Shemeji yangu wa kiume anadharau mji wetu

Shemeji yangu wa kiume anadharau mji wetu

kama ndugu zako wanalizika wewe shida yako nini? unajuaje kama ni kautaratibu kao na ndo maisha waliyochagua?
Wanawake hawawezi mhudumia mwanaume kwa fadhila kila siku na ni rahisi kumchoka elewa kuna kitu jamaa atakua anasimamia shoo na labda usikute ile mbuzi ulochinjiwa siku umerudi ni ya huyo shemu wako.
 
ok,,,,tumekuelewa wewe ndo msomi pekee kwenye familia yenu.....japo nimekuelewa, ila uandishi wako unatia dosari hiyo "DIGILII" yako......kikubwa ngosha zingatia masomo yako....kwenu wote weshakuona wewe ni mnoko.....hakuna kiongozi wa familia.....jianzie maisha yako.....ndo ishakuwa.....dadako kapenda na mwanamke akipenda haoni......usishangae shemejio anamla dadako hapo kwenu.....
 
yaan anamletea" zalau "hivi hivii
 
Labda anamchukulia dada yako kama tu nyumba ndogo . Mwabamke ndie anampenda zaidi mwanaume !! Hiyo ni kali kwani shemeji akidharauliwa hata huyo dada mtu hapendwi
 
Kama wanamkumbatia shemeji yako,we jitenge nao uwaache wafanye yao...
Lakn nna mashaka na degree yako ngosha,kwa uandsh wako huo,au umeandka ukiwa na frustrations!!!?
 
Dah so sad wanajf sijui watu wenye busara wameenda wap mtu anaomba ushaur wa unaanza kuchambua uandishi yan kitu ambacho n nonsense hemu tubadilike kama huna point za kuchangia bora upite kimyakimya.by the way ngosha m naona umefanya kitu kikubwa sana cha kijasir na kwa anafavofanya shemej yako syo hata kama ameona nature ya family hko so kigezo means hafai kuwa mwanamme na pia familia yako nao umeona walivo sasa nakushauri kama unaroho ngumu ya kwangu ukiona wanasaport ujinga we wape conditions tu afu endelea na life maana yake wakiendelea kukumbatia ujinga lolote litakalotokea wasikuhusishe na msaada kata kabisa
 
Familia ikiwa na wanawake wengi inakuwa na matatizo Sana.
Hicho ndicho unachokutana nacho
 
huna mbele wala nyuma ndio nini yani maisha yako hayaeleweki yako ovyo ama? au unamaanisha hiyo ishu ndio unasema huna mbele wala nyuma...kwa style hiyo we unamatatizo sasa....we kama vipi angalia maisha yako tu kila mtu atavun aanachopanda...suijeleta ugomvi mahala ambapo ni zero
 
Wakuu habari!
Naomba niende moja kwa moja kwenye mada sisi katika familia yetu tumezaliwa watoto wanane(08),wakiume wanne(04)na wakike wanne(04).

Dada yangu wa kwanza alishaolewa lakini familia yao haikudumu,lakini huyu dada yangu wa pili yaani anaenifata mimi aliolewa na kijana mwezake toka 2013.

Sikuwepo nyumbani kwa muda wa miaka miwili kwa ajiri ya masomo yangu kwani ni mimi tu katika familia yetu niliofanikiwa kufika elimu ya juu(degree).

Niliporudi nyumbani nilikuta dada yangu zaidi ya mwaka mzima anaishi nyumbani ila Ikifika usiku anaenda kulala kwa mmewe.

Nilipokuwa shule nilikuwa nawasiliana nao asa mama kwani ni mzazi pekee aliebaki duniani nikijaribu kumuuliza, kwanini dada yangu anaishi nyumbani mpaka mwaka mzima na miezi kadhaa wakati mme wake yupo, tena kijana?

Jibu nilikuwa napewa na mama yangu mzazi,shemeji yako bado anajipanga.

Nikauliza tena,anakoishi yeye(shemeji) hapafai kuishi na mke wake?nikasema basi ngoja nje mwezi wa saba niongee na uyo shemeji

Mwezi wa saba ukafika nikaenda nyumbani nikiwa natokea shule nilitisha kikao cha mama na dada yangu, kumueleza kwanini mmeo asikae na wewe?pia kuna tarifa nilipewa huwa anapelekewa chakula cha nyumbani,hiki ndo kiliniuma sana kwanini apelekewe chakula cha nyumbani?

Kikao kilisha nikaamua kumwambia mke wake nenda umwambie kesho aje nyumbani mmeo,pia nikampigia simu ili aje ,haikutosha nilimtumia sms kuwa kesho aje nyumbani.

Ilifika siku hiyo lakini kwa zarau hakuweza kutokea hata kidogo na akatuma sms hatoweza fika nyumbani kwa siku hiyo.

Basi hatua niliochukua nimbebesha dada yangu(mkewe)mabegi na mtoto wake wote nikawapeleka anapoishi huyo mmewe.

Nilivofika tu pale anapoishi akakimbia kulekea nyumbani kwetu,na mimi nilikuwa nishabadilisha mawazo kabisa ya kumusikiliza.ndipo nilimfukuza nyumbani kwetu kwani mimi ndo mkubwa kutokana na mila za kisukuma.

Cha ajabu alianza kukatalia nyumbani hapo ndo niliweka elimu pembeni na kumtoa kwa nguvu,watu walijaa sana,mama pia nae alikuja kutuamua lakini nilikuwa nishapaniki kwa wakati ule nikaona huyu shemeji amezarau familia yetu.

Baada ya siku chache nilichukiwa na familia zima kuanzia mama,wadogo zangu wa kike wote na wakiume wote kwa kitendo kile..mpka sasahivi nishatoka zangu nyumbani nimeamua nikajitaftie maisha yangu.pia nilikuwa natuma sana hela yangu ya kujikimu shuleni kwa ajiri ya kuwasidia hapo nyumbani.

shemeji yangu alikuwa atoi hata mia pale nyumbani lakini chakula anapelekewa na mke wake jioni anaenda kulala nae.qn to ask hivi ile ilikuwa ndoa au walikuwa wanafanya mapenzi..pia nikumpa huyu shemeji uvivu wa kufikiri kabisa.

Wakuu naombeni ushauri wa mawazo kwani hapa sina mbele wala nyuma najua hapa jf kuwa watu wenye uwezo mkubwa wa kuchambua mambo.ushauri wako utanipanua mawazo yangu nilionaya sasa.

Asanteni na karibuni kwa mawazo.

Pole sana kaka. Nimesoma post yako kwakweli nimesononeka sana kwa hali ilivyo sasa. Unakila sababu ya kuwa mkali na hasira juu ya hili jambo kwasababu dada yako inaonekana anatumiwa tu kama chombo cha starehe.

Kabla ya kuzungumzia namna ambayo tunaweza kumaliza au kupunguza makali ni vyema nikukumbushe vitu vichahache vya msingi.

a) Wewe kama mtoto wa kwanza au kaka, kuwa ukijuwa kwamba hauna mamlaka yeyote kisheria kumfukuza dada yako hapo nyumbani.Hii ni kwasababu wote ni watoto na hapo ni nyumbani kwenu wote. Labda mama yako pekee ndiye anaweza kumfukuza hapo nyumbani. Pia hauna mamlaka ya kupanga nani apewe chakula na nani asipewe.

b)Juwa yakwamba hauna uwezo wowote wakuingilia mahusiano ya dada yako kwasababu yeye ni mtu mzima. Sheria inamruhusu kuwa na uhuru wakuchaguwa mtu yeyote.

c)Pia inaonesha kwamba dada yako hakulipiwa mahali na wala hakuna michakato yeyote ambayo ilifanywa kuhusu ndoa na pande zote mbili.

Nakushauri uwende kwa ndugu wa huyo kijana.Hapa unaweza kutafuta mashangazi au wajomba. wajulishe kwamba familia yenu imeomba mambo yote ya mila yafanyike ikiwemo swala la malipo ya mahali. Unaweza kuweka mahali ndogo tu, lengo hapo nikufanya huyo kijana na familia yake kuwa serious na hiyo ndoa. Nadhani baada ya kukamilisha mambo yote ya ndoa bila shaka utakuwa umemaliza matatizo yote au itakuwa rahisi kuyatatua kupitia kwa wakwe.

Kila la kheri kaka.
 
Nakwambia mimi ningetoa kipigo kikali,kipigo kitakatifu na mama yangu lazima angejua sina adabu.wangenielewa pumbavu zao.
 
Mkuu jitenge kwanza na familia yako,jiweke mbali nao huenda wakapata akili na uelewa.Wakishajua huwataki watakuja na hapo hekima itafuata mkondo.wakikupuuza nawe wapuuze.
 
Pole sana kaka. Nimesoma post yako kwakweli nimesononeka sana kwa hali ilivyo sasa. Unakila sababu ya kuwa mkali na hasira juu ya hili jambo kwasababu dada yako inaonekana anatumiwa tu kama chombo cha starehe.

Kabla ya kuzungumzia namna ambayo tunaweza kumaliza au kupunguza makali ni vyema nikukumbushe vitu vichahache vya msingi.

a) Wewe kama mtoto wa kwanza au kaka, kuwa ukijuwa kwamba hauna mamlaka yeyote kisheria kumfukuza dada yako hapo nyumbani.Hii ni kwasababu wote ni watoto na hapo ni nyumbani kwenu wote. Labda mama yako pekee ndiye anaweza kumfukuza hapo nyumbani. Pia hauna mamlaka ya kupanga nani apewe chakula na nani asipewe.

b)Juwa yakwamba hauna uwezo wowote wakuingilia mahusiano ya dada yako kwasababu yeye ni mtu mzima. Sheria inamruhusu kuwa na uhuru wakuchaguwa mtu yeyote.

c)Pia inaonesha kwamba dada yako hakulipiwa mahali na wala hakuna michakato yeyote ambayo ilifanywa kuhusu ndoa na pande zote mbili.

Nakushauri uwende kwa ndugu wa huyo kijana.Hapa unaweza kutafuta mashangazi au wajomba. wajulishe kwamba familia yenu imeomba mambo yote ya mila yafanyike ikiwemo swala la malipo ya mahali. Unaweza kuweka mahali ndogo tu, lengo hapo nikufanya huyo kijana na familia yake kuwa serious na hiyo ndoa. Nadhani baada ya kukamilisha mambo yote ya ndoa bila shaka utakuwa umemaliza matatizo yote au itakuwa rahisi kuyatatua kupitia kwa wakwe.

Kila la kheri kaka.
Ushauri Kuntu kabisa, NAKAZIA.
 
Back
Top Bottom