Shemeji yenu hataki tufuge mbwa

Shemeji yenu hataki tufuge mbwa

Zekidon

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2013
Posts
1,903
Reaction score
569
Huyu sabuni ya roho anataka kunikalia kichwani wakuu.

Kaanza na gambe, sasa amehamia kwenye mbwa, halafu anaweka ngumu vile vitu navyopenda kupita maelezo.

Tokea nikiwa mdogo mimi ndio nilikua nikileta mvwa nyumbani, kwa asilimia kubwa mbwa wamekua wanyama ninao wapenda mno.

sasa huyu mama anataka kunitenga na furaha yangu ya moyo.

Msaada jamani.
 
Achana nae......we leta mbwa wako bana.......atamzoea tu.......hakuna namna.......
 
Mambwa yafie mbele. Yanachafua uwanja mzima na vinyesi vyao kawa vya binadamu mambo ya kuanza kupita na koleo asbh kuzoa tofauti vimejaa minyoo. Yanabwekea madirishani hadi hakulaliki. Mambwa tupa kuleeee
 
Achana nae......we leta mbwa wako bana.......atamzoea tu.......hakuna namna.......

itabidi tu hakuna namna mbwa ni wanyama wakipekee kabisa.
 
Mambwa yafie mbele. Yanachafua uwanja mzima na vinyesi vyao kawa vya binadamu mambo ya kuanza kupita na koleo asbh kuzoa tofauti vimejaa minyoo. Yanabwekea madirishani hadi hakulaliki. Mambwa tupa kuleeee

Haujui uzuri wa mbwa......""""
 
Mambwa yafie mbele. Yanachafua uwanja mzima na vinyesi vyao kawa vya binadamu mambo ya kuanza kupita na koleo asbh kuzoa tofauti vimejaa minyoo. Yanabwekea madirishani hadi hakulaliki. Mambwa tupa kuleeee

Huyu wako atakuwa koko tu........aina gani ya mbwa hii mkuu.......hivi unajua mbwa kweli.........?..........
 
German sherpherd. Kuna aina ya mbwa wanaenda kunya chooni?

Basi huyo jeremani wako kafundishwa kiswazi..........mimi ninalolijua lina sehemu yako maalum ya kufanya hizo shughuli.........
 
Basi huyo jeremani wako kafundishwa kiswazi..........mimi ninalolijua lina sehemu yako maalum ya kufanya hizo shughuli.........

Kafundishwa na kitengo cha wataalam wa mbwa polisi keko
 
Ni mbwa gani unamleta........?......ngoja nikuwekee picha ya wangu nimemnunua jana..........

tupia mkuu, napenda german shepherd, hawa wanyama wanahisia kama sisi mkuu ukirudi home anakukimbilia na kukurukia huku anatikisa mkia inaleta hisia nzuri sana mkuu stress zote zinapungua.
 
Umezuiwa mpaka gambe hahahahahaha...Pole mkuu na wewe fuga mbwa kumzuia michepuko yake
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom