Preta
JF-Expert Member
- Nov 28, 2009
- 24,320
- 18,886
mkuu mbona huyu dizaini mbegu fupi sana, kazi anaiweza?
Weee.......kinasimamia kucha mbayaaaa..........
mkuu mbona huyu dizaini mbegu fupi sana, kazi anaiweza?
German Shepherd siyo Mbwa wa kucheza cheza naye na kukutikisia mkia, hawa ni mbwa wa kazi.
Unataka toy la kucheza nalo, tafuta aina nyingine ya mbwa.
Usiharibu kizazi cha German Shepherd.
Natafuta kama lile la Obama........sijui linaitwaje.......ila linaonekana linajua intelijensia.............nina kazi nalo kubwa sana.......
Hahaha.........Weee.......kinasimamia kucha mbayaaaa..........
Wangu ni aina ya Rottweller kama una watoto wadogo sikushauri kabisa hawa ni hatari sana wanamjua mkuu wa nyumba tu au mtu anayewapatia chakula mara kwa mara.Wana wivu sana watoto wadogo wana tabia ya kumkimbilia Baba anaporeje nyumbani Rottweler anaweza kukasirika na kujawa na wivu na kuhisi mtoto anataka kuchukua nafasi yake ya kupendwa siku mtoto akiwa mwenyewe anaweza kumshambulia.
Rottweller anatakiwa mara kwa mara kukaa na watu wa nyumbani na pia nyumba yenye nafasi kubwa sio kumweka uchochoroni akifungiwa ndani muda mrefu anakuwa mkali kupitiliza na anaweza kuwasahau watu wa nyumbani na kufanya mashambulizi yasiyotarajiwa.
Kuna wakati home mzee alifuga hawa mbwa.
Kuna siku aliwakuta wanakula mbuzi akajaribu kumuokoa yule mbuzi akajikuta anang'atwa yeye.
Akawauza wote.