Shemeji yangu ni Snitch nifanye nini kumkomesha

Huyu ni mke wa brother wangu kwenye mambo mengine tunaishi fresh tu ila kitu kimoja ananikela ni tabia yake ya usnitc,

Jana nimepigwa kibuti na demu wangu kwa sababu yake ya kutembeza umbea kwa mademu zangu kwamba mimi ni malaya na sometime huwapa location/data kabisa jinsi ya kunifumania,

Kusema kweli nimemchoka sana huyu shemeji yangu kwa tabia yake ya usnitch japo kwenye inshu zingine yuko fair ata ikifika kwenye swala la hela siyo bahili kivile ukiwa na shida anakupiga tafu fresh tatizo huo usnitch tu wakuu,

Nifanye nini nikomeshe hii tabia kwake wakuu.?

Sent using Jamii Forums mobile app
Cha msingi ongeza usiri kwenye mambo yako unayofanya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kajuaje kama uko location flani na demu.? Na pili, kawajuaje mademu zako wote?

Kuna mawili, ama stori ya kufurahisha jukwaa au umesimuliwa ila hukuelewa vizuri!
 
Mkuu, jipange, hama kwa kaka yako, acha kuwa tegemezi, omba omba hawezi kuheshimiwa, kuna siku atakuja kukupiga masingi kabisa mbele ya wavulana wenzako.
 
We kweli ni 0 unaruhusuje ajue mambo yako. Mwanaume huwezi kuwa na privacy.

Acha umbea kumwambia mambo yako ni element za kike

Shida haijirudii
 
Back
Top Bottom