku hizi ayo mambo ya vipigo kila sehem zipo uku kwetu kuna jamaa kamchoma mkewe na mkaa na co Mkurya!!!
 
Siku hizi wanaoa wachaga (makabila) vipigo vimepungua sababu ya kuoa wageni.

Lakini wakioa wanawake wa Kabila Lao vipigo huwa pale pale kama kawaida.
 
Wakioa makabila wengine wanakuwa na adabu zaidi hawawabutui wanawake zao kirahisi rahisi lakini wakioa wakurya wezao vipigo huwa palepale.
 
Kuna unyanyasaji mkubwa wa kijinsia na wengine hata kupoteza maisha na ulemavu wa kudumu lakini juhudi za kutoa elimu ya mahusiano na kuwachukulia hatua kali wakosaji wala hazionekani Ndiyo maana matukio huendelea kufanyika siku hadi siku.

Tabia ya wanafamilia wengine kupenda kuyamaliza mambo kienyeji ndipo matatizo huaendelea.
 
Mkuu hapa umejazia nyama huu uzi,nilifika tarime,kemange,gamasara daah! yaani wanawake mara kanyofolewa sikio mara mkono,Inatisha
 
Wakurya hawajui thamani ya mwanamke na Mateso ni mengi acha kabisa
Mke kapika nyama ya kuku baba mkwe katembelea ghafla kaandaliwa kidali mume arudi aandaliwa chakula aulizia kidali mke akajibu nimempa baba mkwe(baba wa mume)
Mume akapandwa hasira akamkata mkewe mkono.visa vya hovyo kabisa
 
Mkuu hapa umejazia nyama huu uzi,nilifika tarime,kemange,gamasara daah! yaani wanawake mara kanyofolewa sikio mara mkono,Inatisha
Na wengi hawajui kama ni jukumu Lao kumhudumia mwanamke.....mwanamke ni kama punda afanye kazi mume ale na watoto na ni marufuku kulala lala eti anaumwa,
 
Tena makabila hayo ya bara huko kanda ya ziwa kuoa mitala kwao ni jambo la kawaida hata kama ni Wakristo

Yani kuwa na michepuko ni jambo la kawaida kwao.

Unakuta baba mkwe mwenyewe anamitala chungu nzima halafu ni Mkristo eti?!

Kesi ya uasi ktk ndoa Mwanaume kuchepuka ukiwaambia ndugu zake au wanajamii watakushangaa wewe mwanamke wa ndoa.
 
Yani Mwanaume kuchepuka, kuwa na watoto nje ya ndoa ni jambo la kawaida kupita kiasi.

Sijui ukristo wanafundishwaje?
 
Na wengi hawajui kama ni jukumu Lao kumhudumia mwanamke.....mwanamke ni kama punda afanye kazi mume ale na watoto na ni marufuku kulala lala eti anaumwa,
Tuna safari ndefu sana wanaume sisi
 
Huku kanda pendwa hatujui kubembeleza wanawake sie.lakini cha ajabu watoto wakali kutoka kilimanjaro na Singida wanatupenda hatari.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom