pet geo pet
JF-Expert Member
- Jun 30, 2018
- 518
- 815
Wakuu habari!
Naomba niende moja kwa moja kwenye mada sisi katika familia yetu tumezaliwa watoto wanane(08),wakiume wanne(04)na wakike wanne(04).
Dada yangu wa kwanza alishaolewa lakini familia yao haikudumu,lakini huyu dada yangu wa pili yaani anaenifata mimi aliolewa na kijana mwezake toka 2013.
Sikuwepo nyumbani kwa muda wa miaka miwili kwa ajiri ya masomo yangu kwani ni mimi tu katika familia yetu niliofanikiwa kufika elimu ya juu(degree).
Niliporudi nyumbani nilikuta dada yangu zaidi ya mwaka mzima anaishi nyumbani ila Ikifika usiku anaenda kulala kwa mmewe.
Nilipokuwa shule nilikuwa nawasiliana nao asa mama kwani ni mzazi pekee aliebaki duniani nikijaribu kumuuliza, kwanini dada yangu anaishi nyumbani mpaka mwaka mzima na miezi kadhaa wakati mme wake yupo, tena kijana?
Jibu nilikuwa napewa na mama yangu mzazi,shemeji yako bado anajipanga.
Nikauliza tena,anakoishi yeye(shemeji) hapafai kuishi na mke wake?nikasema basi ngoja nje mwezi wa saba niongee na uyo shemeji
Mwezi wa saba ukafika nikaenda nyumbani nikiwa natokea shule nilitisha kikao cha mama na dada yangu, kumueleza kwanini mmeo asikae na wewe?pia kuna tarifa nilipewa huwa anapelekewa chakula cha nyumbani,hiki ndo kiliniuma sana kwanini apelekewe chakula cha nyumbani?
Kikao kilisha nikaamua kumwambia mke wake nenda umwambie kesho aje nyumbani mmeo,pia nikampigia simu ili aje ,haikutosha nilimtumia sms kuwa kesho aje nyumbani.
Ilifika siku hiyo lakini kwa zarau hakuweza kutokea hata kidogo na akatuma sms hatoweza fika nyumbani kwa siku hiyo.
Basi hatua niliochukua nimbebesha dada yangu(mkewe)mabegi na mtoto wake wote nikawapeleka anapoishi huyo mmewe.
Nilivofika tu pale anapoishi akakimbia kulekea nyumbani kwetu,na mimi nilikuwa nishabadilisha mawazo kabisa ya kumusikiliza.ndipo nilimfukuza nyumbani kwetu kwani mimi ndo mkubwa kutokana na mila za kisukuma.
Cha ajabu alianza kukatalia nyumbani hapo ndo niliweka elimu pembeni na kumtoa kwa nguvu,watu walijaa sana,mama pia nae alikuja kutuamua lakini nilikuwa nishapaniki kwa wakati ule nikaona huyu shemeji amezarau familia yetu.
Baada ya siku chache nilichukiwa na familia zima kuanzia mama,wadogo zangu wa kike wote na wakiume wote kwa kitendo kile..mpka sasahivi nishatoka zangu nyumbani nimeamua nikajitaftie maisha yangu.pia nilikuwa natuma sana hela yangu ya kujikimu shuleni kwa ajiri ya kuwasidia hapo nyumbani.
shemeji yangu alikuwa atoi hata mia pale nyumbani lakini chakula anapelekewa na mke wake jioni anaenda kulala nae.qn to ask hivi ile ilikuwa ndoa au walikuwa wanafanya mapenzi..pia nikumpa huyu shemeji uvivu wa kufikiri kabisa.
Wakuu naombeni ushauri wa mawazo kwani hapa sina mbele wala nyuma najua hapa jf kuwa watu wenye uwezo mkubwa wa kuchambua mambo.ushauri wako utanipanua mawazo yangu nilionaya sasa.
Asanteni na karibuni kwa mawazo.